< ܒ-ܛܝܡܬܐܘܣ 4 >

ܡܤܗܕ ܐܢܐ ܠܟ ܩܕܡ ܐܠܗܐ ܘܡܪܢ ܝܫܘܥ ܡܫܝܚܐ ܗܘ ܕܥܬܝܕ ܠܡܕܢ ܚܝܐ ܘܡܝܬܐ ܒܓܠܝܢܐ ܕܡܠܟܘܬܗ 1
Nakuamuru mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu atakayewahukumu watu walio hai na wafu, na kwa sababu anakuja kutawala akiwa Mfalme:
ܐܟܪܙ ܡܠܬܐ ܘܩܘܡ ܒܚܦܝܛܘܬܐ ܒܙܒܢܐ ܘܕܠܐ ܙܒܢܐ ܐܟܤ ܘܟܘܢ ܒܟܠܗ ܡܓܪܬ ܪܘܚܐ ܘܝܘܠܦܢܐ 2
hubiri huo ujumbe, sisitiza kuutangaza (iwe ni wakati wa kufaa au wakati usiofaa), karipia, onya na himiza watu ukiwafundisha kwa uvumilivu wote.
ܢܗܘܐ ܓܝܪ ܙܒܢܐ ܕܠܝܘܠܦܢܐ ܚܠܝܡܐ ܠܐ ܢܫܬܡܥܘܢ ܐܠܐ ܐܝܟ ܪܓܝܓܬܗܘܢ ܢܤܓܘܢ ܠܢܦܫܗܘܢ ܡܠܦܢܐ ܒܚܘܬܚܬܐ ܕܡܫܡܥܬܗܘܢ 3
Utakuja wakati ambapo watu hawatasikiliza mafundisho ya kweli, ila watafuata tamaa zao wenyewe na kujikusanyia walimu tele watakaowaambia mambo yale tu ambayo masikio yao yako tayari kusikia.
ܘܡܢ ܫܪܪܐ ܢܗܦܟܘܢ ܐܕܢܗܘܢ ܠܫܘܥܝܬܐ ܕܝܢ ܢܤܛܘܢ 4
Watakataa kuusikia ukweli, watageukia hadithi za uongo.
ܐܢܬ ܕܝܢ ܗܘܝܬ ܥܝܪ ܒܟܠܡܕܡ ܘܤܝܒܪ ܒܝܫܬܐ ܘܥܒܕܐ ܥܒܕ ܕܡܤܒܪܢܐ ܘܬܫܡܫܬܟ ܫܠܡ 5
Wewe, lakini, uwe macho katika kila hali; vumilia mateso, fanya kazi ya mhubiri wa Habari Njema, timiza kikamilifu utumishi wako.
ܐܢܐ ܓܝܪ ܡܟܝܠ ܡܬܢܩܐ ܐܢܐ ܘܙܒܢܐ ܕܐܫܬܪܐ ܡܛܐ 6
Kwa upande wangu mimi, niko karibu kabisa kutolewa dhabihu na wakati wa kufariki kwangu umefika.
ܐܓܘܢܐ ܫܦܝܪܐ ܐܬܟܬܫܬ ܘܪܗܛܝ ܫܠܡܬ ܘܗܝܡܢܘܬܝ ܢܛܪܬ 7
Nimefanya bidii katika mashindano, nimemaliza safari yote na imani nimeitunza.
ܘܡܢ ܗܫܐ ܢܛܝܪ ܠܝ ܟܠܝܠܐ ܕܟܐܢܘܬܐ ܕܢܦܪܥܝܘܗܝ ܠܝ ܡܪܝ ܒܝܘܡܐ ܗܘ ܕܗܘܝܘ ܕܝܢܐ ܟܐܢܐ ܠܐ ܕܝܢ ܒܠܚܘܕ ܠܝ ܐܠܐ ܐܦ ܠܐܝܠܝܢ ܕܐܚܒܘ ܠܓܠܝܢܗ 8
Na sasa imebakia tu kupewa tuzo la ushindi kwa maisha ya uadilifu, tuzo ambalo Bwana Hakimu wa haki, atanipa mimi Siku ile na wala si mimi tu, ila na wale wote wanaotazamia kwa upendo kutokea kwake.
ܢܬܒܛܠ ܠܟ ܕܬܐܬܐ ܠܘܬܝ ܒܥܓܠ 9
Fanya bidii kuja kwangu karibuni.
ܕܡܐ ܓܝܪ ܫܒܩܢܝ ܘܐܚܒ ܥܠܡܐ ܗܢܐ ܘܐܙܠ ܠܗ ܠܬܤܠܘܢܝܩܐ ܩܪܤܩܘܤ ܠܓܠܛܝܐ ܛܛܘܤ ܠܕܠܡܛܝܐ (aiōn g165) 10
Dema ameupenda ulimwengu huu akaniacha na kwenda zake Thesalonike. Kreske amekwenda Galatia, na Tito amekwenda Dalmatia. (aiōn g165)
ܠܘܩܐ ܗܘ ܒܠܚܘܕܘܗܝ ܥܡܝ ܠܡܪܩܘܤ ܕܒܪ ܘܐܝܬܝܗܝ ܥܡܟ ܥܗܢ ܠܝ ܓܝܪ ܠܬܫܡܫܬܐ 11
Luka peke yake ndiye aliye hapa pamoja nami. Mpate Marko uje naye, kwa maana ataweza kunisaidia katika kazi yangu.
ܠܛܘܟܝܩܘܤ ܕܝܢ ܫܕܪܬ ܠܐܦܤܘܤ 12
Nilimtuma Tukiko kule Efeso.
ܒܝܬ ܟܬܒܐ ܕܝܢ ܕܫܒܩܬ ܒܛܪܘܐܘܤ ܠܘܬ ܩܪܦܘܤ ܡܐ ܕܐܬܐ ܐܢܬ ܐܝܬܝܗܝ ܘܟܬܒܐ ܝܬܝܪܐܝܬ ܟܪܟܐ ܕܡܓܠܐ 13
Utakapokuja niletee koti langu nililoacha kwa Karpo kule Troa; niletee pia vile vitabu, na hasa vile vilivyotengenezwa kwa ngozi.
ܐܠܟܤܢܕܪܤ ܩܝܢܝܐ ܒܝܫܬܐ ܤܓܝܐܬܐ ܚܘܝܢܝ ܦܪܥ ܠܗ ܡܪܢ ܐܝܟ ܥܒܕܘܗܝ 14
Yule sonara aitwaye Aleksanda amenitendea maovu mengi; Bwana atamlipa kufuatana na hayo matendo yake.
ܐܦ ܐܢܬ ܕܝܢ ܐܙܕܗܪ ܡܢܗ ܛܒ ܓܝܪ ܙܩܝܦ ܠܘܩܒܠ ܡܠܝܢ 15
Jihadhari naye kwa sababu aliupinga ujumbe wetu kwa ukali.
ܒܡܦܩ ܒܪܘܚܝ ܩܕܡܝܐ ܠܐ ܐܢܫ ܗܘܐ ܥܡܝ ܐܠܐ ܟܠܗܘܢ ܫܒܩܘܢܝ ܠܐ ܬܬܚܫܒ ܠܗܘܢ ܗܕܐ 16
Wakati nilipojitetea kwa mara ya kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu; wote waliniacha. Mungu asiwahesabie kosa hilo!
ܡܪܝ ܕܝܢ ܩܡ ܠܝ ܘܚܝܠܢܝ ܕܒܝ ܟܪܘܙܘܬܐ ܬܫܬܠܡ ܘܢܫܡܥܘܢ ܥܡܡܐ ܟܠܗܘܢ ܕܐܬܦܨܝܬ ܡܢ ܦܘܡܐ ܕܐܪܝܐ 17
Lakini, Bwana alikaa pamoja nami, akanipa nguvu, hata nikaweza kuutangaza ujumbe wote, watu wa mataifa wausikie; tena nikaokolewa katika hukumu ya kifo kama kinywani mwa simba.
ܘܢܦܨܝܢܝ ܡܪܝ ܡܢ ܟܠ ܥܒܕ ܒܝܫ ܘܢܚܝܢܝ ܒܡܠܟܘܬܗ ܕܒܫܡܝܐ ܕܠܗ ܫܘܒܚܐ ܠܥܠܡ ܥܠܡܝܢ ܐܡܝܢ (aiōn g165) 18
Bwana ataniokoa na mambo yote maovu, na kunichukua salama mpaka katika Utawala wake wa mbinguni. Kwake uwe utukufu milele na milele! Amina. (aiōn g165)
ܗܒ ܫܠܡܐ ܠܦܪܝܤܩܠܐ ܘܠܐܩܠܘܤ ܘܠܒܝܬܐ ܕܐܢܤܝܦܘܪܘܤ 19
Wasalimu Priska na Akula, pamoja na jamaa ya Onesiforo.
ܐܪܤܛܘܤ ܦܫ ܠܗ ܒܩܘܪܢܬܘܤ ܛܪܘܦܝܡܘܤ ܕܝܢ ܫܒܩܬܗ ܟܕ ܟܪܝܗ ܒܡܝܠܝܛܘܤ ܡܕܝܢܬܐ 20
Erasto alibaki Korintho, naye Trofimo nilimwacha Mileto kwa sababu alikuwa mgonjwa.
ܢܬܒܛܠ ܠܟ ܕܩܕܡ ܤܬܘܐ ܬܐܬܐ ܫܐܠ ܒܫܠܡܟ ܐܘܒܘܠܘܤ ܘܦܘܕܤ ܘܠܝܢܘܤ ܘܩܠܘܕܝܐ ܘܐܚܐ ܟܠܗܘܢ 21
Fanya bidii kuja kabla ya majira ya baridi. Ebulo, Pude, Lino na Klaudia wanakusalimu; vilevile ndugu wengine wote.
ܡܪܢ ܝܫܘܥ ܡܫܝܚܐ ܥܡ ܪܘܚܟ ܛܝܒܘܬܐ ܥܡܟ ܐܡܝܢ 22
Bwana awe nawe rohoni mwako. Nawatakieni nyote neema.

< ܒ-ܛܝܡܬܐܘܣ 4 >