< James 2 >
1 be yi mrivayi be ta ji kponji u tibu yesu Almasihu irji u gbirasan be kan tsoro kanka ni bru idi na
Ndugu zangu msiifuate imani ya Bwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, kwa kupendelea watu fulani.
2 u idiri nita ye ni yi ni mi shubi u bi nda suru zobban zinariya ni ikulon dedema udiri a ye nda suru gbajan kolon
Kama mtu fulani akiingia kwenye mikutano yenu amevaa pete za dhahabu na mavazi mazuri, pia akaingia masikini mwenye mavazi machafu,
3 u be ta kpa idi ukulon dedema nde no bubu u
na mkaonyesha kumjali zaidi yule mwenye mavazi mazuri na kusema, “Tafadhari wewe keti hapa mahali pazuri” lakini mkamwambia yule masikini, “Wewe simama pale,” au “Kaa chini ya miguu yangu.”
4 kuson dedema u idi uya anita ye u be hla du kukri ghugbamu n yi ko juma be kahla wu du kuson ni meme ni koshishi u be na toh ade be si yo latre ni kpabina u be hi be turon ni meme sonron na?
Je, hamuhukumiani ninyi wenyewe, na kuwa waamuzi wenye mawazo mabaya?
5 wori imrivayi mubeyi be na toh ade irji a chu be ya ni mi gbuugblu du mba he be wo ni mi njaaji nda he be wa mba kpa nkon wa yonyu ni be wa mba son wu
Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa, je, Mungu hakuwachagua masikini wa dunia kuwa matajiri katika imani na kurithi ufalme aliowaahidia wampendao?
6 u be kpa be ya tsiri be na toh a nde be wo yi mba o yi ya na?
Lakini mmewadharau masikini! Je, sio matajiri wanaowatesa ninyi, na sio wao wanaowaburuta mahakamani?
7 mba mbayi mba mri yi ni idedede ma be yoa
Je, si matajiri wanaolitukana jina lile zuri ambalo kwalo mnaitiwa?
8 ko ni he u tta cika ituron be chu na wa vuvu a tre a u ka sonvayime na wa u sontume u ti dede ma
Hata hivyo, kama mwaitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa katika maandiko, “Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe,” mwafanya vyema.
9 amma u be ta tsoro kankan ni mi bi be kpaturon tsiri
Lakini kama mkipendelea baadhi ya watu, mnatenda dhambi, mwahukumiwa na sheria kuwa ni wavunja sheria.
10 u wa a hu turon wawu da kwubza ni riri a sontuma ni turon a wawu
Kwa kuwa yeyote atiiye sheria yote, na bado akajikwaa katika nukta moja tu, amekuwa na hatia ya kuvunja sheria yote!
11 udiri ni ta tre na ti ta na nde la tre na wu na u ta na ti fa na u ta wu u he idi u kpa turon tsiri
Kwa kuwa Mungu aliyesema, “Usizini,” ndiye pia aliyesema, “Usiue.” Kama hauzini, lakini una uwa, umekwishavunja sheria ya Mungu.
12 nakima be ka tre de ti na be wa mba bla ni mi turon u son tu
Kwa hiyo zungumzeni na kutii kama wale ambao mko karibu kuhukumiwa na sheria ya uhuru.
13 u hukunci a ni ye ba lonsoron mba ni idi wa ana consonrona. consonron ni ijur ni mi hukunci
Kwa kuwa hukumu huja pasipo huruma kwa wale wasio na huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.
14 dedema a hi ge imrivayimu idan idiri ni ta tre de wa wu he ni njaaji da na ti idu ba na? u njaaji kima ana kpchuwona ko ani ya?
Kuna uzuri gani, ndugu zangu, kama mtu anasema ninayo imani, lakini hana matendo? Je, imani hiyo yaweza kumwokoa?
15 misali idan vayime lilo ko vayi me vrewa ana suru ikolo meme ma da wa ila hama u cha chuki
Kama ndugu wa kiume au wa kike ni muhitaji wa mavazi au chakula cha kila siku,
16 misali du irirbi du hla ni mba hi ni si sonron son ni hruhu ni hwt u tana no mba kpi wa ikpamba ni sona na u demema a hige?
na mmoja wenu akawaambia, “Nendeni kwa amani, mkaote moto na mle vizuri,” lakini hamuwapi mahitaji muhimu ya mwili, hiyo yafaaa nini?
17 ni kon kima njaaji ni tuma idan ana tiduna a hi kuboma
Hali kadhalika, imani pekee, kama haina matendo, imekufa.
18 e idri ani tre u he ni kpouji ti du na tsoro me kpohji me wa ana he ni iduana u me mi tsoro ikpohji mu ni idum
Bado mtu fulani anaweza kusema, “Una imani, na mimi ninayo matendo.” Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu.
19 u ka kpakyeme ande irji a hi riri u ti bi u ko ibrji me mba kpakyemi ni mi sisiri
Waamini kuwa kuna Mungu mmoja; uko sahihi. Lakini mapepo nayo yanaamini hivyo na kutetemeka.
20 u son toh u na he idi u mre na de njaaji wa ana he ni iduna a hi mege
Je, unataka kujua, ewe mtu mpumbavu, namna ambavyo imani hiyo pasipo matendo isivyofaa?
21 ana hi itibu Ibrahim wa mba giri ni duma wa a ban ivrema Ishaku no ni bagadi irji na?
Je, si baba yetu Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo alipomtoa mwanawe Isaka juu ya madhabahu?
22 u ka tohde njaji a ni tidu ni duma mba nidu u njaaji ani kpau gboru
Mnaona kuwa imani yake ilifanya kazi na matendo yake, na kwa matendo yake, imani yake ilifikia kusudio lake.
23 u vuvu a kle tre de Ibrahim a kpakyeme ni irji u a bla yo ni be tsatsara u mba ka yo de ikpa irji
Maandiko yalitimizwa yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu, na akahesabiwa kuwa ni mwenye haki.” Hivyo Abrahamu aliitwa rafiki wa Mungu.
24 be toh ade a he ni tu idu mba gbiradisa ana ni kpakyeme na
Mwaona kuwa kwa matendo mtu huhesabiwa haki, na si kwa imani tu.
25 ni ko kma me Rahab ghughu wa mba gbirasa ni tu du wa a kpa be tsiri da tsoro mba ikorikha na?
Hali kadhalika, je, hakuwa Rahabu yule kahaba alihesabiwa haki kwa matendo, alipowakaribisha wajumbe na kuwapeleka kwa barabara nyingine?
26 na ikpa wa ana he ni ibrji na a hi ikobuma kpoji wa ana he ni du na a hi kobon ma.
Kwa kuwa kama vile mwili usipokuwa na roho umekufa, vivyo hivyo imani pasipo matendo imekufa.