< Mithali 27 >
1 Usijisifu kwa ajili ya kesho, maana hujui siku italeta nini.
Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja.
2 Mtu mwingine akusifu na wala si kinywa chako mwenyewe, mgeni na wala si midomo yako mwenyewe.
Mwache mwingine akusifu, wala si kinywa chako mwenyewe; mtu mwingine afanye hivyo na si midomo yako mwenyewe.
3 Fikiria uzito wa jiwe na uzito wa mchanga- uchokozi wa mpumbavu ni mzito zaidi kuliko hivyo vyote.
Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo, lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili.
4 Kuna ukatili wenye ghadhabu kali na mafuriko ya hasira, lakini ni nani anayeweza kusimama mbele ya wivu?
Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika, lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu?
5 Ni bora karipio la wazi kuliko upendo uliofichwa.
Afadhali karipio la wazi kuliko upendo uliofichika.
6 Mwaminifu ni jeraha zilizosababishwa na rafiki, lakini adui anaweza kukubusu kwa kuomba radhi mno.
Majeraha kutoka kwa rafiki yaonyesha uaminifu, bali kubusu kwa adui ni kwingi sana.
7 Mtu aliyekula na kushiba hulikataa hata sega la asali, bali kwa mtu mwenye njaa, kila kitu kichungu ni kitamu.
Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali, bali kwa mwenye njaa hata kile kilicho kichungu kwake ni kitamu.
8 Ndege anayezurura kutoka kwenye kiota chake ni kama mtu anayepotea sehemu ambayo anaishi.
Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake, ndivyo alivyo mtu atangatangaye mbali na nyumbani mwake.
9 Pafumu na manukato huufanya moyo ufurahi, lakini utamu wa rafiki ni bora kuliko ushauri wake.
Manukato na uvumba huleta furaha moyoni, nao uzuri wa rafiki huchipuka kutoka kwenye ushauri wake wa uaminifu.
10 Usimwache rafiki yako na rafiki wa baba yako, na usiende kwenye nyumba ya ndugu yako katika siku ya msiba wako. Ni bora rafiki ambaye yupo karibu kuliko ndugu ambaye yupo mbali.
Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako, tena usiende nyumbani mwa ndugu yako wakati umepatwa na maafa. Bora jirani wa karibu kuliko ndugu aliye mbali.
11 Mwanangu, uwe na busara, moyo wangu ufurahi; kisha nitamjibu yule anayenidhihaki.
Mwanangu, uwe na hekima, nawe ulete furaha moyoni mwangu, ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote anitendaye kwa dharau.
12 Mtu mwenye busara huiona taabu na kujificha mwenyewe, lakini mjinga huendelea mbele na kuteseka kwa ajili ya taabu.
Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele nayo ikamtesa.
13 vazi kama mwenyewe anaweka pesa kama dhamana kwa deni la mgeni; lichukue kama anaweka dhamana kwa malaya.
Chukua vazi la yule awekaye dhamana kwa ajili ya mgeni; lishikilie iwe dhamana kama anafanya hivyo kwa ajili ya mwanamke mpotovu.
14 Anayempa jirani yake baraka kwa sauti ya juu mapema asubuhi, baraka hiyo itafikiriwa kuwa laana!
Kama mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu asubuhi na mapema, itahesabiwa kama ni laana.
15 Mke mgomvi ni kama siku ya manyunyu ya mvua ya daima;
Mke mgomvi ni kama matone yasiyokoma ya siku ya mvua.
16 kumzuia ni kama kuuzuia upepo, au kujaribu kushika mafuta kwa mkono wako wa kulia.
Kumzuia yeye ni kama kuuzuia upepo au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono.
17 Chuma hunoa chuma; kwa njia ile ile; mtu humnoa rafiki yake.
Kama vile chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.
18 Yule anayeutunza mtini atakula matunda yake, na yule mwenye kumlinda bwana wake ataheshimiwa.
Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake, naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa.
19 Kama maji yanavyoakisi taswira ya sura ya mtu, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwaksi mtu.
Kama uso uonekanavyo kwenye maji, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonyesha alivyo.
20 Kama kuzimu na Uharibifu havitosheki, ndivyo yalivyo macho ya mtu hayawezi kutosheka. (Sheol )
Kuzimu na Uharibifu havishibi kadhalika macho ya mwanadamu. (Sheol )
21 Kalibu ni kwa fedha na tanuru ni kwa dhahabu; na mtu hujaribiwa anaposifiwa.
Kalibu ni kwa ajili ya fedha na tanuru kwa ajili ya dhahabu, bali mtu hupimwa kwa sifa azipokeazo.
22 Hata kama utamponda mpumbavu kwa mchI- pamoja na nafaka- bado upumbavu wake hautatoka.
Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake.
23 Hakikisha unajua hali ya makundi yako na ujishughulishe juu ya makundi yako,
Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi, angalia kwa bidii ngʼombe zako.
24 maana utajiri haudumu daima. Je taji hudumu kwa vizazi vyote?
Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nayo taji haidumu vizazi vyote.
25 Majani huondoka na ukuaji mpya huonekana na milima ya chakula cha mifugo hukusanywa ndani.
Wakati majani makavu yameondolewa na mapya yamechipua, nayo majani toka milimani yamekusanywa,
26 Wanakondoo watakupatia mavazi yako na mbuzi watakupatia gharama ya shamba.
wana-kondoo watakupatia mavazi na mbuzi thamani ya shamba.
27 Kutakuwa na maziwa ya mbuzi kwa chakula chako- chakula kwa kaya yako- na chakula kwa watumishi wako wasichana.
Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi kukulisha wewe na jamaa yako, na kuwalisha watumishi wako wa kike.