< Yohana 13 >
1 Igan idin tsatsra rigyen u ye, u Yesu to andi inton tsra wa a lu ni gbungblu hi ni Ti'a. Niwa ani son bi ma wa ba he ni gbungblu, a son ba ye ni kekle.
Sasa kabla ya sikukuu ya pasaka, kwa sababu Yesu alifahamu kuwa saa yake imefika ambayo atatoka katika dunia hii kwenda kwa baba, akiwa amewapenda watu wake ambao walikuwa duniani, aliwapenda upeo.
2 Ibrji yo ni sron Yahuda Iskariyoti ivren Saminu, aka Yesu le.
Na ibilisi alikuwa amewekwa tayari katika moyo wa Yuda Isikariote, mwana wa simoni, kumsaliti Yesu.
3 Ato ndi Iti a ka kongeri no ni woma, na rji ni Rji, ani la kma hi ni Rji.
Yesu alifahamu kuwa baba ameweka vitu vyote katika mikono yake na kwamba ametoka kwa Mungu na alikuwa anakwenda tena kwa Mungu.
4 A lunde ni bubu ri biri, na ju kpima, na ban inklon u se ma kpa na ka kpa ma niwu.
Aliamka chakulani na akatandika chini vazi lake la nje. Kisha alichukua taulo na akajifunga mwenyewe.
5 Wa sur ima ni konko na si ngla za ni almajere ma ba na se za ba wu ni inklon u se kpa wa a ka kpama niwu'a.
Kisha akatia maji katika bakuli na akaanza kuwaosha miguu wanafunzi wake na kuwafuta na taulo ambayo alijifunga yeye mwenyewe.
6 Na ye ni Siman Bitrus, u Bitrus tre niwu, “Bachi, u ngla za mu me?”
Akaja kwa Simoni Petro, na Petro akamwambia, “Bwana, Unataka kuniosha miguu yangu?”
7 Yesu sa niwu na tre, “Ikpe wa mi si ti'a una to na zizan? U to ni ton u ye (ajima).
Yesu akajibu na kumwambia, “Nifanyalo hulijui sasa, lakini utaelewa baadaye.”
8 Bitrus hla niwu, una ti bre ngla za mu.” Yesu hla niwu, “Mita ngla niwu na, una he ni san me ni me na.” (aiōn )
Petro akamwambia, “Hutaniosha miguu yangu kamwe.” Yesu akamjibu, “Ikiwa sitakuosha, hutakuwa na sehemu pamoja nami.” (aiōn )
9 Siman Bitrus hla niwu, “Bachi, na ngla zamu migyen na, ngla womu ni tu mu.”
Simoni Petro akamwambia, “Bwana, usinioshe miguu yangu tuu, bali pia na mikono na kichwa changu.”
10 Yesu hla niwu, “Indji wa a sukpa'a ana wa sukpa na, se ka ngla za, wa ahi tsatsra ndji wawu bi tsatsra, ama ani wawu mbi na.
Yesu akamwambia, “Yeyote ambaye amekwisha kuoga haitaji kuoga isipokuwa miguu yake, na amekuwa safi mwili wake wote; ninyi mmekuwa safi, lakini si nyote.”
11 (Yesu a to indji wa ani kawu le, kima sa wa tre naki, ana wawu mbi bi tsatsra na).
Kwa kuwa Yesu alijua yule atakaye msaliti; hii ndiyo sababu alisema, si nyote mmekuwa safi.”
12 Ni kokon wa Yesu ngla za bawu, a ban konlon ma na kuson ngari, na hlabawu, “Bito kpe wa mi ti ni yiwu'a?
Wakati Yesu alipokuwa amewaosha miguu yao na akiisha chukua vazi lake na kukaa tena, aliwaambia, “Je Mnaelewa kile ambacho nimewafanyia?
13 Bi yo me ni 'Mala' ni 'Bachi,' u bi yo me tsra, a naki mi he.
Mnaniita mimi “Mwalimu” na Bwana hii mnasema kweli, maana ndivyo nilivyo.
14 U to Me wa mi Bachi ni Mala, u mi ngla za mbi, biyi ngame bika ngla za ni kpambi.
Ikiwa mimi Bwana na mwalimu, nimewaosha miguu yenu, ninyi pia imewapasa kuwaosha wenzenu miguu.
15 U mi tsro yi misali, ni ndu ti na wa mi tie ni yiwu.
Kwa kuwa nimewapa mfano ili kwamba ninyi pia mfanye kama mimi nilivyo fanya kwenu.
16 Gbigbi njanji mi si hla ni yiwu, igran na zan tiko ma ni ninkon na, ivren u ton ndu ana zan indji wa ton'u ndu ninkon na.
Amini, Amini, nawambia, mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala yule ambaye ametumwa ni mkuu kuliko yule aliye mtuma.
17 Bita to kpi biyi, bi-bi lulu ni nde bi ti ba.
Ikiwa unafahamu mambo haya, umebarikiwa ukiyatenda.
18 Mi na si tre yi wawu na; Mi to biwa mi chu ba'a - nitu ndi nassi tsra indji wa a tan bredi a tayar nimu.
Sisemi kuhusu ninyi nyote, kwa kuwa nawajua wale ambao nimewachagua - bali nasema haya ili kwamba maandiko yaweze kutimilizwa: 'Yeye alaye mkate wangu ameniinulia kisigino chake.'
19 Mi si hla wa yi ni yiwu zizan ri ni ndu ka ti naki ni ndu yi ka kpa-nyeme ni me ni nton wa ani ti naki'a.
Ninawambia hili sasa kabla halijatokea ili kwamba litakapotokea, muweze kuamini kuwa mimi NDIYE.
20 Njanji, njanji, mi si hla ni yiwu, indji wa a kpa ndi wa mi ton'wu, ahi Me a kpa, indji wa a kpa Me, a kpa Indji wa a ton Me.
“Amini, amini, nawambia, anipokeaye mimi humpokea ambaye nina mtuma, na yule anipokeaye mimi humpokea yule aliye nituma mimi.”
21 Ni kogon wa Yesu tre naki, na lo sron ni (Ruhu), na ti gban (shada) andi, gbigbi njanji, mi si hla ni yieu ndi iri ni mibi ani le ni me.”
Wakati Yesu aliposema haya, alisumbuka rohoni, alishuhudia na kusema, “Amini, amini, nawambia kwamba mmoja wenu atanisaliti.”
22 Almajire ba ba kma ya kpa mba, na ni tamre, ka ahi nha ni mi mba a si tre ni tu ma.
Wanafunzi wake wakatazamana, wakishangaa ni kwa ajili ya nani alizungumza.
23 Iri nimi almajire ma, wa Yesu ni son, ahe ni tebru, na kunyre ni san Yesu.
Kulikuwa katika meza, mmoja wa wanafunzi wake ameegama kifuani mwa Yesu yule ambaye Yesu alimpenda.
24 Siman Bitrus hla ni almajire bika minye, “Ndu hla tawu a hi nha a si tre ni tu ma.”
Simoni Petro alimuuliza mwanafunzi huyu na kusema, “Twambie ni yupi ambaye kwake anazungumza.”
25 Wa hla bru kunyre ni san Yesu, na tre niwu, Bachi, ahi nha?
Mwanafunzi yule aliye egama kifuani mwa Yesu na akamwambia, “Bwana, ni nani?”
26 U Yesu hla niwu, a wawu yi wa mi ka cichon bredi sun ni kano. Naki ri na ka bredi sun, na ka no Yahuda ivren Siman Iskariyoti.
Kisha Yesu alijibu, “Ni kwake yule nitakaye chovya kipande cha mkate na kumpatia.” Hivyo alipo kuwa amechovya mkate, alimpatia Yuda mwana wa Simon Iskariote.
27 Ni kogon bredi'a u ibrji a ri ni wu, u Yesu hla niwu, “Ikpe wa u son ti'a, uka ti gbagbla.”
Na baada ya mkate, Shetani alimuingia. Kisha Yesu akamwambia, “Kile ambacho unataka kukifanya ukifanye haraka.”
28 Indrjori na la he ni tebru na, wa ani to ikpe wa yo'a hla niwu naki'a.
Sasa hakuna mtu katika meza alijua sababu ya Yesu kusema jambo hili kwake.
29 Bari mba ba ya ndi, a Yahuda yi ni nji imbu nklen Yesu hla niwa, “Le ikpe wa ki son ti ndu niwu ni idin,” ko ka no ikpe ni bi wa ba kunyre'a.
Baadhi yao walidhani kwamba, kwa sababu Yuda alishika mfuko wa fedha, Yesu alimwambia, “Nunua vitu tunavyohitaji kwa ajili ya sikukuu,” au kwamba anapaswa kutoa kitu kwa masikini.
30 Ni kogon wa Yahuda a kpa bredi'a, wa rju gbagbla gbagbla me ni chu me.
Baada ya Yuda kupokea mkate, alitoka nje harak; na ilikuwa usiku.
31 Ni kogon wa Yahuda hi'a, Yesu tre, zizan ba no Vren Indji ni kon, ngari ba no Irji ninkon ni mi ma.
Wakati Yuda alipokuwa ameondoka, Yesu alisema, “Sasa mwana wa Adam ametukuzwa, na Mungu ametukuzwa katika yeye.
32 Irji ni no ninkon ni mi ma, ani no ninkon zizan zizan.
Mungu atamtukuza katika yeye mwenyewe, na atamtukuza haraka.
33 Imri bi tsitsa mi he ni yi ni vi ton tsa me, biwa me na wa mi hla Yahudawa, bubu wa me mi hi bi na ya hi na. Zizan mi hla wa yi ni yiwu.
Watoto wadogo, niko pamoja nanyi kitambo kidogo. Mtanitafuta, na kama nilivyowambia Wayahudi, 'Niendako, hamuwezi kuja.' sasa nawambia ninyi, pia.
34 Mi si no yi indu ri sama, son kpa mbi, na wa mi son yi, na bi ka son kpambi.
Ninawapa amri mpya, kwamba mpendane; kama mimi nilivyo wapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi pia imewapasa kupendana ninyi kwa ninyi.
35 Na ko nha ni to yi ndi bi almajire mu, inde bi son kpambi.”
Kwa ajili ya hili watu watatambua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu, ikiwa mna upendo kwa kila mmoja na mwingine.”
36 Siman Bitrus tre niwu, Bachi, u hi ni ntsen?” Yesu hla ni wu, bubu wa mi si hi'a, una ya hina me zizan hi na, u wuka ye hu me ni kogon.”
Simoni Petro alimwambia, “Bwana, unakwenda wapi?” Yesu akajibu, “Mahali ninapokwenda kwa sasa hutaweza kunifuata, lakini utanifuata baadaye.”
37 Bitrus hla niwu, “Bachi, a ngyeri mba sa mi na hu zizan na? Mi no re (ivri) mu ni tu me.”
Petro akamwambia, “Bwana, kwa nini nisikufuate hata sasa? Mimi nitayatoa maisha yangu kwa ajili yako.”
38 Yesu hla niwu, u ka re (ivri) me no ni tu mu? Gbigbi njanji, mi si hla niwu, u kame ni me ni kpatron ingyu tra ri ndu mble ndu kpan
Yesu akajibu, “Je utayatoa maisha yako kwa ajili yangu? Amini amini nakwambia, jogoo hatawika kabla hujanikana mara tatu.”