< 歷代志上 11 >

1 [達味為王]那時,全以色列人聚集到赫貝龍,來見達味說:「看,我們都是你的骨肉。
Kisha Waisraeli wote walikuja Hebroni kwa Daudi na kusema, “Angalia, sisi ni nyama na mifupa yako.
2 以前連撒烏耳為王時,也是你率領以色列出入征討;並且上主你的天主,也曾對你說過:你應牧養我的百姓以色列,作我的百姓以色列的領袖。」
Katika wakati uliopita, Sauli alipoo kuwa mfalme juu yetu, ni wewe uliye ongoza jeshi la Israeli. Yahweh Mungu wako alisema kwako, 'utawachunga watu wangu wa Isaraeli, na utakuwa mtawala wa watu wangu wa Israeli”'.
3 以色列所有的長老都到赫貝龍來見君王,達味就在赫貝龍,在上主面前同他們立了約;他們便按照上主藉撒慕爾所吩咐的,給達味傅油,立他為以色列王。[佔領耶路撒冷]
Kwaiyo wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni, na Daudi akafanya agano nao mbele ya Yahweh. Wakampaka mafuta Daudi kuwa mfalme wa Israeli. Kwa namna hii, neno la Yahweh lilo nenwa na Samweli likawa kweli.
4 達味和全以色列人便向耶路撒冷,即耶步斯進發,當時住在那地方的是耶步斯人。
Daudi na Israeli yote wakaenda Yerusalemu (yani, Yebusi). Sasa Wayebusi, wakazi wa nchi, walikuwa pale.
5 耶步斯的居民對達味說:「你決攻不進此地。」但是,達味卻佔領了熙雍山堡,即今達味城。
Wakazi wa yebusi wakamwabia Daudi, “Hautakuja humu.” Lakini Daudi alichukuwa ngome ya Sayuni, mji wa Daudi.
6 達味曾說過:「誰首先擊敗耶步斯人,誰將升為將領和元帥。」責魯雅的兒子約阿布首先上去了,所以他成了元帥。
Daudi alisema, “Yeyote atakaye washambulia Wayebusi wa kwanza atakuwa mkuu wa jeshi” kwaiyo Yoabu mwana wa Zeruia akashambulia wa kwanza, hivyo akafanywa mkuu wa jeshi.
7 達味便住在那山堡內,因此人稱之為達味城。
Daudi akaanza kuishi katika hiyo ngome. Kwaiyo wakaiita mji wa Daudi.
8 達味又重修四周城垣,從米羅起,重修一週;城的其餘部份由約阿布修建。
Akaimarisha mji kutoka Milo na hadi mpaka ukuta unao zunguka. Yoabu akaimairisha mji wote uliyo baki.
9 達味日漸強盛,萬軍的上主與他同在。[達味的將士名單]
Daudi akawa mkuu na mkuu kwa sababu Yahweh wa Majeshi alikuwa naye.
10 以下這些人,是極力擁護達味建國,與全以色列人照上主對以色列所吩咐的,立他為王的主要將士。
Hawa walikuwa viongozi Daudi aliyo kuwa nao, waliyo jionyesha imara katika ufalme wake, pamoja na Israeli, kumfanya mfalme, kutii neno la Yahweh kuhusu Israeli.
11 達味的將士名單如下:哈革摩尼的兒子依市巴耳,是三傑之首;一次他曾舉起長矛,擊殺了三百人。
Hii ni orodha ya wanajeshi shupavu wa Daudi. Yashobeami, mwana wa Mhakimoni, alikuwa mkuu wa kikosi cha thelathini. Aliwaua wanaume mia tatu na mkuki wake katika sehemu moja.
12 次為阿曷亞人多多的兒子厄肋阿匝爾,三傑之一,
Baada ya yeye alikuwa Eleazari mwana wa Dodo, Mahohi, aliyekuwa mmoja wa wanaume watatu hodari.
13 他以前同達味在帕斯達明,培肋舍特人正在那裏集合準備交戰時,【以色列人退卻,他卻固守陣地,擊殺培肋舍特人,直到他手軟無力,粘在刀柄上。上主在那一天完成了一大勝利;民眾返回,隨著他去搶戰利品。再其次是哈辣黎人厄拉的兒子沙瑪,那時培肋舍特人在肋希集合,】在那裏有一塊長滿大麥的田地,民眾由培肋舍特人面前逃走,
Alikuwa na Daudi huko Pasidamimu, na pale Wafilisti wakakusanyika pamoja kwa mapambano, ambapo palikuwa na uwanja wa ngano na jeshi liliwakimbia Wafilisti.
14 他卻立在田間保護了那塊田地,殺敗了培肋舍特人,如此上主又完成了一次大勝利。
Walisimama katikati ya uwanja. Wakautetea na kuwakata Wafilisti na Yahweh akawaokoa na ushindi mkubwa.
15 一次三十勇士中,有三位下到阿杜藍山砦附近的岩石裏去見達味,那時培肋舍特人正紮營在勒法因平原,
Kisha watatu wa viongozi thelathini wakashuka chini kwenye mwamba wa Daudi, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti walieka kambi katika bonde la Refaim.
16 同時達味恰在山砦內,培肋舍特人當時也在白冷駐防,
Kwa wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, Wafilisti walikita kambi yao Bethilehemu.
17 達味渴望說:「誰能從白冷城門旁的井中,給我打一點水來喝呢﹖」
Daudi alikuwa na kiu ya maji na akasema, “Laiti mtu akanipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho Bethilehemu, kisima kilicho pembeni mwa lango!”
18 那三位勇士就衝過培肋舍特人的營幕,從白冷城門旁的井中打了水,將水取來帶到達味前;但達味不肯喝,反而將水奠於上主前,
Hawa wanaume hodari watatu wakatoboa kupita jeshi la Wafilisti na kuchota maji kwenye kisima cha Bethilehemu, kisima pembeni mwa lango. Wakachukuwa maji na kumletea Daudi, lakini alikataa kunywa. Badala yake, akamwaga chini kwa Yahweh.
19 說「我的天主決不許我做這事! 我豈能喝這些冒生命危險者的血﹖因為這是他們冒生命危險取來的。」所以他不肯喝。這是這三個勇士所做的。
Kisha akasema, “Yahweh, iwe mbali na mimi, kwamba ni yanywe haya maji. Je ninywe damu ya wanaume walio hatarisha maisha yao?” Kwa sababu wameeka maisha ya hatarini, akakataa kunywa. Haya ni mambo wanaume hodari watatu walio fanya.
20 約阿布的兄弟阿彼瑟,是三十勇士的領袖,他揮舞長矛殺了三百人,因此在三十勇士中出了名;
Abishai kaka wa Yoabu, alikuwa kiongozi wa watatu. Alitumia mkuki wake dhidi ya watu mia tatu na kuwaua. Ametajwa pamoja na wale watatu.
21 他在三十勇士中享有雙重的名望,做了他們的領袖,做了他們的領袖,但尚不及三傑。
Kati ya wale watatu, yeye alipewa heshima mara mbili na akawa kiongozi wao. Japo hakuwa mmoja wa miongoni mwao.
22 約雅達的兒子貝納雅原是卡貝責耳人,是一位英勇大有作為的人,曾擊殺摩阿布人阿黎耳的兩個兒子;又在下雪天,下到旱井裡打死了一隻獅子。
Benaia mwana wa Yehoiada alikuwa mwanaume mwenye nguvu aliye fanya mambo makuu. Aliua wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka chini ya shimo na kumuua simba wakati theluji ikianguka.
23 他也曾打死了一個埃及巨人。這埃及人人身高五肘,手中拿著粗如織布機軸的長矛,貝納雅下去,手中僅拿著一根棍杖,從那埃及人手中,把長矛奪了過來,用那長矛將他殺死。
Alimua hadi Mmisri, mwanaume mwenye mita mbili na theluthi moja. Mmisri alikuwa na mkuki kama gongo la mshonaji, lakini alimfuata chini na fimbo tu. Akakamata mkuki katika mkono wa Mmisri na kumuua na mkuki wake.
24 這是約雅達的兒子貝納雅所做的事。因此在三十勇士中出了名。
Benaia mwana wa Yehoiada alifanya haya matukio, na akatajwa miongoni mwa wale wanaume hodari watatu.
25 他比三十勇士更有名望,但尚不及三傑。達味派他作侍衛長。
Alisifika zaidi ya wale wanajeshi thelathini kwa ujumla, lakini hakuwa pewa hadhi ya wale wanajeshi watatu hodari. Daudi alimueka kiongozi wa walinzi wake.
26 其餘的勇士:有約阿布的兄弟阿撒耳,白冷人多多的兒子厄耳哈難,
Wanaume hodari walikuwa Asaheli kaka wa Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethilehemu,
27 哈洛得人沙摩特,帕耳提人赫肋茲,
Shamothi Mherori, Helezi Mpeloni,
28 特科亞人依刻士的兒子依辣,阿納托特人阿彼厄則爾,
Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi, Abi Eza Manathothi,
29 胡沙人息貝開,阿曷亞人衣來,
Sibekai Mhushathite, Ilai Mahohite,
30 乃托法人瑪哈賴,乃托法人巴阿納的兒子赫肋得,
Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana Mnetofathite,
31 本雅明族基貝亞人黎拜的兒子依泰、丕辣通人貝納雅,
Itai mwana wa Ribai wa Gibea uzao wa Benjamini, Benaia Mpirathoni,
32 加阿士士溪人胡賴,貝特阿辣巴人阿彼巴耳,
Hurai wa mabonde ya Gaashi, Abieli Marbathi,
33 巴胡陵人阿次瑪委特,沙阿耳賓人厄里雅巴,
Azmavethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni,
34 基宗人雅笙,哈辣黎人沙革的兒子約納堂,
Mwana wa Hashemu Mgizoni, Yonathani mwana wa Shagee Mhararite,
35 哈辣黎人撒加爾的兒子阿希楊,烏爾的兒子厄里法耳,
Ahiamu mwana wa Sacari Mhararite, Elifali mwana wa Uri,
36 默革辣人赫費爾,基羅人阿希雅,
Hefa Mmekarathi, Ahija Mpeloni,
37 加爾默耳人赫茲賴,厄次拜的兒子納阿賴,
Hezro Mcarmeli, Maarai mwana wa Ezibai,
38 納堂的兄弟約厄耳,哈革黎的兒子米貝哈爾,
Yoeli kaka wa Nathani, Mibhari mwana wa Hagiri,
39 阿孟人責肋克,貝厄洛特人納赫賴,他是責魯雅的兒子約阿布的執戟者,
Zeleki Mamoni, Naharai Mberothi ( mbeba ngao ya Yoabu mwana wa Zeruia),
40 雅提爾人依辣,雅提爾人加勒布,
Ira Mithire, Garebu Mithire,
41 赫特人烏黎雅,阿赫來的兒子匝巴得,
Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Ahlai,
42 勒烏本人史匝的兒子阿狄納,他是勒烏本人的首領,有三十個人跟隨他,
Adina mwana wa Shiza Mreubeni ( kiongozi wa Wareubeni) na thelathini pamoja nae,
43 瑪加的兒子哈南,默騰人約沙法特,
Hanani mwana wa Maaka, na Yoshafati Mmithini,
44 阿市塔洛特人烏齊雅,阿洛厄爾人曷堂的兒子沙瑪和耶厄耳,
Uzia Mashiterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Waaroeri,
45 提漆人史默黎的兒子耶狄阿耳和他的兄弟約哈,
Jediaeli mwana wa Shimri, Joha ( kaka yake Mtize),
46 瑪紅人厄里耳,厄耳納罕的兒子耶黎拜和約沙委雅,摩阿布人依特瑪,
Elieli Mmahavi, Yeribai na Yoshavia mwana wa Elnaamu, Ithima Mmoabi,
47 厄里耳,敖貝得和祚巴人雅息耳。
Elieli, Obedi, na Yaasieli Wamezobai.

< 歷代志上 11 >