< Yona 2 >

1 Kisha Yona akamwomba Bwana Mungu wake kutoka katika tumbo la samaki.
约拿在鱼腹中祷告耶和华—他的 神,
2 Akasema, Nimemwita Bwana juu ya shida yangu naye akanijibu; kutoka tumbo la Kuzimu nililia kwa msaada! Uliisikia sauti yangu. (Sheol h7585)
说: 我遭遇患难求告耶和华, 你就应允我; 从阴间的深处呼求, 你就俯听我的声音。 (Sheol h7585)
3 Ulikuwa umenitupa ndani ya kina, ndani ya moyo wa bahari, na maji yaliyonizunguka; mawimbi yako yote na gharika yalipita juu yangu.
你将我投下深渊, 就是海的深处; 大水环绕我, 你的波浪洪涛都漫过我身。
4 Nikasema, 'Nimefukuzwa mbele ya macho yako; lakini nitaangalia tena juu ya hekalu lako takatifu. '
我说:我从你眼前虽被驱逐, 我仍要仰望你的圣殿。
5 Maji yalifunika kunizunguka karibu na shingo yangu; kina kilinizunguka; mwani ukakizinga kichwa changu.
诸水环绕我,几乎淹没我; 深渊围住我; 海草缠绕我的头。
6 Nilikwenda chini ya milima; nchi na baa zake zimefungwa juu yangu milele. Lakini wewe umeinua uhai wangu shimoni, Bwana, Mungu wangu!
我下到山根, 地的门将我永远关住。 耶和华—我的 神啊, 你却将我的性命从坑中救出来。
7 Wakati nafsi yangu ilipozimia ndani yangu, nikamwita Bwana; basi sala yangu ilikujia, katika hekalu lako takatifu.
我心在我里面发昏的时候, 我就想念耶和华。 我的祷告进入你的圣殿, 达到你的面前。
8 Wote ambao huzingatia miungu isiyofaa hukataa uaminifu wako wao wenyewe.
那信奉虚无之神的人, 离弃怜爱他们的主;
9 Lakini mimi, nitakuchinjia kwa sauti ya shukrani; Nitayatimiza yale niliyoapa. Wokovu hutoka kwa Bwana!
但我必用感谢的声音献祭与你。 我所许的愿,我必偿还。 救恩出于耶和华。
10 Kisha Bwana akanena na samaki, akamtapika Yona juu ya nchi kavu.
耶和华吩咐鱼,鱼就把约拿吐在旱地上。

< Yona 2 >