< Milu Pareinae 27 >
1 Joseph capa Manasseh imthung, Makhir, ahnie capa Gilead, ahnie capa Hepher, ahnie capa Zelophehad e canu naw doeh. A canunaw e minnaw teh, Mahlah, Noah, Hoglah, Milkah hoi Tirzah tinaw doeh.
Kisah wakaja kwa Musa binti wa Zelofehadi mwana wa Hefa mwana wa Gilied mwana wa Machiri mwana wa Manase, wa ukoo wa Manase mwana wa Yusufu. Hawa ndio waliokuwa binti zake: Mahala, Noha, Hogla, Milika, na Tiriza.
2 Kamkhuengnae lukkareiim takhang koe Mosi hoi vaihma Eleazar hoi tamikalennaw kamkhuengnaw e hmalah a kangdue awh teh,
Walisimama mbele ya Musa, Eliazari kuhani, kwa. viongozi, na mbele ya watu wote langoni mwa hema ya kukutania. Walisema,
3 Kahrawngum vah maimae na pa a due teh, BAWIPA taranlahoi cusin hane tamihu, Korah tamihu koe bawk van hoeh. Hatei, ama yon e lahoi a due teh a capa hai tawn hoeh
“Baba yetu alifia jangwani. Hakuwa mmoja wa wale waliompinga BWANA katika lile kundi la Kora. Alikufa kwa dhambi zake, na hakuwa na watoto wa kiume.
4 Capa a tawn hoeh kecu dawkvah, bangkongmaw apa min teh miphun thung hoi a kahma han, mintoenaw thung dawkvah, ka ham kawi na poe van leih ati awh.
Kwa nini jina la baba yetu liondolewe mioingoni mwa ukoo wa jamaa zake kwa sababu ya kukosa wana? Tupeni ardhi miongoni mwa ndugu wa baba zetu.”
5 Hot patetlah Mosi ni hote lawk teh BAWIPA koe a pha sak.
Kwa hiyo Musa alileta shauri hilo mbele za BWANA.
6 BAWIPA ni Mosi hah a pato teh,
BWANA akanena na Musa akamwambia, “Binti wa
7 Zelophehad canunaw ni kathuem e a sak awh. A na pa hmaunawnghanaw rahak vah, a ham kawi na poe awh roeroe vaiteh, a na pa ham hah na poe awh han.
Zelofehadi wanasema kitu sahihi. Lazima uwaptie ardhi kama urithi miongoni mwa ndugu wa baba zao, na uhakikishe kuwa urithi wa baba zao wanapata.
8 Isarel catounnaw koevah, tami buet touh ca tongpa tawn laipalah dout pawiteh, a râw teh a canunaw na poe han.
Utawaambia wana wa Israeli na kusema, 'Kama mtu anakufa na hana mtoto wa kiume, basi utaufanya urithi wake wapewe binti zake.
9 Hahoi a canu tawn hoehpawiteh, a râw teh a hmaunawngha na poe han.
Kama hana binti, basi urithi wake atapewa kaka zake.
10 Hmaunawngha tawn hoehpawiteh, a na pa e hmaunawngha na poe pouh han.
Kama hana kaka zake basi huo urithi watapewa ndugu wa baba yake.
11 A na pa ni hmaunawngha tawn hoehpawiteh, a râw teh a huikonaw na poe vaiteh, ahnimouh ni a ham awh han. BAWIPA ni Mosi kâ a poe e patetlah Isarel canaw hanlah lawkcengnae phunglam lah ao han, telah dei pouh telah ati.
Kama baba yake hana ndugu, basi huo urithi atapewa ndugu yake wa karibu katika ukoo, na utauchukua kuwa wake. Hii itakuwa sheria iliyoanzishwa kwa amri kwa ajili ya watu wa Israeli kama BWANA akivyoniamuru.”
12 BAWIPA ni Mosi koevah, Abarim mon dawkvah luen nateh, Isarel catounnaw ka poe hane ram hah radoung haw.
BWANA alimwamia Musa, “Nenda juu ya mlima Abaraimu na uitazama nchi ambyo nimewapa wana wa Israeli.
13 Hahoi na hmu toteh, na hmaunawngha Aron e a miphunnaw koevah, a ceikhai awh e patetlah nang hai na ceikhai awh han.
Baada ya kuwa umeiona, pia lazima ufe, kama Haruni kaka yako.
14 Bangkongtetpawiteh, Zin thingyei dawk taminaw pueng ni a phuenang awh navah, a mithmu vah tui dawk kai barilawa na poe nahanelah, kai ni kâ na poe e taranlahoi taran a thaw awh telah ati (hot teh Zin thingyei dawk Kadesh hoi Meribah tie lah a o).
Hii itatokea kwa sababu ulipinga amri yangu katika jangwa la Sini. Pale ambapo maji yalitoka kwenye mwamba, katika hasira yako ulishindwa kuniheshimu mimi kama mtakatifu mbele ya macho ya watu wote.” Haya ni yale maji ya Meriba ya Kadeshi katika jangwa la Sini.
15 Hahoi Mosi ni BAWIPA a pato teh,
Ndipo Musa akamwambia BWANA akisema,
16 moithangnaw pueng e hringnae kaukkung Cathut BAWIPA e taminaw hah kakhoumkung tawn laipalah tu patetlah ao hoeh nahanlah tamihu,
“Wewe, BWANA, Mungu wa wote wenye mwili, uchague mtu awe juu ya watu,
17 hmalah cei hoi ahnimouh tâcokhai hane hoi kâenkhai hane kahrawikung hah rawi seh, telah ati.
mtu ambaye atatoka na kuingia kuja kwao na kuwatoa kisha kuwarudisha, ili kwamba watu wako wasije kuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji.”
18 BAWIPA ni Mosi koevah, Nun capa hnotithainae ka tawn e Joshua hrawi nateh, ahni van na kut toung pouh.
BWANA akanena na Musa, “Mchukue Joshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yangu hukaa, na umwekee mikono yako juu yake.
19 Vaihma Eleazar hoi ka kamkhuengnaw hmalah kangdout sak nateh, ahnimae mithmu vah caksak.
Umweke mbele ya Eliazari kuhani na mbele ya watu wote, na umwamuru kuwaongoza mbele ya macho yao.
20 Isarel catounnaw pueng ni a lawk a ngâi pouh thai nahan, na kâtawnnae a tangawn hah na poe han.
Utaweka baadhi ya mamlaka yako kwake, ili kwamba watu wote wa Isareli wamtii.
21 Ahni teh vaihma Eleazar hmalah a kangdue vaiteh, ama ni BAWIPA hmalah, Urim hno lahoi lawkkamnae a la vaiteh, ama kâ lahoi Isarel catounnaw pueng teh a tâco a kâen awh han, telah ati.
Ataenda mbele ya Eliazari kuhani ili kutafuta mapenzi yangu kwake kwa ajili ya maamuzi ya kura. Yeye ndiyo atakayetoa amri ili watu kutoka na kuingia, yeye pamoja na watu wa Israeli, ambao ni watu wote.”
22 Mosi ni BAWIPA kâpoe e patetlah a sak, Joshua hah a hrawi teh, Eleazar hoi kamkhuengnaw hmalah a kangdue sak.
Kwa hiyo Musa akafanya kama alivyoagizwa na BWANA. Alimchukua Joshua na kumweka mbele ya Eliazari kuhani na mbele ya jamii yote.
23 A lathueng vah kut a toung pouh teh, Mosi hno lahoi BAWIPA ni kâ a poe e patetlah kâtawnnae hah a poe.
Akaweka mikono yake juuy ake na kumwamuru aongoze, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.