< إِشَعْيَاءَ 20 >
فِي سَنَةِ مَجِيءِ تَرْتَانَ إِلَى أَشْدُودَ، حِينَ أَرْسَلَهُ سَرْجُونُ مَلِكُ أَشُّورَ فَحَارَبَ أَشْدُودَ وَأَخَذَهَا، | ١ 1 |
Katika mwaka ambao Tartani alipofika kwa Ashdodi, alipotumwa na Sarjoni mfalme wa Asiria, nae akapigana na Ashdodd na akachukua.
فِي ذَلِكَ ٱلْوَقْتِ تَكَلَّمَ ٱلرَّبُّ عَنْ يَدِ إِشَعْيَاءَ بْنِ آمُوصَ قَائِلًا: «اِذْهَبْ وَحُلَّ ٱلْمِسْحَ عَنْ حَقْوَيْكَ وَٱخْلَعْ حِذَاءَكَ عَنْ رِجْلَيْكَ». فَفَعَلَ هَكَذَا وَمَشَى مُعَرًّى وَحَافِيًا. | ٢ 2 |
Mda huo Yahwe alizungumza na Isaya mwana wa Amozi, ''Nenda ukaondoe nguo za magunia katika kiuno chako, na ondoeni viatu vyenu kwenye miguu.'' Alifanya hivyo, tembeeni uchi na miguu wazi.
فَقَالَ ٱلرَّبُّ: «كَمَا مَشَى عَبْدِي إِشَعْيَاءُ مُعَرًّى وَحَافِيًا ثَلَاثَ سِنِينٍ، آيَةً وَأُعْجُوبَةً عَلَى مِصْرَ وَعَلَى كُوشَ، | ٣ 3 |
Yahwe asema, ''Kama ilivyokuwa kwa mtumishi wangu Isaya alivyotembea uchi na pasipo kuvaa viatu kwa miaka mitatu, ni ishara na dalili kuhusu Misri na kuhusu Ethiopia—
هَكَذَا يَسُوقُ مَلِكُ أَشُّورَ سَبْيَ مِصْرَ وَجَلَاءَ كُوشَ، ٱلْفِتْيَانَ وَٱلشُّيُوخَ، عُرَاةً وَحُفَاةً وَمَكْشُوفِي ٱلْأَسْتَاهِ خِزْيًا لِمِصْرَ. | ٤ 4 |
katika njia hii mfalme wa Asiria atawaongoza mateka wa Misri, na walioko uhamishoni Ethiopia, watoto kwa wazee, waliouchi na wasio na viatu, na ambao hawajajisitiri kuiweka Misri katika aibu.
فَيَرْتَاعُونَ وَيَخْجَلُونَ مِنْ أَجْلِ كُوشَ رَجَائِهِمْ، وَمِنْ أَجْلِ مِصْرَ فَخْرِهِمْ. | ٥ 5 |
Watafadhaika na kuona aibu, kwa sababu ya Ethiopia ni matumaini yao na Misri ni utukufu wao.
وَيَقُولُ سَاكِنُ هَذَا ٱلسَّاحِلِ فِي ذَلِكَ ٱلْيَوْمِ: هُوَذَا هَكَذَا مَلْجَأُنَا ٱلَّذِي هَرَبْنَا إِلَيْهِ لِلْمَعُونَةِ لِنَنْجُو مِنْ مَلِكِ أَشُّورَ، فَكَيْفَ نَسْلَمُ نَحْنُ؟». | ٦ 6 |
Wenyeji wa pwani hiiwatasema siku hiyo, 'Kweli, hichi ndicho chanzo chetu cha matumaini, tulipokimbilia kuhitaji msaada kutoka kwa mfalme wa Asiria, je ni kwa jisi gani tunaweza kupona?''