< Mark 3 >
1 Bachi a ri no mitra u pre da same ni Indi wu lullo wu so wo.
Na tena aliingia ndani ya sinagogi na mle palikuwa na mtu mwenye mkono uliopooza.
2 Indi ba sure shishi niwu ko ani wurka ni wu cacu asabar don da ka to ni la ter.
Baadhi ya watu walikuwa wakimfuatilia kwa ukaribu kuona kama atamponya siku ya Sabato ili kwamba wamshitaki.
3 Yesu hla nindi wu lullo wo, rhu kli ni tsutsu Indi ba, Yesu a miye ndi ba.
Yesu alimwambia mtu mwenye mkono uliopooza, “Inuka na usimame katikati ya umati huu.”
4 Abi duba tie zizi nive asabar d kpa ndi cuwo ka ndu tie meme indu Indi ba que? Indi ba ba son ng bage.
Kisha akawaambia watu, “Je ni halali kutenda tendo jema siku ya Sabato au kutenda yasiyo haki; kuokoa maisha, au kuua?” Lakini walibaki kimya.
5 Yesu a kma ya ndi ba nifu done touri dir mba da hla ni gu n ma wo me? igu n ma wo ma u won bi.
Akawaangalia kwa hasira, akihuzunika kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, na akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako”. Akaunyoosha na Yesu akamponya mkono wake.
6 Farisawa banu gla me da hadatu niti rudiyawo di ba wo Yesu.
Mafarisayo wakaenda nje na mara wakafanya njama pamoja na Maherode dhidi yake ili kumuua.
7 Yesu ni mini koma ba hi nen wu Indi gbugbu ba hu bari ba ni ni Galilee ba ri bani Judia
Kisha Yesu, pamoja na wanafunzi wake, walienda baharini, na umati mkubwa wa watu uliwafuata ukitokea Galilaya na Uyahudi
8 Urshalima, indumi ya bari me gaba ni Jordan, Tyre har ni Sidon. Daba wo gbi a si ti Indi gbugbu u bayi niwu.
na kutoka Yerusalemu na kutoka Idumaya na mbele ya Yorodani na jirani ya Tiro na Sidoni, umati mkubwa, uliposikia kila kitu alichokuwa anakifanya, walikuja kwake.
9 A hla ni miniko ma duba samu ni igu tsitsima ni wawu don into du ba na matse bi was wu na.
Na aliwaambia wanafunzi wake kuandaa mtubwi mdongo kwa ajili yake kwa sababu ya umati, ili kwamba wasije wakamsonga.
10 A warka indi gbugbu u bi lullo ba turn kpamba ni baba sawo niwu da fe se. Bachi a kpa bari just ni lullon.
Kwa kuwa aliponya wengi, ili kila mtu aliyekuwa na mateso alikuwa na shauku ya kumfikia ili amguse.
11 Ko nitan bi ruhu brji bajoku ni koshishi da Yar go da ter wu vir irji.
Popote roho wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kulia, na walisema, “Wewe ni Mwana wa Mungu”.
12 A kpa nha ni ba duba dubu nde ma na
Aliwaamuru kwa msisitizo wasifanye ajulikane.
13 A ho he ni gbulu da yo biwa a ni son u ba ye same ni wu.
Alienda juu ya mlima, na akawaita aliowataka, na wakaenda kwake.
14 A ju ndi woto dan ha wa yo ba di (apostles) do duba he ni wa,
Akawachagua kumi na wawili (aliowaita mitume), ili kwamba wawe pamoja naye na aweze kuwatuma kuhubiri,
15 wa turba du ba hla ter wada he ni glegle wu zu bryi.
na kuwa na mamlaka ya kutoa mapepo.
16 Mazani wolo dan ha wanda ju ba na he nayi Simon wanda a non dema Bitrus.
Na akawachagua kumi na wawili: Simoni, aliyempa jina la Petro,
17 Yakub very Zabadi, Yohana vayi Yakub Wanda a nu de Banergas wato minizan
Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake Yakobo, aliyepewa jina la Bonagesi, hao ni, wana wa ngurumo,
18 wu Adarawas u Fibus, Bar ta Lamawas, Matiwu, Tomas, Yakub very Haifa u Yahuza, Thaddaeus, Simon Bakan ane
na Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo,
19 wu Yahuza Iskanyoti Wanda ya bashe shi.
na Yuda Iskariote, ambaye atamsaliti.
20 A kma he ko, wu kpetren indi bakaba da iya ri bin na.
Kisha alienda nyumbani, na umati wa watu wakaja pamoja tena, hata wasiweze kula hata mkate.
21 Da bikoma ba won naki da he niwu da ter, imiri ma na he na he ni wu na.
Familia yake waliposikia habari hiyo, walienda kumkamata, kwani walisema, “Amerukwa na akili”.
22 Bi nha wa ba ni Urishalima ba ter di, a he ni ruhu Beelzebul, “mba meme brji”.
Waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli,” na, “Kwa mtawala wa mapepo anatoa mapepo”.
23 Yesu yo ba da ter ba yi-yi, ibrji ani ti ni he da zu ibrji?
Yesu aliwaita kwake na kusema nao kwa mifano, “Jinsi gani Shetani aweza kumtoa Shetani?
24 Idam mulki gu kpama te kam-kan mulki ba na to kle gbangba na.
Kama ufalme ukigawanyika wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama.
25 Idam iko ga kpema komba ana kle gbangba na idan b
Kama nyumba ikigawanyika yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
26 a tayar ni nituma da ga gba ana he niglegle-glegle na anijoku.
Kama Shetani atainuka kinyume chake mwenyewe na kugawanyika, hawezi kusimama, na atakuwa amefika mwisho wake.
27 Idi na ya da ri ko idi u gle-gle da yi bi kpe ma na ha ma ni vu indi glegle u ko.
Lakini hakuna hata mmoja awezaye kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuiba vitu vyake bila kumfunga mwenye nguvu kwanza, na kisha kukusanya kilichomo nyumbani.
28 Jaji mu me hla you la tre we me wa wa Indi ba ti iha wur la bawu.
Kweli nawambieni, dhambi zote za wana wa watu zitasamehewa, pamoja na kufuru ambazo wanatamka,
29 A ma wa ba ti ni Ruhu tsatsra ba na wur le meml mu, dona la tre u ka kle. (aiōn , aiōnios )
lakini yeyote atakaye mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, bali ana hatia ya dhambi ya milele”. (aiōn , aiōnios )
30 Yesu tree ni tu wa ha tre, ahei brji
Yesu alilisema hili kwa sababu walikuwa wakisema, “Ana roho chafu”.
31 I yima ni mir vayi ba ye kril ko ra. Ba to ba ka yo'u ye gba nmba.
Kisha mama yake na ndugu zake walikuja na kusimama nje. Wakamtuma mtu, kumwita.
32 Kpetren ndi ba ki kagon ma da me yer, I yi me ni mir vayi me ba hei ko ra da ki wa u
Na umati wa watu uliokuwa umekaa karibu naye wakamwambia, “mama yako na ndugu zako wako nje, na wanakutafuta wewe”.
33 A sa ni ba'u, ba nha ba mir vayi mu?
Aliwajibu, “Ni nani mama yangu na ndugu zangu?”
34 A ka ya ndi wa ba ki gon kla ma da tre, “To ibiyi yi bi mir vayi mu!
Aliwaangalia waliokuwa wamekaa wamemzunguka, na akasema, “Tazama, hawa ni mama zangu na ndugu zangu!
35 Duk ndi wa ni ti kpe wa rji tre a wa u yi hi yimu da hi mir vayi mu.
Yeyote afanyaye mapenzi ya Mungu, mtu huyo ni ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu”.