< Zaburi 63 >

1 Mungu, wewe ni Mungu wangu! Ninakutafuta wewe kwa bidii, moyo wangu unakiu yako, mwili wangu unakutamani sana wewe, katika ukame na nchi iliyochoka mahali ambapo hakuna maji.
Zaburi ya Daudi. Wakati alipokuwa katika Jangwa la Yuda. Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu, nakutafuta kwa moyo wote; nafsi yangu inakuonea kiu, mwili wangu unakuonea wewe shauku, katika nchi kame na iliyochoka mahali ambapo hapana maji.
2 Hivyo nimekutafuta wewe katika watu watakatifu kuona nguvu zako na utukufu wako.
Nimekuona katika mahali patakatifu na kuuona uwezo wako na utukufu wako.
3 Kwa sababu uaminifu wa agano lako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakusifu wewe.
Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakuadhimisha.
4 Hivyo nitakutukuza wewe niwapo hai; kwa jina lako nitainua mikono yangu juu.
Nitakusifu siku zote za maisha yangu, na kwa jina lako nitainua mikono yangu.
5 Itakuwa kana kwamba nilikula mlo wa mafuta na wenye kunona, kwa midomo ya furaha kinywa changu kitakusifu wewe,
Nafsi yangu itatoshelezwa kama kwa wingi wa vyakula; kwa midomo iimbayo kinywa changu kitakusifu wewe.
6 nikufikiripo kitandani mwangu na kukutafakari wewe wakati wa saa za usiku.
Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe, ninawaza juu yako makesha yote ya usiku.
7 Kwa maana umekuwa msaada wangu, na katika uvuli wa mbawa zako ninafurahia.
Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu, chini ya uvuli wa mbawa zako naimba.
8 Ninashikamana nawe; mkono wako wa kuume unanisaidia.
Nafsi yangu inaambatana nawe, mkono wako wa kuume hunishika.
9 Lakini wale watafutao kuuharibu uhai wangu wataenda chini kwenye sehemu ya chini kabisa ya nchi;
Wale wanaotafuta uhai wangu wataharibiwa, watakwenda chini kwenye vilindi vya dunia.
10 watakabidhiwa kwa wale ambao mikono yao hutumia upanga, nao watakuwa chakula cha mbweha.
Watatolewa wafe kwa upanga, nao watakuwa chakula cha mbweha.
11 Bali mfalme atashangilia katika Mungu; yeyote anaye apa kupitia yeye atajivunia yeye, lakini vinywa ya wale wasemao uongo watanyamazishwa.
Bali mfalme atafurahi katika Mungu, wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu, bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa.

< Zaburi 63 >