< 撒母耳記上 11 >

1 大約過了一個月,阿孟人納哈士上來圍困基肋阿得的雅貝士,雅貝士所有的居民對納哈士說:「你與我們立約,我們就服事你。」
Ndipo Nahashi Mwamoni akaenda na kupiga kambi kuzunguka Yabeshi Gileadi. Watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, “Fanya mkataba nasi, na tutakutumikia,”
2 阿孟人納哈士回答他們說:「在這條件下,我纔與你們立約:就是剜出你們各人的右眼,我要藉此羞辱全以色列。」
Nahashi Mwamoni akawajibu, “Kwa sharti hili nitafanya mkataba na ninyi, kwamba wote niwang'oe macho ya kulia, na kwa kitendo hiki kilete fedheha katika Israeli yote.”
3 雅貝士的長老回答他說:「請讓我們休戰七天,我們派人到以色列全境去,如果沒有人來救我們,我們就向你投降。
Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, “Tuache kwa siku saba, ili tuwatume wajumbe katika nchi yote ya Israeli. Ndiposa, kama hakuna mtu wa kutuokoa, tutasalimu amri kwako.”
4 使者到了撒烏耳的基貝亞,就把這事講給民眾聽,民眾遂放聲大哭。
Nao wajumbe wakafika Gibea, alipoishi Sauli, na wakawaeleza watu kile kilichotokea. Watu wote wakalia kwa sauti kuu.
5 那時撒烏耳正跟著牛從田間回來,便問說:「民眾有什麼事,如此號淘大哭﹖」人們就把雅貝士人的話講給他聽。
Na Sauli alikuwa akiwafuata nyuma maksai kutoka shambani. Sauli akauliza, “Watu wamepatwa na nini hadi wanalia?” Ndipo wakamweleza Sauli kile ambacho watu wa Yabeshi walikisema.
6 撒烏耳一聽說這些話,上主的神便降在他身上,遂勃然大怒,
Sauli aliposikia kile walichosema, Roho ya Mungu ikamjia kwa nguvu, na akakasirika.
7 立即牽了一對牛來,剖分成塊,託使者分送到以色列全境說:「凡不隨從撒烏耳如撒慕爾出征的,也必這樣對待他的牛! 」上主的驚嚇降在民眾身上,因而他們好像一個人一齊出征。
Akashika nira ya maksai, akawakata hao ng'ombe vipande vipande, na akavituma hivyo vipande katika nchi yote ya Israeli kwa kuwatumia wajumbe, Akasema, “Yeyote asiyejitokeza akimfuata Sauli na Samweli, hivi ndivyo ng'ombe wake watakavyofanywa.” Na hofu ya BWANA ikawaingia watu, na wakajitokeza wote kwa pamoja.
8 撒烏耳在貝則克檢閱了他們;以色列人共三十萬,猶大人三萬。
Alipowahesabu hapo Beseki, watu wa Israeli walikuwa elfu mia tatu, na watu wa Yuda elfu thelathini.
9 撒烏耳對來的使者說:「你們這樣對基肋阿得的雅貝士人說:明天太陽正熱時,救援就必達到你們那裏。」使者便回去,向雅貝士人報告,他們都很喜歡。
Wakawaambia wale wajumbe waliotumwa, “Mtawaambia watu wa Yabeshi Gileadi, 'Kesho, wakati wa jua kali, Mtaokolewa.”' Basi wale wajumbe wakaenda na kuwaambia watu wa Yabeshi, na watu wakafurahi.
10 雅貝士人遂對阿孟人說:「明天我們向你們投降,你們看著怎樣好,就怎樣對待我們罷!
Ndipo watu wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, “Kesho tutasalimu amri kwako, na utaweza kutufanyia chochote unachoona kinakupendeza.”
11 第二天撒烏耳把民眾分作三隊,在黎明以前衝入了阿孟人營中,擊殺他們一直到日中最熱的時候;剩下的人都逃散了,以至沒有兩人在一起。
Siku iliyofuata Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu. Wakafika katikati ya Kambi wakati wa asubuhi, wakawashambulia na kuwashinda Waamoni ilipofika mchana. Waliosalimika nao walitawanyika, kiasi kwamba hata watu wawili hawakuachwa pamoja.
12 民眾於是對撒慕爾說:「誰曾說過:撒烏耳豈能作我們的君王﹖把這些人交出來,讓我們處死他們! 」
Ndipo watu wakamwambia Samweli, “Wako wapi waliosema, 'Hivi kweli Sauli atatutawala?' Walete watu hao, ili tuwauwe.”
13 撒烏耳回答說:「今天不可處死任何人,因為今天上主在以色列中施行了救恩。」
Lakini Sauli akasema, “Hakuna atakayeuwawa siku ya leo, kwa sababu leo BWANA amemuokoa Isreli.”
14 撒慕爾以後對民眾說:「來,我們到基耳加耳去,在那裏重新建立王國。」
Kisha Samweli akawaambia watu, “Njoni, twendeni Gilgali na tuimarishe ufalme tena huko.”
15 民眾便都去了基耳加耳,在那裏於上主面前立撒烏耳為王,並給上主奉獻了和平祭;撒烏耳同全體以色列人舉行了盛大的盛會。
Hivyo watu wote wakaenda Gilgali na wakamsimika Sauli kuwa mfalme mbele za BWANA huko Gilgali. Na huko walitoa sadaka za amani mbele za BWANA, na watu wote wa Israeli wakafurahi sana.

< 撒母耳記上 11 >