< 歷代志上 7 >

1 [依撒加爾的後代]依撒加爾的兒子:托拉、普瓦、雅叔布和史默龍四人。
Isiakari alikuwa na wana wanne Tola, Pua, Yashubi, na Shimironi.
2 托拉的子孫:烏齊、勒法雅、耶黎耳、雅赫買、依貝散和舍慕耳,都是托拉家族的族長,英勇的戰士;再達味時代,依他們的家系,人數有二萬二千六百。
Wana wa Tola walikuwa Uzi, Refaia, Yerie, Yamai, Ibisami, Shemueli. Walikua vichwa katika nyumba za baba yao, toka uzao wa Tola na waliorodheshwa kama mashujaa hodari miongoni mwa kizazi chao. Katika siku za Daudi walikua na idadi ya 22, 600.
3 烏齊的兒子依次辣希雅;依次辣希雅的兒子:米加耳、敖巴狄雅、約厄耳和依史雅......五人,┬歐是族長。
Mwana wa Uzi alikua Izrahia. Mwana wake alikua Michaeli, Obadia, Yoeli, na Ishia, wote watano walikua viongozi wa ukoo
4 按家系和家族歸屬於他們的,尚有三萬六千出征的戰士;因為他們有很多婦女和兒童。
Pamoja nao walikua na jeshi la watu elfu thelathini na sita kwa mapambano, Kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao, kwa kuwa walikuwa na wake wengi pamoja na wana.
5 連他們的兄弟,即全依撒加爾支派中的英勇的戰士,登記的人數,共計八萬八千。[本雅明的後代]
Kaka zao, kabila la Isakari, walikua na wanaume wa vita themanini na saba, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao.
6 本雅明的兒子:貝拉貝革爾、耶狄厄耳三人。
Wana watatu wa Benjamini walikuwa Bela, Beka, na Yediaeli.
7 貝拉的兒子:厄茲朋、烏齊、烏齊耳、耶黎摩特和依黎五人,都是家族的族長;英勇的戰士,按家族統計,共計二萬二千三十四人。
Wana watano wa Bela walikuwa Ezibono, Uzi, Uzieli, Yerimoti, na Iri. Walikua ni wanajeshi na waanzilishi wa koo. Watu wao walikuwa na idadi ya wanaume wa vita 22, 034, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao.
8 貝革爾的兒子:則米辣、約阿士、厄里厄則爾、厄里約乃、敖默黎、耶肋摩特、阿彼雅、阿納托特和阿拉默特:以上是貝革爾的兒子,
Wana wa Beka walikuwa Zemira, Yoashi, Elieza, Elionai, Omri, Yeremoti, Abiya, Anatoti, na Alemeti. Wote hawa walikuwa wana wake.
9 是家族的族長;英勇的戰士,按家族統計共計二萬二百人。
Orodha ya koo zao ilikua na idadi ya 20, 200 viongozi wa familia na wanaume wa vita.
10 耶狄厄耳的兒子彼耳漢;彼耳漢的兒子:耶烏士、本雅明、厄胡得、革納阿納、則堂塔爾史士和希沙哈爾:
Mwana wa Yediaeli alikuwa Bilhani. Wana wa Bilhani walikuwa Yeushi, Benjamini, Ehudi, Kenaana, Zetani, Tarishishi, na Ahishahari.
11 以上是耶狄厄耳的子孫,家族的族長;英勇的戰士能上陣作戰的,有一萬七千二百人。
Wote hawa waikuwa wana wa Yediaeli. Waliorodheshwa katika ukoo orodha ilikuwa 17, 200 viongozi na wanaume wa vita imara kwa kazi ya jeshi.
12 依爾的兒子叔平和胡平;阿赫爾的兒子胡生。納斐塔里支派
(Shupimu na Hupimu walikuwa wana wa Iri, na Hushimu alikuwa mwana wa Aheri.)
13 納斐塔里的兒子:雅赫則耳、古尼、耶則爾、沙隆:是彼耳哈的子孫。[默納協支派]
Wana wa Naftali walikuwa Yazieli, Guni, Yezeri, na Shalumu. Hawa walikuwa wajukuu wa Bilhahi.
14 默納協的兒子:馬基爾,是他的一個阿蘭妾給他生的;瑪基爾是基肋阿得的父親。
Manasse alikua na mtoto wa kiume aliitwa Asrieli, Ambaye suria wake wa Kiaramia alimzalia. Pia alimzaa na Makiri, baba wa Gileadi.
15 瑪基爾娶了妻,妻名叫瑪阿加,她的姊妹名叫責羅斐哈得,她只有女兒。
Makiri alimchukua mke wake kutoka Hupite na Shupite. Jina la dada yake lilikuwa Maaka. Mwingine wa uzao wa Manasse alikuwa Zalofehadi, ambaye alikuwa na mabinti pekee.
16 瑪基爾的妻子瑪阿加生了一個兒子,給他起名叫培勒士;他的兄弟名叫舍勒士。舍勒士的兒子:烏藍和勒耿。
Maaka mke wa Makiri, alimzaa mwana na alimuita Pereshi. Kaka yake aliitwa Shereshi, na wana wake walikuwa Ulamu na Rakemu.
17 烏藍的兒子貝丹:以上是默納協的子孫,瑪基爾的兒子基肋阿得的子孫。
Mwana wa Ulami alikuwa Bedani. Hawa walikuwa uzao wa Gileadi mwana wa Makiri mwana wa Manase.
18 他的姊妹摩肋革特生依市曷得、阿彼厄則爾和瑪赫拉。
Dada wa Gileadi Hamoleketi alimzaa Ishihodi, Abi Ezeri, na Mahila.
19 舍米達的兒子:阿希楊、舍根、里刻希和阿尼罕。[厄弗辣因支派]
Wana wa Shemida walikuwa Ahiana, Shekemu, Liki, na Aniamu.
20 厄弗辣因的兒子:叔特拉;叔特拉的兒子貝勒得,貝勒得的兒子塔哈特,塔哈特的兒子厄拉達,厄拉達的兒子塔哈特,
Uzao wa Efraimu ulikuwa kama ifuatavyo: Efraimu mwana wa Shutela. Shutela mwana wa Beredi. Beredi mwana wa Tahati.
21 塔哈特的兒子匝巴得。厄弗辣因的兒子叔特拉和厄則爾以及厄拉得,為加特的土人所殺,因為他們下去劫掠土人的牲畜。
Tahati mwana wa Eleada. Eleada mwana wa Shutela. (Eza na Eleadi waliuawa na wanaume wa Gati, wenyeji wa nchi, walipoenda kuiba mifugo yao.
22 他們的父親厄弗辣因哀悼他們多日,他的兄弟們也來慰弔。
Efraimu baba yao aliomboleza kwa siku nyingi, na kaka zake walikuja kumfariji.
23 以後,他又走近了自己的妻子,她懷孕生了一個兒子,給他起名叫貝黎雅說:「我家遭過患難。」
Alilala na mkewe. Akapata mimba akamzaa mwana. Efraimu akamuita Beria, kwa sababu maafa yalishakuja nyumbani mwake.
24 他的女兒舍厄辣建立了上下貝特曷龍和烏曾舍厄辣。
Binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga miji juu na chini Beth Horon na Uzzen Sheerah.)
25 貝黎雅的兒子勒法黑,勒法黑的兒子勒舍夫,勒舍夫的兒子特拉黑,特拉黑的兒子塔罕,
Mwana wake alikuwa Rafa. Mwana wa Rafa alikuwa Reshefi. Mwana wa Reshafi alikuwa Tela. Mwana wa Tela alikuwa Tahani.
26 塔罕的兒子拉丹,拉丹的兒子阿米胡得,阿米胡得的兒子厄里沙瑪,
Mwana wa Tahani alikuwa Ladani. Mwana wa Ladani alikuwa Amihudi. Mwana wa Amihudi alikuwa Elishama.
27 厄里沙瑪的兒子農,農的兒子若蘇厄。
Mwana wa Elishama alikuwa Nuni. Mwana wa Nuni alikuwa Joshua.
28 他們佔據和居留的地方:貝特耳和所屬村鎮,往東有納阿郎,往西有革則爾和所屬村鎮,舍根和所屬村鎮,直到阿雅和所屬村鎮。
Mali zao na makazi yao yalikuwa Betheli na yalizungukwa na vijiji. Waliongeza upande wa mashariki hadi Naarani na upande wa magharibi hadi Gezeri na vijiji vyake, na Shekemu na vijiji vyake hadi Aya na vijiji vyake.
29 在默納協子孫手中的,有貝特商和所屬村鎮,塔納客和所屬村鎮,默基多和所屬村鎮,多爾和所屬村鎮:以色列的兒子若瑟的子孫住在以上各地。[阿協爾支派]
Katika mipaka pamoja na Manasse kulikuwa na Beti shani na vijiji vyake, Taanaki na vijiji vyake, Megido na vijiji vyake, na Dori na vijiji vyake. Katika huu mji waliishi uzao wa Josefu mwana wa Israeli.
30 阿協爾的兒子:依默納、依市瓦、依市偉和貝黎雅,和他們的姊妹色辣黑。
Wana wa Asha walikuwa Imna, Ishiva, Ishivi, na Beria. Sera alikuwa dada yao.
31 貝黎雅的兒子:赫貝爾和瑪耳基耳,後者是彼爾匝依特的父親。
Wana wa Beria walikuwa Heberi na Malchieli, Ambaye alikuwa baba wa Birzaiti.
32 赫貝爾生雅費肋特、芍默爾、曷堂和他們的姊妹叔亞。
Wana wa Heberi walikuwa Yafeti, Shomer, na Hotamu. dada yao alikuwa Shua.
33 雅費肋特的兒子:帕撒客、彼默哈耳和阿市瓦特:以上是雅費肋特的兒子。
Wana wa Yafeti walikuwa Pasach, Bimhali, na Ashivati. hawa walikuwa watoto wa yafeti.
34 他兄弟芍默爾的兒子:洛赫加、胡巴和阿蘭。
shoma, kaka wa Yafeti alikuwa na wana hawa: Roga, Yehuba, Aram.
35 他兄弟曷堂的兒子:祚法黑、依默納、舍肋士和阿瑪耳。
Kaka yake Shema, Helemu, alikuwa na wana hawa: Zofa, Imna, Sheleshi na Amali.
36 祚法黑的兒子:穌亞、哈爾乃費爾、叔阿耳、黎依默辣、
Wana wa Zofa walikuwa Sua, Harinefa, Shua, Beri, IMra,
37 貝責爾、曷得、沙瑪、史耳沙、耶特爾和貝厄辣。
Beza, Hodi, Shamma, Shilsha, Ithrani, na Beera.
38 耶特爾的兒子:耶孚乃、丕斯帕和阿辣。
Wana wa Yeta walikuwa Jefune, Pispa, na Ara.
39 烏拉的兒子:阿辣黑、哈巴耳和黎茲雅:
Wana wa Ulla walikwa Ara, Hannieli, na Rizia.
40 以上全是阿協爾的子孫,家族出名的族長,英勇的戰士,傑出的將領;能上陣打仗的登記人數,共計二萬六千。
Hawa wote walikuwa uzao wa Asha. Walikua mababu wa ukoo, viongozi wa familia, wananume wa kipekee, wanaume wa vita, na machifu kati ya viongozi. Kulikuwa na wanaume elfu ishirini na sita walioorodheshwa waliokuwa imara kwa kazi ya jeshi, kwa mujibu wa idadi iliyo orodheshwa.

< 歷代志上 7 >