< ܒ-ܩܘܪ̈ܝܢܬܝܐ 6 >
ܘܐܝܟ ܡܥܕܪܢܐ ܒܥܝܢܢ ܡܢܟܘܢ ܕܠܐ ܬܤܬܪܩ ܒܟܘܢ ܛܝܒܘܬܐ ܕܐܠܗܐ ܕܩܒܠܬܘܢ | 1 |
Na kwa hiyo, kufanya kazi pamoja, tunawasihi ninyi msiipokee neema ya Mungu pasipo matokeo.
ܐܡܪ ܓܝܪ ܕܒܙܒܢܐ ܡܩܒܠܐ ܥܢܝܬܟ ܘܒܝܘܡܐ ܕܚܝܐ ܥܕܪܬܟ ܗܐ ܗܫܐ ܙܒܢܐ ܡܩܒܠܐ ܘܗܐ ܗܫܐ ܝܘܡܐ ܕܚܝܐ | 2 |
Kwa kuwa anasema, “Wakati uliokubalika nilikuwa makini kwenu, na katika siku ya wokovu niliwasaidia.” Tazama, sasa ni wakati uliokubalika. Tazama, sasa ni siku ya wokovu.
ܠܡܐ ܒܡܕܡ ܬܬܠܘܢ ܠܐܢܫ ܥܠܬܐ ܕܬܘܩܠܬܐ ܕܠܐ ܢܗܘܐ ܡܘܡܐ ܒܬܫܡܫܬܢ | 3 |
Hatuweki jiwe la kizuizi mbele ya mtu yeyote, kwa kuwa hatuitakii huduma yetu iletwe katika sifa mbaya.
ܐܠܐ ܒܟܠ ܡܕܡ ܢܚܘܐ ܢܦܫܢ ܕܡܫܡܫܢܐ ܚܢܢ ܕܐܠܗܐ ܒܡܤܝܒܪܢܘܬܐ ܤܓܝܐܬܐ ܒܐܘܠܨܢܐ ܒܐܢܢܩܤ ܒܚܒܘܫܝܐ | 4 |
Badala yake, tunajihakiki wenyewe kwa matendo yetu yote, kwamba tu watumishi wa Mungu. Tu watumishi wake katika wingi wa ustahimilivu, mateso, dhiki, ugumu wa maisha,
ܒܢܓܕܐ ܒܐܤܘܪܐ ܒܫܓܘܫܝܐ ܒܠܐܘܬܐ ܒܫܗܪܐ ܒܨܘܡܐ | 5 |
kupigwa, vifungo, ghasia, katika kufanya kazi kwa bidii, katika kukosa usingizi usiku, katika njaa,
ܒܕܟܝܘܬܐ ܒܝܕܥܬܐ ܒܢܓܝܪܘܬ ܪܘܚܐ ܒܒܤܝܡܘܬܐ ܒܪܘܚܐ ܕܩܘܕܫܐ ܒܚܘܒܐ ܕܠܐ ܢܟܠܐ | 6 |
katika usafi, maarifa, uvumilivu, wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo halisi.
ܒܡܠܬܐ ܕܩܘܫܬܐ ܒܚܝܠܐ ܕܐܠܗܐ ܒܙܝܢܐ ܕܙܕܝܩܘܬܐ ܕܒܝܡܝܢܐ ܘܒܤܡܠܐ | 7 |
Tu watumishi wake katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu. Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kuuume na wa kushoto.
ܒܫܘܒܚܐ ܘܒܨܥܪܐ ܒܩܘܠܤܐ ܘܒܓܘܢܝܐ ܐܝܟ ܡܛܥܝܢܐ ܘܫܪܝܪܐ | 8 |
Tunafanya kazi katika heshima na kudharauliwa, katika kashfa na sifa. Tunatuhumiwa kuwa wadanganyifu na wakati tu wakweli.
ܐܝܟ ܠܐ ܝܕܝܥܐ ܘܝܕܝܥܝܢܢ ܐܝܟ ܡܝܬܝܢܢ ܘܗܐ ܚܝܝܢ ܚܢܢ ܐܝܟ ܕܡܬܪܕܝܢܢ ܘܠܐ ܡܝܬܝܢܢ | 9 |
Tunafanya kazi kana kwamba hatujulikani na bado tunajulikana vizuri. Tunafanya kazi kama wanaokufa na -Tazama! - bado tunaishi. Tunafanya kazi kama tunaoadhibiwa kwa ajili ya matendo yetu lakini sio kama waliohukumiwa hata kufa.
ܐܝܟ ܕܟܪܝܐ ܠܢ ܘܒܟܠܙܒܢ ܚܕܝܢܢ ܐܝܟ ܡܤܟܢܐ ܘܠܤܓܝܐܐ ܡܥܬܪܝܢܢ ܐܝܟ ܕܡܕܡ ܠܝܬ ܠܢ ܘܟܠ ܡܕܡ ܐܚܝܕܝܢܢ | 10 |
Tunafanya kazi kama wenye masikitiko, lakini siku zote tuna furaha. Tunafanya kazi kama maskini, lakini tunatajirisha wengi. Tunafanya kazi kana kwamba hatupati kitu bali kama tunaomiliki kila kitu.
ܦܘܡܢ ܦܬܝܚ ܗܘ ܠܘܬܟܘܢ ܩܘܪܢܬܝܐ ܘܠܒܢ ܪܘܝܚ | 11 |
Tumezungumza ukweli wote kwenu, Wakorintho, na mioyo yetu imefunguka kwa upana.
ܠܐ ܐܠܝܨܝܬܘܢ ܒܢ ܐܠܝܨܝܬܘܢ ܕܝܢ ܒܪܚܡܝܟܘܢ | 12 |
mioyo yenu haizuiliwi na sisi, bali mnazuiliwa na hisia zenu wenyewe.
ܐܝܟ ܕܠܒܢܝܐ ܕܝܢ ܐܡܪ ܐܢܐ ܦܘܪܥܘܢܝ ܚܘܒܠܝ ܕܠܘܬܟܘܢ ܘܪܘܚܘ ܚܘܒܟܘܢ ܠܘܬܝ | 13 |
Sasa katika kubadilishana kwa haki - ninaongea kama kwa watoto - fungueni mioyo yenu kwa upana.
ܘܠܐ ܬܗܘܘܢ ܒܢܝ ܙܘܓܐ ܠܐܝܠܝܢ ܕܠܐ ܡܗܝܡܢܝܢ ܐܝܕܐ ܓܝܪ ܫܘܬܦܘܬܐ ܐܝܬ ܠܙܕܝܩܘܬܐ ܥܡ ܥܘܠܐ ܐܘ ܐܝܢܐ ܚܘܠܛܢܐ ܐܝܬ ܠܢܗܝܪܐ ܥܡ ܚܫܘܟܐ | 14 |
Msifungamanishwe pamoja na wasioamini. Kwa kuwa kuna uhusiano gani kati ya haki na uasi? Na kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?
ܐܘ ܐܝܕܐ ܫܠܡܘܬܐ ܐܝܬ ܠܡܫܝܚܐ ܥܡ ܤܛܢܐ ܐܘ ܐܝܕܐ ܡܢܬܐ ܐܝܬ ܠܕܡܗܝܡܢ ܥܡ ܕܠܐ ܡܗܝܡܢ | 15 |
Ni makubaliano gani Kristo anaweza kuwa nayo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na asiyeamini?
ܐܝܕܐ ܕܝܢ ܐܘܝܘܬܐ ܐܝܬ ܠܗܝܟܠܗ ܕܐܠܗܐ ܥܡ ܕܫܐܕܐ ܐܢܬܘܢ ܕܝܢ ܗܝܟܠܗ ܐܢܬܘܢ ܕܐܠܗܐ ܚܝܐ ܐܝܟܢܐ ܕܐܡܝܪ ܕܐܥܡܪ ܒܗܘܢ ܘܐܗܠܟ ܒܗܘܢ ܘܐܗܘܐ ܐܠܗܗܘܢ ܘܗܢܘܢ ܢܗܘܘܢ ܠܝ ܥܡܐ | 16 |
Na kuna makubaliano gani yapo kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai, kama ambavyo Mungu alisema: “Nitakaa kati yao na kutembea kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
ܡܛܠ ܗܢܐ ܦܘܩܘ ܡܢ ܒܝܢܬܗܘܢ ܘܐܬܦܪܫܘ ܡܢܗܘܢ ܐܡܪ ܡܪܝܐ ܘܠܛܡܐܐ ܠܐ ܬܬܩܪܒܘܢ ܘܐܢܐ ܐܩܒܠܟܘܢ | 17 |
Kwa hiyo, “Tokeni kati yao, na mkatengwe nao,” asema Bwana. “Msiguse kitu kichafu, na nitawakaribisha ninyi.
ܘܐܗܘܐ ܠܟܘܢ ܠܐܒܐ ܘܐܢܬܘܢ ܬܗܘܘܢ ܠܝ ܠܒܢܝܐ ܘܠܒܢܬܐ ܐܡܪ ܡܪܝܐ ܕܟܠ ܐܚܝܕ | 18 |
Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa wanangu wa kiume na wa kike,” asema Bwana Mwenyezi.