< Mika 1 >

1 Hili ni neno la Yahwe ambalo lilikuja kwa Mika Mmorashti katika siku za Yotahamu, Ahazi, na Hezekeia, mfalme wa Yuda, lile neno aliloliona kuhusiana na Samaria na Yerusalemu.
Neno la Bwana lilimjia Mika, Mmoreshethi, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu.
2 Sikilizeni, ninyi watu wote. Sikilizeni, dunia, na vyote vilivyomo kwenye dunia. Acheni Yahwe ashuhudiwe dhidi yenu, Bwana kutoka kwenye hekalu lake takatifu.
Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote, sikilizeni, ee dunia na wote mliomo ndani yake, ili Bwana Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu, Bwana kutoka Hekalu lake takatifu.
3 Tazama, Yahwe anakuja kutoka mahali pake; atashuka chini na kupakanyaga mahali pa juu katika dunia.
Tazama! Bwana anakuja kutoka mahali pake; anashuka na kukanyaga mahali palipoinuka juu pa dunia.
4 Milima itayeyuka chini yake; mabonde yatapasuka vipande vipande kama mshumaa mbele ya moto, kama maji ambayo yamemwagika chini ya mteremko mkali.
Milima inayeyuka chini yake na mabonde yanagawanyika kama nta mbele ya moto, kama maji yatiririkayo kasi kwenye mteremko.
5 Haya yote ni kwasababu ya uasi wa Yakobo, na kwasababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. Je sababu ilikuwa nini kwa uasi wa Yakobo? Je ilikuwa Samaria? Je sababu ilikuwa nini kwa mahali pa juu pa Yuda? Je haiukuwa Yerusalemu?
Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo, ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. Kosa la Yakobo ni lipi? Je, sio Samaria? Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini? Je, sio Yerusalemu?
6 “Nitaifanya Samaria rundo la uharibifu katika shamba, kama eneo la kupandia mizabibu. Nitayavuta mawe ya jengo lake kwenda kwenye bonde; Nitaifunua misingi yake.
“Kwa hiyo nitaufanya Samaria kuwa lundo la kokoto, mahali pa kuotesha mizabibu. Nitayamwaga mawe yake katika bonde na kuacha wazi misingi yake.
7 Sanamu zake zote za kuchonga zitapondwa vipande vipande; na zawadi zake zote zitachomwa moto. Kwa kuwa zawadi zake za ukahaba amezikusanya, na kama malipo ya ukahaba yatarudi.”
Sanamu zake zote zitavunjwa vipande vipande; zawadi zake zote za Hekalu zitachomwa kwa moto; nitaharibu vinyago vyake vyote. Kwa kuwa alikusanya zawadi zake kutokana na ujira wa kahaba, nazo zitatumika tena kulipa mishahara ya kahaba.”
8 Kwa sababu hii nitalia na kuomboleza; nitaenda peku peku na uchi; Nitaomboleza kama mbeha na kuomboleza kama bundi.
Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza; nitatembea bila viatu na tena uchi. Nitabweka kama mbweha na kuomboleza kama bundi.
9 Kwa kuwa jeraha lake haliponi, kwa kuwa imefika kwa Yuda. Imefikia lango la watu wangu, hadi Yerusalemu.
Kwa sababu jeraha lake halitibiki; limekuja Yuda. Limefika hasa kwenye lango la watu wangu, hata Yerusalemu kwenyewe.
10 Msiache kuwambia kuhusu katika Gathi; msilie tena. Katika Bethi Leafra nabiringisha mwenyewe kwenye mavumbi.
Usiliseme hili huko Gathi; usilie hata kidogo. Huko Beth-le-Afra gaagaa mavumbini.
11 Piteni karibu na, makao ya Shafiri, katika uchi na aibu. Makazi ya Zaanani hayatatoka nje. Maombolezo ya Beth Ezeli, kwa ajili ya ulinzi yamechukuliwa.
Piteni mkiwa uchi na wenye aibu, ninyi mkaao Shafiri. Wale waishio Saanani hawatatoka nje. Beth-Eseli iko katika maombolezo; kinga yake imeondolewa kwako.
12 Kwa kuwa wakaaji wa Marothi hungoja habari njema, kwa sababu hofu, kwa sababu msiba umetoka kwa Yahwe hadi kwenye malango ya Yerusalemu.
Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu wakingoja msaada, kwa sababu maangamizi yamekuja kutoka kwa Bwana, hata katika lango la Yerusalemu.
13 Wfuungeni lijamu farasi wakokote gari la farasi, makazi ya Lakishi. Wewe Lakishi, ulikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni, kwa kuwa makosa ya Israeli yalionekana kwako.
Enyi mkaao Lakishi, fungeni farasi kwenye magari ya vita. Mlikuwa chanzo cha dhambi kwa Binti Sayuni, kwa kuwa makosa ya Israeli yalikutwa kwako.
14 Hivyo utaipa zawadi ya kuagia Moreshethi Gathi; mji wa Akzibu utawavunja moyo wafalme wa Israeli.
Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi zawadi za kuagana. Mji wa Akzibu utaonyesha wazi udanganyifu kwa wafalme wa Israeli.
15 Tena nitaleta ushindi kwako, makazi ya Maresha; uzuri wa Israeli utakuja Adulamu.
Nitawaleteeni atakayewashinda ninyi mnaoishi Maresha. Yeye aliye utukufu wa Israeli atakuja Adulamu.
16 Kata kipara chako na kata nywele zako kwa ajili ya watoto ambao unaowafurahisha. Fanya kipara chako mwenyewe kama tai, kwa ajili ya watoto wako watakao kwenda utumwani kutoka kwako
Nyoeni nywele zenu katika kuomboleza kwa ajili ya watoto wenu mnaowafurahia; jifanyieni upara kama tai, kwa kuwa watawaacha na kwenda uhamishoni.

< Mika 1 >