< Ufunuo 4 >
1 Baada ya mambo haya nilitazama, nikaona kuwa mlango ulikuwa umefunguliwa mbinguni. Ile sauti ya kwanza, ikizungumza nami kama tarumbeta, ikisema, “Njoo hapa, nitakuonesha yatakayotokea baada ya mambo haya.”
ᎣᏂᏃ ᏓᏆᎧᎿᎭᏅᎩ, ᎠᎴ ᎬᏂᏳᏉ ᎦᎶᎯᏍᏗᏱ ᎤᎵᏍᏚᎢᏛ ᎨᏒᎩ ᎦᎸᎳᏗ; ᎢᎬᏱᏱᏃ ᎧᏁᎬ ᎠᏆᏛᎦᏅᎯ ᎠᏤᎷᎩ ᏣᏆᎵᏃᎮᏗᏍᎪ ᎾᏍᎩᏯ ᎨᏒᎩ; ᎯᎠ ᏥᎾᎩᏪᏎᎰᎢ, ᎡᎭᎩᎳᏩ, ᏓᎬᎾᏄᎪᏫᏎᎵᏃ ᏧᏓᎴᏅᏛ ᎾᏍᎩ ᎣᏂ ᎢᏳᎵᏍᏔᏂᏓᏍᏗ ᎨᏒᎢ.
2 Mara moja nilikuwa katika Roho, niliona kulikuwa na kiti cha enzi kimewekwa mbinguni, na mtu amekikalia.
ᎩᎳᏉᏃ ᎢᏴᏛ ᎠᏓᏅᏙ ᎠᏆᏘᏂᏙᎲᎩ; ᎠᎴ ᎬᏂᏳᏉ ᎦᏍᎩᎶ ᎦᎸᎶᎢ ᎤᏂᏍᎩᎳᏛᎩ, ᎩᎶᏃ ᎾᎿᎭᎦᏍᎩᎸ ᎤᏪᏅᎩ.
3 Mmoja aliyekuwa amekikalia alionekana kama jiwe la yaspi na akiki. Kulikuwa na upinde wa mvua umekizunguka kiti cha enzi. Upinde wa mvua ulionekana kama zumaridi.
ᎤᏬᎵᏃ ᏣᎦᎦᏃᏗᏱ ᏣᏍᏆ ᏅᏯ ᎾᏍᎩᏯ ᎨᏒᎩ, ᎠᎴ ᏌᏗᏂ ᏅᏯ; ᎤᏅᎪᏔᏛᎩᏃ ᎬᏩᏚᏫᏛ ᎦᏍᎩᎸᎢ, ᏗᎧᏃᏗᏱ ᎡᎻᎳ ᏅᏯ ᎾᏍᎩᏯ ᎨᏒᎩ.
4 Kukizunguka kiti cha enzi kulikuwa na viti vya enzi vingine ishirini na vinne, na waliokaa kwenye viti vya enzi walikuwa wazee ishirini na wanne, wamevikwa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani mwao.
ᎠᎴ ᎬᏩᏚᏫᏛ ᎾᎿᎭᎦᏍᎩᎸ ᏅᎩᏦᏁ ᏕᎦᎧᎲ ᏗᏍᎩᎳᏗᏍᏗ; ᏗᏍᎩᎳᏗᏍᏗᏱᏃ ᎥᎦᏥᎪᎥᎩ ᏅᎩᏦᏁ ᎢᏯᏂᏛ ᏧᎾᏛᏐᏅᎯ ᎠᏂᏅᎩ ᏧᏁᎬ ᏚᎾᏄᏩᎥᎩ; ᏚᎾᎵᏍᏚᎸᏃ ᏗᎵᏍᏚᎶ ᎠᏕᎸ ᏓᎶᏂᎨ ᏗᎪᏢᏔᏅᎯ.
5 Kutoka katika kiti cha enzi kulitoka miale ya radi, muungurumo na radi. Taa saba zilikuwa zikiwaka mbele ya kiti cha enzi, taa ambazo ni roho saba za Mungu.
ᎦᏍᎩᎸᏃ ᏓᏓᎴᎲᏍᎬᎩ ᎠᎾᎦᎵᏍᎩ, ᎠᎴ ᎠᏴᏓᏆᎶᏍᎩ ᎠᎴ ᎤᏃᏴᎬᎢ; ᎠᎴ ᎦᎵᏉᎩ ᏗᏨᏍᏙᏗ ᏧᏥᏍᏟ ᏓᏓᏪᎵᎩᏍᎬᎩ ᎢᎬᏱᏗᏢ ᎦᏍᎩᎸᎢ, ᎯᎠ ᎾᏍᎩ ᎦᎵᏉᎩ ᏗᏓᏅᏙ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᏧᏤᎵᎦ.
6 Tena mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na bahari, iliyowazi kama kioo. Wote kuzunguka kiti cha enzi kulikuwa na wenye uhai wanne, waliojaa macho mbele na nyuma.
ᎦᏍᎩᎸᏃ ᎢᎬᏱᏗᏢ ᎥᏓᎸᎩ ᎠᏓᎰᏗ ᎢᏗᎬᏤᎵᏛ, ᏅᏯ ᏗᎬᏩᎸᏌᏛ ᎾᏍᎩᏯ ᎨᏒᎩ; ᎦᏍᎩᎸᏃ ᎠᏰᎵ, ᎠᎴ ᎬᏩᏚᏫᏛ ᎾᎿᎭᎦᏍᎩᎸ ᏅᎩ ᎢᏯᏂᏛ ᏗᏅᏃᏛ ᎥᎦᏥᎪᎥᎩ, ᎠᎧᎵᏬᎯ ᏓᏂᎧᏅᎩ ᎢᎬᏱᏗᏢ ᎠᎴ ᎣᏂᏗᏢ.
7 Kiumbe wa kwanza mwenye uhai alikuwa kama simba, kiumbe wa pili mwenye uhai alikuwa kama ndama, kiumbe wa tatu mwenye uhai alikuwa na uso kama wa mwanadamu, na yule mwenye uhai wa nne alikuwa kama tai apaaye.
ᎢᎬᏱᏱ ᎾᏍᎩ ᎯᎠ ᎬᏃᏛ ᏢᏓᏥ ᎤᏃᏕᎾ ᎾᏍᎩᏯ ᎨᏒᎩ, ᏔᎵᏁᏃ ᎾᏍᎩ ᎯᎠ ᎬᏃᏛ ᏩᎦ ᎠᎩᎾ ᎾᏍᎩᏯ ᎨᏒᎩ, ᏦᎢᏁᏃ ᎾᏍᎩ ᎯᎠ ᎬᏃᏛ ᏴᏫ ᎤᎧᏛ ᎾᏍᎩᏯ ᎤᎧᏛᎩ, ᎤᎩᏁᏃ ᎾᏍᎩ ᎯᎠ ᎬᏃᏛ ᎦᏃᎯᎵᏙᎯ ᎠᏬᎭᎵ ᎾᏍᎩᏯ ᎨᏒᎩ.
8 Viumbe wenye uhai wanne kila mmoja alikuwa na mabawa sita, wamejaa macho juu na chini yake. Usiku na mchana hawakomi kusema, “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana Mungu, mtawala juu ya wote, aliyekuwepo, na aliyepo na atakayekuja.”
ᎾᏍᎩᏃ ᏅᎩ ᎢᏯᏂᏛ ᏗᏅᏃᏛ ᎠᏂᏏᏴᏫᎭ ᏑᏓᎵ ᏓᏃᏯᏛᎩ; ᎬᏩᏚᏫᏛᏃ ᎠᎴ ᎭᏫᏂ ᎧᎵᏬᎯ ᎨᏒ ᏗᏂᎧᏅᎢ; ᎠᎴ ᎾᎾᏣᏪᏐᎸᏍᏗᏍᎬᎾ ᎨᏐ ᎢᎦ ᎠᎴ ᏒᏃᏱ ᎯᎠ ᎾᏂᏪᏍᎬᎢ; ᎦᎸᏉᏗᏳ, ᎦᎸᏉᏗᏳ, ᎦᎸᏉᏗᏳ, ᎤᎬᏫᏳᎯ ᎤᏁᎳᏅᎯ ᏫᎾᏍᏛᎾ ᎤᎵᏂᎩᏛ, ᎾᏍᎩ ᏤᎲᎩ, ᎠᎴ ᏤᎭ, ᎠᎴ ᏤᎮᏍᏗ.
9 Kila wakati viumbe wenye uhai walipotoa utukufu, heshima, na kushukuru mbele za aliyekuwa ameketi kwenye hicho kiti cha enzi, yeye aishiye milele na daima, (aiōn )
ᎾᏍᎩᏃ ᏗᏅᏃᏛ ᎠᏂᎸᏉᏓ ᎠᎴ ᎠᎾᎵᎮᎵᏥ ᎾᏍᎩ ᎦᏍᎩᎸ ᎤᏬᎵ, ᎾᏍᎩ ᏂᎪᎯᎸ ᎾᎵᏍᏆᏗᏍᎬᎾ ᏤᎭ, (aiōn )
10 wazee ishirini na wanne walisujudu wenyewe mbele yake aliyekikalia kiti cha enzi. Waliinama chini kwake aishiye milele na daima na kutupa chini taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema, (aiōn )
ᎿᎭᏉ ᏅᎩᏦᏁ ᎢᏯᏂᏛ ᏧᎾᏛᏐᏅᎯ ᎡᎳᏗ ᏓᎾᏓᏅᎥᏍᎪ ᎢᎬᏱᏗᏢ ᎤᏬᎸ ᎾᏍᎩ ᎦᏍᎩᎸ ᎤᏬᎵ, ᎠᎴ ᎠᎾᏓᏙᎵᏍᏓᏁᎰ ᎾᏍᎩ Ꮎ ᏂᎪᎯᎸ ᎾᎵᏍᏆᏗᏍᎬᎾ ᏤᎭ, ᎠᎴ ᏧᎾᎵᏍᏚᎶ ᎦᏍᎩᎸ ᎢᎬᏱᏗᏢ ᏚᎾᏓᎡᎯ, ᎯᎠ ᎾᏂᏪᏍᎪᎢ; (aiōn )
11 “Wastahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu. Kwa kuwa uliviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako, vilikuwepo na viliumbwa.”
ᏰᎵᏉ ᏂᎯ ᏣᎬᏫᏳᎯ ᎦᏰᏣᏁᎢᏍᏓᏁᏗ ᎡᏣᎸᏉᏗᏳ ᎨᏒ, ᎠᎴ ᎡᏣᎸᏉᏙᏗ ᎨᏒ, ᎠᎴ ᏣᎵᏂᎩᏗᏳ ᎨᏒᎢ; ᏂᎦᏗᏳᏰᏃ ᎪᎱᏍᏗ ᏦᏢᏅᎯ, ᎠᎴ ᎭᏓᏅᏖᏍᎬ ᎢᏨᏁᎵᏓᏍᏗᏱ ᎡᎭ, ᎠᎴ ᎪᏢᏅᎯ.