< Yakobo 3 >
1 Ndugu zangu, wengi wenu msiwe walimu. Kama mjuavyo, sisi walimu tutapata hukumu kubwa zaidi kuliko wengine.
Not many should become teachers, my brothers, knowing that we will receive greater judgment.
2 Lakini kama mtu hakosi katika usemi wake, basi, huyo ni mkamilifu, na anaweza kutawala nafsi yake yote.
For we all stumble in many things. If any man does not stumble in word, this is a perfect man, able also to bridle the whole body.
3 Sisi huwatia farasi lijamu kinywani mwao ili watutii; na kwa njia hiyo twaweza kuwaongoza kokote tunakotaka.
Behold we put bits into the mouths of horses for them to obey us, and we guide about their whole body.
4 Meli nazo pia, ingawa ni kubwa sana, na husukumwa na upepo mkali, huweza kugeuzwa kwa usukani mdogo sana, zikaelekea kokote nahodha anakotaka.
Behold also the ships, being so great and driven by fierce winds, are guided about by a very small rudder, wherever the impulse of the man who steers determines.
5 Vivyo hivyo, ulimi, ingawa ni kiungo kidogo cha mwili, hujisifia makuu sana. Moto mdogo waweza kuteketeza msitu mkubwa.
So also the tongue is a little body-part, and boasts greatly. Behold a little fire, how much wood it kindles.
6 Hali kadhalika ulimi ni kama moto. Umejaa maovu chungu nzima, unayo nafasi yake katika miili yetu na hueneza ubaya katika nafsi zetu zote. Huteketeza maisha yetu yote kwa moto utokao Jehanamu kwenyewe. (Geenna )
And the tongue is a fire, the world of unrighteousness. Thus, the tongue is made to lead among our body-parts, defiling the whole body, and setting the cycle of nature on fire, and being set on fire by hell. (Geenna )
7 Binadamu anaweza kuwafuga wanyama, na amefaulu kufuga viumbe vyote—wanyama wa mwituni, ndege, nyoka na viumbe vya baharini.
For every species, both of beasts and of birds, both of creeping things and things in the sea, is tamed, and has been tamed by the human species.
8 Lakini hakuna mtu aliyeweza kuufuga ulimi. Ulimi ni kitu kiovu, hakitawaliki, na kimejaa sumu inayoua.
But no man is able to tame the tongue of men, an unruly evil, full of deadly poison.
9 Kwa ulimi sisi twamshukuru Bwana na Baba yetu. Kwa ulimi huohuo twawalaani watu, watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.
By it we bless the God and Father, and by it we curse men, who were made according to a likeness of God.
10 Maneno ya laana na ya kusifia hutoka katika kinywa kimoja. Ndugu zangu, mambo haya hayapaswi kuwa hivyo.
Out of the same mouth proceeds blessing and curse. My brothers, these things ought not to happen this way.
11 Je, chemchemi moja yaweza kutoa maji matamu na maji machungu pamoja?
Does the spring pour out from the same opening the sweet and the bitter?
12 Ndugu zangu, je, mti wa mtini waweza kuzaa zeituni? Au, mzabibu waweza kuzaa tini? Chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu.
A fig tree, my brothers, cannot make olives, or a grapevine figs. In the same way, no one spring makes water salty and sweet.
13 Je, ni nani mwenye hekima na akili miongoni mwenu? Basi, aonyeshe jambo hilo kwa mwenendo wake mzuri na kwa matendo yake mema yanayofanyika kwa unyenyekevu na hekima.
Who is wise and understanding among you? Let him show from his good behavior his works in meekness of wisdom.
14 Lakini ikiwa mioyo yenu imejaa wivu, chuki na ubinafsi, basi, msijisifu na kusema uongo dhidi ya ukweli.
But if ye have bitter envy and selfish ambition in your heart, do not boast, and do not lie against the truth.
15 Hekima ya namna hiyo haitoki juu mbinguni; hekima hiyo ni ya ulimwengu, na ya kidunia, tena ni ya kishetani.
This wisdom is not descending from above, but is earthly, world-soul, demonic.
16 Maana popote palipo na wivu na ubinafsi hapo pana fujo na kila aina ya uovu.
For where envy and selfish ambition are, there is instability and every evil deed.
17 Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki.
But the wisdom from above is indeed first pure, then peaceful, gentle, easily entreated, full of mercy and good fruits, impartial and non-hypocritical.
18 Uadilifu ni mazao ya mbegu ambazo wapenda amani hupanda katika amani.
And the fruit of righteousness is sown in peace to those who make peace.