< 約翰一書 5 >

1 凡信耶穌為默西亞的,是由天主所生的;凡愛生他之父的,也必愛那由他所生的。
Yeyote anayeamini kuwa Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na yeyote ampendaye yeye ambaye ametoka kwa Baba pia huwapenda watoto wake.
2 幾時我們愛天主,又遵行他的誡命,由此知道我們真愛天主的子女。
Kwa hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu — tunapompenda Mungu na kutekeleza amri zake.
3 原來愛天主,就是遵行他的誡命,而他的誡命並不沉重,
Hivi ndivyo tunavyompenda Mungu kwamba twazishika amri zake. Na amri zake ni nyepesi.
4 因為凡是由天主所生的,必得勝世界;得勝世界的勝利武器,就是我們的信德。
Kwa kuwa kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Na huu ndio ushindi wa kuushinda ulimwengu, imani yetu.
5 誰是得勝世界的呢?不是那信耶穌為天主子的人嗎?
Ni nani aliyeushinda ulimwengu? Ni yule aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.
6 這位就是經過水及血而來的耶穌基督,他不但以水,而且也是以水及血而來的;並且有聖神作證,因為聖神是真理。
Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu- Yesu Kristo. Hakuja tu kwa maji bali kwa maji na damu.
7 原來作證的有三個:
Kwa kuwa kuna watatu washuhudiao:
8 就是聖神,水及血,而這三個是一致的。
Roho, maji na damu. Hawa watatu hukubaliana. (Zingatia: Maneno haya “Baba, Neno, na Roho Mtakatifu” hayaonekani katika nakala bora za kale).
9 人的證據,我們既然接受,但天主的證據更大,因為天主的證據就是他為自己的子作證。
Kama tunaupokea ushuhuda wa wanadamu ushuhuda wa Mungu ni mkuu kuliko huo. Kwa kuwa ushuhuda wa Mungu ni huu- kwamba anao ushuhuda kuhusiana na Mwanawe.
10 那信天主子的,在自己內就懷有這證據;那不信天主的,就是以天主為撒謊者,因為他不信天主為自己的子所作的證。
Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu ana ushuhuda ndani yake mwenyewe. Na yeyote asiye mwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu ameuleta kuhusu Mwanawe.
11 這證據就是天主將永遠的生命賜給了我們,而這生命是在自己的子內。 (aiōnios g166)
Na ushuhuda ndio huu — kwamba Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huu umo ndani ya Mwanawe. (aiōnios g166)
12 那有子的,就有生命;那沒有天主子的,就沒有生命。
Aliye naye Mwana ana uzima. Asiyekuwa naye Mwana wa Mungu hana uzima.
13 我給你們這些信天主子名字的人,寫了這些事,是為叫你們知道:你們已獲有永遠的生命。 (aiōnios g166)
Nimewaandikia haya mweze kujua kwamba mnao uzima wa milele — ninyi mnaoamini katika jina la Mwana wa Mungu. (aiōnios g166)
14 我們對天主所懷的依恃之心就是:如果我們按他的旨意求什麼,他必俯聽我們。
Na huu ndio ujasiri tulionao mbele zake, kwamba kama tukiomba kitu chochote sawa sawa na mapenzi yake, hutusikia.
15 我們既然知道:我們不拘向他祈求什麼,他會俯聽我們,我們也知道向他所祈求的,必要得到。
Na kama tunajua kwamba hutusikia — chochote tumwombacho tunajua kwamba tunacho hicho tulichomwomba.
16 誰若看見自己的弟兄犯了不至於死的罪,就應當祈求,天主必賞賜他生命:這是為那些犯不至於死的罪人而說的;然而有的罪卻是至於死的罪,為這樣的罪,我不說要人祈求。
Kama mtu amwonaye ndugu yake anatenda dhambi isiyopelekea kifo, yampasa kuomba na Mungu atampa uzima. Ninasema kwa wale ambao dhambi yao ni ile isiyopelekea kifo — Kuna dhambi ipelekeayo kifo — sisemi kwamba anapaswa kuomba kwa ajilli ya dhambi hiyo.
17 任何的不義都是罪過,但也有不至於死的罪過。
Uasi wote ni dhambi — lakini kuna dhambi isiyopelekea kifo.
18 我們知道:凡由天主生的,就不犯罪過;而且由天主生的那一位必保全他,那惡者不能侵犯他。
Tunajua ya kuwa aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi. Bali aliyezaliwa na Mungu hutunzwa naye salama daima, na yule mwovu hawezi kumdhuru.
19 我們知道我們屬於天主,而全世界卻屈服於惡者。
Tunajua kuwa sisi ni wa Mungu na tunajua kwamba ulimwengu wote uko chini ya utawala wa yule mwovu.
20 我們也知道天主子來了,賜給了我們理智,叫我們認識那真實者;我們確實是在那真實者內,即在他的子耶穌基督內,他即是真實的天主和永遠的生命。 (aiōnios g166)
Lakini twajua kwamba Mwana wa Mungu amekuja na ametupatia ujuzi, kwamba tunamjua yeye aliye kweli na kwamba tumo ndani yake yeye aliye kweli, hata katika Mwanawe Yesu Kristo. Ni Mungu wa kweli na uzima wa milele. (aiōnios g166)
21 孩子們,你們要謹慎,遠避偶像!
Watoto wapenzi, jiepusheni na sanamu.

< 約翰一書 5 >