< 1 Yohana 2 >

1 Mri, mi si han kpi biyi ni yu'u du yina lahtre na. Uri ni ta lahtre ki hei ni di u kpa wo mbu ni wo timbu, wato yesu christy wa wu di riri wa ana latre na.
Watoto wangu, ninawaandikieni mambo haya, kusudi msitende dhambi. Lakini, ikijatokea mtu akatenda dhambi, tunaye mmoja ambaye hutuombea kwa Baba, ndiye Yesu Kristo aliye mwadilifu kabisa.
2 Wa wu yi ni wur latre mbu laga ana'u mbu ni klembu na u gbugbu wawu.
Kristo ndiye sadaka iondoayo dhambi zetu; wala si dhambi zetu sisi tu, bali pia dhambi za ulimwengu wote.
3 Kitoh di ki ye toh idan ki u tre ma.
Tukizitii amri za Mungu, basi, tunaweza kuwa na hakika kwamba tunamjua.
4 Indi wa atre di wawu toh Irji da na hu tre ma na a hi di wu che u jaji na hei ni suron ma na.
Mtu akisema kwamba anamjua, lakini hazitii amri zake, basi mtu huyo ni mwongo, na ukweli haumo ndani yake.
5 Indi wa a grji trema jaji hei wu ni Irji. Na yi ki toh di ki hei tare ni wu.
Lakini mtu yeyote anayeshika neno la Mungu, huyo ndiye aliye na upendo kamili wa Mungu ndani yake. Hivi ndivyo tunavyoweza kuwa na hakika kwamba tunaungana naye:
6 Indi wa a tre di wa wu hei ni. Irji ka zre na wawu a zre a.
mtu yeyote anayesema kwamba ameungana na Mungu, anapaswa kuishi kama alivyoishi Yesu Kristo.
7 Mir ya, mina si han tre sisa ma ni yu'u na ahi cihe tre wa bi woh rimumal chiche tre a hi tre wa bi wo'a.
Wapenzi wangu, amri hii ninayowaandikieni si amri mpya; ni amri ileile ya zamani mliyokuwa nayo tangu mwanzo. Amri hiyo ya zamani ni ule ujumbe mliousikia.
8 Misi han tre sa ma ni yu'u wa a jaji ni mi kristi ni mi mbi me, don ibwu a zren ka si hi kpama. u kpan u jaji a si kpan
Hata hivyo, amri hii ninayowaandikieni ni amri mpya, na ukweli wake unaonekana ndani ya Kristo na ndani yenu pia. Maana giza linatoweka, na mwanga wa ukweli umekwisha anza kuangaza.
9 Indi wa a tre di wawu hei ni mi kpan, da ni kran vayi ma ahei ni mi bwu, da si zre ni mi bwu har ni zizah.
Yeyote asemaye kwamba yumo katika mwanga, lakini anamchukia ndugu yake, mtu huyo bado yumo gizani.
10 Indi wa a ni yiem vayi ma ahei ni mi kpan, ama kub zah na.
Yeyote ampendaye ndugu yake, yuko katika mwanga, na hamna chochote ndani yake kiwezacho kumkwaza mtu mwingine.
11 Naki, i wa a nikra vayi ma ahei ni mi bwu da si zre ni mi bwu a na ton bubu wa a si hi na; don ibwu a ka shishi ma.
Lakini anayemchukia ndugu yake, yumo gizani; anatembea gizani, na hajui anakokwenda, maana giza limempofusha.
12 Mi si han ni yu'u mri, ba wur lahtre mbi hie ni yu'u ni tu de ma.
Ninawaandikieni ninyi watoto, kwa kuwa dhambi zenu zimeondolewa kwa jina la Kristo.
13 Mi si han ni yu'u bati dan bi yi bi toh wa ahei rji ni mumla, Mi si han ni yu'u mri ze don bi zan gbe ngbenlen ibrji, mi han ni yu'u mri don bi toh ti'a.
Nawaandikieni ninyi kina baba kwani mnamjua yeye ambaye amekuwako tangu mwanzo, Nawaandikieni ninyi vijana kwa sababu mmemshinda yule Mwovu.
14 Mi riga nan ni yuwu ba ti don bi toh ndia rji ni mumla, Mi riga han ni yu'u mrize don bi hei ni gbengbenlen, u tre Irji a hei ni yi, na ki bi zan gbengbenlen bi me me dri.
Nawaandikieni ninyi watoto, kwa sababu mnamjua Baba. Nawaandikieni ninyi kina baba, kwa kuwa mnamjua yeye ambaye amekuwako tangu mwanzo. Nawaandikieni ninyi vijana kwa sababu mna nguvu; neno la Mungu limo ndani yenu na mmemshinda yule Mwovu.
15 Na kpayiem ni kpi gbugbulu na, ni kpi bi wa ba hei ni mi gbugbulu 'a indi wa a ni son gbugbulu, i son 'u Irji na ni 'u na.
Msiupende ulimwengu, wala chochote kilicho cha ulimwengu. Mtu anayeupenda ulimwengu, upendo wa Baba hauwezi kuwamo ndani yake.
16 Du ikpi bi wa ba hei ni mi gbugbulu, ba bi nma kpa ba vo shishi, ni bi kpa di tsri, nu zu tu ba na rji ni ti na ba rji ni gbugbulu.
Vitu vyote vya ulimwengu-tamaa mbaya za mwili, vitu wanavyoviona watu na kuvitamani, majivuno yasababishwayo na mali-vyote hivyo havitoki kwa Baba, bali vyatoka kwa ulimwengu.
17 Gbugbulun ni kpi bi wa a ni son ba si kle, indi wa a si ti du ni tre rji a ni son seisei nisei. (aiōn g165)
Ulimwengu pamoja na vitu vyake vyote vyenye kutamanika unapita; lakini mtu atendaye atakalo Mungu, anaishi milele. (aiōn g165)
18 Imir itoh a ye 'u kle, na wa bi woh bi kran kristi ba si ye zizan gbugbu'u ba ye. Na ki bi ka toh di itoh ye kle.
Watoto, mwisho u karibu! Mlikwisha sikia kwamba adui wa Kristo anakuja, na sasa adui wengi wa Kristo wamekwisha fika, na hivyo twajua kwamba mwisho u karibu.
19 Ba ryu ni mi mbu iki tsro di ba na hei ni ta na. Bana hei ni ta ba na san ni ta, da ba ni kpaba a tsro di bana hei ni ta na.
Watu hao wametokea kati yetu lakini hawakuwa kweli wa kwetu na ndiyo maana walituacha; Kama wangalikuwa wa kwetu, wangalibaki nasi. Lakini waliondoka, wakaenda zao, kusudi ionekane wazi kwamba hawakuwa kamwe wa kwetu.
20 Bi hei ni anointing u rji ni tsa tsra ka bi toh wa wu bi.
Ninyi, lakini, mlipata kumiminiwa Roho Mtakatifu na Kristo, na hivyo mnaujua ukweli.
21 Mi na han ni yuu di bina toh jaji na naki bi toh'o, iche na hei ni mi jaji na.
Basi, nawaandikieni, si kwa kuwa hamuujui ukweli, bali kwa sababu mnaujua; na pia mnajua kwamba uongo wowote haupatikani katika ukweli.
22 A hi gha hi ndi u'iche, a hi ndi wa ana kpayiem ni yesu da kristi na ndi ki ma hi wa ba kran yesu, wa ana toh ti'a mba ver a na.
Mwongo ni nani? Ni yule anayekana kwamba Yesu ni Masiha. Mtu wa namna hiyo ni adui wa Kristo—anamkana Baba na Mwana.
23 Indi wa ana yeini ni vre'a na a nato ti'a na. Indi wa a buh yun ma da kpa vre'a hei ni ti'a game.
Maana yeyote anayemkana Mwana, anamkana pia Baba; na yeyote anayemkubali Mwana, anampata Baba pia.
24 Naki iwu du kpi wa'u woh rji ni mumla krie ni'u inde kpi wa u woh rji ni mumla ahei ni wu, in u' wu hei ni vre ba tima game.
Basi, ujumbe ule mliousikia tangu mwanzo na ukae mioyoni mwenu. Kama ujumbe huo mliousikia tangu mwanzo ukikaa ndani yenu, basi, mtaishi daima katika umoja na Mwana na Baba.
25 Wa yi hi ikpie wa a chu yun ni ta wu ire u tutru. (aiōnios g166)
Na ahadi aliyotuahidia sisi ndiyo hii: uzima wa milele. (aiōnios g166)
26 Me han kpi bi yi yiwu du bari gru ye yi you ni nkon meme ma na.
Nimewaandikieni mambo haya kuhusu wale wanaotaka kuwapotosha ninyi.
27 Naki u' ikpie wa'u kpa ni wu ahei ni wu, wuna si wa indio du ye tsro u na du Ruhu ma wa wu kpa tsro kpe ba wawu wa ba jaji bana che na, ni yada a tsro u son ni'u na ki me.
Lakini, kwa upande wenu ninyi, Kristo aliwamiminieni Roho wake. Na kama akiendelea kukaa ndani yenu, hamhitaji kufundishwa na mtu yeyote. Maana Roho wake anawafundisheni kila kitu na mafundisho yake ni ya kweli, si ya uongo. Basi shikeni mafundisho ya huyo Roho na kubaki katika muungano na Kristo.
28 Zizan mri son naki chachu wa aye ki hei ni gbengbenlen, ana shan ni tita niye ma na.
Naam, watoto, kaeni ndani yake kusudi wakati atakapotokea tuwe hodari bila kuwa na sababu ya kujificha kwa aibu Siku ya kuja kwake.
29 Inde wu toh da a hei ni kiklan suron, u ka toh di indi wa ani ti kpe wa a zizi ba grji di ki ma ni'u.
Mnajua kwamba Kristo ni mwadilifu kabisa; basi, mnapaswa kujua pia kwamba kila mtu atendaye mambo adili ni mtoto wa Mungu.

< 1 Yohana 2 >