< Zaburi 136 >

1 Oh, mshukuruni Yahwe; kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema.
2 Oh, Mshukuruni Mungu wa miungu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Mshukuruni Mungu wa miungu.
3 Oh, mshukuruni Bwana wa mabwana, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Mshukuruni Bwana wa mabwana:
4 Mshukuruni yeye ambaye peke yake hufanya maajabu makuu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu,
5 Yeye aliyezifanya mbingu kwa hekima zake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu,
6 Mshukuruni yeye alitetandaza nchi juu ya maji, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji,
7 Yeye aliyefanya mianga mikubwa, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Ambaye aliumba mianga mikubwa,
8 Mshukuruni yeye alipaye jua kutawala mchana, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Jua litawale mchana,
9 Mwezi na nyota vitawale usiku, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Mwezi na nyota vitawale usiku,
10 Mshukuruni yeye aliyewaua wazaliwa wa kwanza wa Misri, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri,
11 Akawatoa Waisraeli kati yao, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Na kuwatoa Israeli katikati yao,
12 Kwa mkono hodari na mkono ulio nyooshwa, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa,
13 Mshukuruni yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu,
14 Na kuwapitisha Waisraeli katikati yake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Na kuwapitisha Israeli katikati yake,
15 Lakini akamtupa Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu,
16 Mshukuruni yeye aliye waongoza watu wake jangwani, kwa maana uaminifu wa agano lake ni wa milele.
Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa,
17 Yeye aliyewaua wafalme wakuu, kwa maana uaminifu wa agano lake ni wadumu milele.
Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu,
18 Mshukuruni yeye aliyewaua wafalme maarufu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Naye aliwaua wafalme wenye nguvu,
19 Sihoni mfalme wa Waamori, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Sihoni mfalme wa Waamori,
20 Na Ogu, mfalme wa Bashani, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Ogu mfalme wa Bashani,
21 Mshukuruni yeye aliyewapa nchi yao kama urithi, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Akatoa nchi yao kuwa urithi,
22 Urithi wa Israel mtumishi wake, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Urithi kwa Israeli mtumishi wake,
23 Yeye aliyetukumbuka na kutusaidia katika unyonge wetu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Aliyetukumbuka katika unyonge wetu,
24 Mshukuruni yeye ambaye ametupa ushindi juu ya aui zetu, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Alituweka huru toka adui zetu,
25 Yeye awapaye chakula viumbe hai wote, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Ambaye humpa chakula kila kiumbe.
26 Oh, mshukuruni Mungu wa mbinguni, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
Mshukuruni Mungu wa mbinguni,

< Zaburi 136 >