< 歷代志下 20 >

1 [聯軍進襲猶大]此後,摩阿布人、阿孟人,還有一些瑪紅人前來供打約沙法特。
Ikawa baada ya hayo, kwamba watu wa Moabu na Amoni, na pamoja na baadhi ya Wameuni wakaja juu ya Yehoshafati ili kupigana vita. (Mandishi, “baadhi ya Wameuni” yanatoa masahihisho kwa ajili ya maandishi ya Kiebrania, ambayo yanasomeka, “baadhi ya Waamoni”. Inadhaniwa kwamba “Wameuni” ndilo neno la asili, na wenye kunukuu walilibadili kuwa “baadhi ya Waamoni”. Lakaini jina hili la mwisho halileti maana, kwa sababu Waamoni tayari wamekwisha tajwa katika mstri huu. Vile vile, matoleo tofauti tofauti yanajihusha na tatizo hili katika namna mabli mbali)
2 有人來告訴約沙法特說:「由海那邊,由厄東有一支大軍前來攻擊你;他們現已到達哈匝宗塔瑪爾,即恩革狄。」
Kisha baadhi ya watu wakaja wakamwambia Yehoshafati, wakisema, “Umati mkubwa wanakuja juu yako ng'ambo ya Bahari iliyokufa, kutoka Edomu. Ona, wako Hason- tamari”, ambayo ndiyo En-gedi. (Badala ya “Edomu” baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasomeka, “Aramu.”
3 約沙法特害了怕,一面懇求上主,一面宣佈全猶大禁食。
Yehoshafati akaogopa na akajipanga kumtafuta Yahwe. Akatangaza haraka katika Yuda yote.
4 猶大人遂集會,求上主援助;猶大各城的人也前來祈求上主。[約沙法特的禱詞]
Yuda wakakakusanyika pamoja kwa ajili ya kumtafuta Yahwe; wakaja kutoka miji yote ya Yuda kwa ajili ya kumtafauta Yahwe.
5 約沙法特在猶大和耶路撒冷的會眾中,站在上主殿宇的新院前,
Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, kwenye nyumba ya Yahwe, mbele ya kibaraza kipya.
6 說「上主,我們祖先的天主! 你不是天上的天主嗎﹖你不是治理萬國萬民的麼﹖你手中有能力和權威,沒有誰能抵抗你。
Akasema, “Yahwe, Mungu wa babau zetu, hauko mbinguni? Wewe siyo mtawala juu ya falame zote za mataiafa? Nguvu na uweza viko mkononi mwako, kwa hiyao hakuna anayeweza akukupinga wewe.
7 我們的天主! 不是你將這地方的居民,在你百姓以色列面前趕走,將這地方永遠賜給了你友人亞巴郎的後代嗎﹖
Munagu wetu, Hukuwafuaakuja nje wakaaji wa nchi hii mbe ya watau watau wakop Israeli, na kuitoa milele kwa ajili ya uzaoa wa Abrahamu?
8 他們現在住在這地方,並在這地方為你的名建造了聖殿說:
Wakaishi ndani yake na kujenga sehemu takatifu kwa ajili ya jina lako, wakisema,
9 如果我們遭遇了禍患,刀兵災害,或瘟疫饑饉,我們站在這殿前和你面前,在災難中向你呼籲,你必予以垂聽,施行拯救,因為你的名在這殿內。
'Ikiwa janga litakuja juu yetu —upanga, hukumu, au ugonjwa, au njaa—tutasimama mbele ya nyumba hii, na mbele zako (kwa maana jina lako limo ndani ya nyumba hii), na tutakulilia wewe katika mateso yetu, na utatusikia na kutuokoa.' (Badala ya “hukumu” baadhi ya maandiko ya zamani yanasema “mafuriko”).
10 現在你看,阿孟人、摩阿布人以及色依爾山中的人,這些人是以色列出離埃及時,你曾禁止以色列侵犯,以色列便繞道遠離,未加消滅的人。
Tazama sasa, hapa kuna watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri ambao hukuwaacha Israeli wawapige waalipotoka nchi ya Misri; badala yake, Israeli waliwageukia mbali na hawakuwaangamiza.
11 你看他們如何報復我們要來驅逐我們離開你賜予我們為基業的地方。
Ona jinsi wanavyotuzawadia; wanakuja kutotoa nje ya nchi yako mbayo umetupa kuirithi.
12 我們的天主,你不懲罰他們麼﹖我們實在沒有力量抵抗來攻擊我們的這支龐大的軍隊,我們也不知道該作什麼,我們的眼睛惟有仰望你。」
Mungu wetu, hutawahukumu? Kwa maana hatuna nguvu dhidi ya hili jeshi kubwa ambalo linakuja juu yetu. hatujui cha kufanya, lakini macho yetu yako kwako.
13 當時全猶大民眾,連他們全家妻子兒女,都立在上主面前。[先知預報勝利]
Yuda wote wakasimama mbele ya Yahwe, pamoja na wadogo wao, wake, na watoto.
14 上主的神在會眾中臨於肋未人阿撒夫的後裔,瑪塔尼雅的玄孫,耶依耳的曾孫,貝納雅的孫子,則加黎雅的兒子雅哈齊耳身上,
Kisha kati kati ya kusanyiko, roho ya Yahwe ikaja juu ya Yahazieli, mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, mwana, Mlawi, mmoja wa wana wa Asafu.
15 他遂說:「全猶大人耶路撒冷的居民以及約沙法特王,都要靜聽! 上主這樣對你們說:你們不要為這支龐大軍隊害怕,因為戰爭不在乎你們,而在乎天主。
Yahazieli akasema, “Sikilizeni, Yuda wote na ninyi wakaaji wa Yerusalemu, na Mfalme Yehoshafati. Hivi ndivyo Yahwe asemavyao kwenu, 'Msiogope: msivunjike moyo kwa sababu ya hili jeshsi kubwa, kwa maana vita siyo yenu, bali ni ya Mungu.
16 明天你們要下去迎敵,他們要由漆茲山坡上來,你們要在耶魯耳曠野前的谷口遇到他們。
Lazima muende chini juu ya yao kesho, Ona, wanakuja wakipanda kupia njia ya Sisi. Mtawakuta mwishono mwa bondo, mbele ya jangwa la Yerueli.
17 這次你們無須交戰,只須佈陣以待,觀看上主為你們所行的救援。猶大和耶路撒冷,不必畏懼,不必害怕! 明天你們只管出去迎敵,因為上主與你們同在。」
Hamtahitaji kupigana katika vita hii. Simameni katika nafasi zenu, simameni wima, na muone wokovu wa Yahwe pamoja nanyi, Yuda na Yerusalemu. Msiogope wala kukata tamaa. Tokeni nje juu yao kesho, kwa maana yuko pamoja nanyi.”
18 約沙法特遂俯首至地,猶大民眾和耶路撒冷居民也都俯伏在上主面前,朝拜上主。
Yehoshafati akainamisha kichwa chake pamaoja na uso wake chini. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakaanguka chini mbele za Yahwe, wakimwabudu yeye.
19 刻哈特子孫和科辣黑子孫中的肋未人起立,引吭高歌,讚頌上主以色列的天主。[凱旋歸來]
Walawi, wale wa uzao wa Wakohathi na wa uzao wa Wakorahi, wakasimama juu kumsifu Yahwe, Mungu wa Israeli, kwa sauti kubwa sana.
20 次日,他們一早就起來,開往特科亞曠野;在出發時,約沙法特立起來說:「猶大和耶路撒冷的居民,請聽我的話! 你們信賴上主你們的天主,必保生命;相信他的先知,必定勝利。」
Asubuhi mapema wakasimama na kwenda nje kwenye bonde la Tekoa. Walipokuwa wakienda nje, Yehoshafati akasimama na kusema, “Nisikilizeni, Yuda, na nnyi wakaaji wa Yerusalemu! Aminini katika Yahwe Mungu wenu, na mtasaidiwa. Aminini katika manabii zake, na mtafanikiwa.
21 他與百姓商定之後,便派歌詠人員讚頌上主,身穿聖潔服裝,走在軍隊面前,歌頌說:「你們應讚頌上主,因為他的慈愛永遠常存! 」
Alipokuwa ameshauriana na watu, akawachagaua wale ambao wangemwimbia Yahwe na kumpa sifa kwa ajili ya utukufu wake mtakatifu, walipokuwa wakienda wakilitangulia jeshi, na kusema, “Mshukuruni Yahwe, kwa maana uaminifu wa aganao lake unadumu milele.”
22 他們正歌詠讚美時,上主派出伏兵,襲擊了那些來攻擊猶大的阿孟人、摩阿布人和色依爾山地的居民;他們便被擊敗了。
Walipoanza kuimba na kusifu, Yahwe akapanga wanaume katika mavamizi juu ya watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri, ambao walikuwa wanakauja dhidi ya Yuda. Walishindwa.
23 阿孟人和摩阿布人起來攻擊色依爾山地的居民,決心將他們殺盡滅絕;殲滅了色依爾山地居民以後,他們又自相殘殺。
Kwa maana watu wa Aamoni na Moabu walisimama kupigana na wakaaji wa Mlima Seiri, ili kuwaua kabisa na kuwangamiza. Waliapokuwa wamemaliza kuwaangamiza wakaaji wa Mlima Seiri, wote wakasaidiana kuangamizana kila mmoja.
24 猶大人到了俯瞰曠野的高崗上,觀望大軍,見伏屍遍野,沒有一個逃脫的。
Yuda walipokuwa katika sehemu hiyo wakiangalia jangwani, waliangalia nje juu ya jeshi. Tazama, walikuwa wamekufa, wameanguka chini; hakuna aliyekuwa amepona.
25 約沙法特遂帶他的軍民去掠奪敵人的財物,見有大批的牲畜、財物、衣服和寶物;足足掠取了三天,奪得的財物多得不能攜帶,因為實在太多。
Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara kutoka kwa hao watu, walikuta miongoni mwao bidhaa nyingi, nguo, na johari za thamani, ambazo walizichukua kwa ajili yao wenyewe, nyingi kuliko uwezo wao wa kubeba. Iliwachukua siku tatu kusomba nyara hizo, zilikuwa nyingi sana. (Badala ya “miongoni mwao”, baadhi ya maandishi ya zamani na ya kisasa yanasema, “ng'ombe.” badala ya “nguo” baadhi ya maandiko ya kale na ya kisasa yanasema, “miili iliyokufa”).
26 第四天,他們聚集在巴辣加谷,在那裏讚頌了上主,為此給那地起名叫巴辣加谷,直到今天。
Katika siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka, Huko wakamsifu Yaahwe, kwa hiyo jina la sehemu hiyo hata leo ni “Bonde la Baraka”.
27 此後,猶大和耶路撒冷所有的軍民,由約沙法特率領,凱旋回了耶路撒冷,因為上主使他們戰勝仇敵,因而異常歡樂,
Kisha, wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati katika uongozi wao, kwenda tena Yerusalemu kwa furaha, kwa maana Yahwe alikuwa amewafanya wafurahie juu ya adui zao.
28 都彈著琴,鼓著瑟,吹著號,來到耶路撒冷,進了上主的殿。
Wakaja Yerusalemu na kwenye nyumba ya Yahwe kwa vinanda, vinubi na matarumbeta.
29 列國的民族一聽說上主擊敗了以色列的敵人,都對天主起了恐怖的心。
Hofu ya Yahwe ikawa juu ya falme zote za mataifa waliposikia kwamba Yahwe amepigana dhidi ya adui wa Israeli.
30 約沙法特的王國於是獲享太平,因為上主賜給他四境平安。[對約沙法特的短評]
Kwa hiyo ufaleme wa Yehoshafati ulikuwa mtivu, kwa maana Mungu wake alimpa amani kuzungunga pande zake zote.
31 約沙法特為猶大王,即位時年三十五歲,在耶路撒冷為王凡二十五年;他的母親名叫阿組巴,是史肋希的女兒。
Yehoshafati akatawala juu ya Yuda: Alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala. Jina la mama yke aliitwa Azubahi, binti wa Shilhi.
32 約沙法特走了他父親阿撒的道路,未偏左右,行了上主視為正義的事;
Akatembea katika njia za Asa, baba yake; hakugeka popote kuziacha; akafanya yaliyo mema katika macaho ya Yahwe.
33 只是丘壇沒有剷除,人民仍沒有全心全意歸向他們祖先的天主。
Vile vile, sehemu za juu hazikuwa zimeondoshwa mbali. Watu walikuwa bado hawajaelekeza mioyo yao kwa Mungu wa babu zao.
34 約沙法特前後其餘的事蹟,都記載在哈納尼之子耶胡的言行錄上這言行錄收集在以色列列王實錄內。[船遭破毀]
Kwa mambo mengine kuhusu Yehoshafati, mwanzo na mwisho, tazama, yameandikwa katika historia ya kitabu cha wafalme wa Israeli.
35 此後,猶大王約沙法特與作惡多端的以色列王阿哈齊雅聯盟,
Baada ya hayo, Yehoshafati, mfalme wa Yuda, akapatana na Ahazia, mfalme wa Israeli, ambaye alitenda uovu mwingi.
36 合夥製造船隻,開往塔爾史士去;他們合力在厄茲雍革貝爾製造了一些船。
Akapatana naye kujenga meli za kwenda Tarshishi; Wakazijenga meli hizo huko Esion-geberi.
37 瑪勒沙人多達瓦的兒子厄里厄則爾講預言攻擊約沙法特說:「因為你與阿哈齊雅聯盟,上主必要破壞你所造的船隻。」後來那些船隻果然遭受破壞,未能開往塔爾史士。
Kisha Eliezeli, mwana wa Dadavahu wa Maresha, akatoa unabii juu ya Yehoshafati; akasema, “kwa sababu umepatana na Ahazia, Yahwe ameiharibu miradi yako.” Meli zilivunjika ili kwamba zisiweze kusafiri.

< 歷代志下 20 >