< Yeremia 50 >
1 Hili ni neno alilolisema Yahwe juu ya Babeli, nchi ya Wakalidayo, kwa mkono wa Yeremia nabii,
Hili ndilo neno alilosema Bwana kupitia nabii Yeremia kuhusu Babeli na nchi ya Wakaldayo:
2 “Wajulishe mataifa ili wasikie. Toa ishara ili wasikie. Usiiache. Sema, 'Babeli imetwaliwa. Beli ameaibika. Merodaki amefadhaika. Sanamu zake zimeaibishwa; vinyago vyake vimefadhaika
“Tangazeni na mhubiri katikati ya mataifa, twekeni bendera na mkahubiri; msiache kitu chochote, bali semeni, ‘Babeli utatekwa; Beli ataaibishwa, Merodaki atajazwa na hofu kuu. Sanamu zake zitaaibishwa na vinyago vyake vitajazwa hofu kuu.’
3 Taifa kutoka kaskazini litainuka kinyume chake, ili kuifanya nchi yake ukiwa. Hakuna hata mmoja, awe mtu au mnyama, atakayeishi ndani yake. Wataondoka.
Taifa kutoka kaskazini litamshambulia, na kuifanya nchi yake ukiwa. Hakuna hata mmoja atakayeishi ndani yake, watu na wanyama wataikimbia.
4 Katika siku hizo na wakati huo - hili ni tamko ya Yahwe - watu wa Israeli na watu wa Yuda watakusanyika ili kwenda kwa kulia na kumtafuta Yahwe Mungu wao.
“Katika siku hizo, wakati huo,” asema Bwana, “watu wa Israeli pamoja na watu wa Yuda wataenda wakilia ili kumtafuta Bwana Mungu wao.
5 Watauliza njia ya kwenda Sayuni nao watakwenda huko, wakisema, tutakwenda wenyewe ili kuungana na Yahwe katika agano la milele lisilosahaulikal
Wataiuliza njia iendayo Sayuni na kuelekeza nyuso zao huko. Watakuja na kuambatana na Bwana katika agano la milele ambalo halitasahaulika.
6 Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea. Wachungaji wao wamewapoteza milimani; wamewageuza kutoka mlima hata mlima. Walikwenda, wakasahau mahali walipokuwa wanaishi.
“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea; wachungaji wao wamewapotosha na kuwasababisha kuzurura juu ya milima. Walitangatanga juu ya mlima na kilima, na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia.
7 Kila awaendeaye anawararua. Washitaki wao walisema, 'Hatuna hatia, kwa sababu walimtenda dhambi Yahwe, nyumbani kwao halisi - Yahwe, tumaini la mababu zao.'
Yeyote aliyewakuta aliwala; adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia, kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya Bwana, malisho yao halisi, Bwana, aliye tumaini la baba zao.’
8 Tokeni kati ya Babeli; tokeni katika nchi ya Wakalidayo; iweni kama wafanyavyo mabeberu mbele ya kundi lote.
“Kimbieni kutoka Babeli; ondokeni katika nchi ya Wakaldayo tena kuweni kama mbuzi wale waongozao kundi.
9 Maana tazama, ninaelekea kupeleka na kuinua kinyume cha Babeli kundi la mataifa makubwa kutoka kaskazini. Yatajipanga yenyewe kinyume chake. Kutoka hapo Babeli utatekwa. Mishale yao ni kama shujaa mzoefu asiyerudi mikono tupu.
Kwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini. Watashika nafasi zao dhidi yake, naye kutokea kaskazini atatekwa. Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari, ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.
10 Ukaldayo itakuwa mateka. Wate waitekao wataridhika - asema Yahwe.
Kwa hiyo Ukaldayo utatekwa nyara; wote wamtekao nyara watapata za kutosha,” asema Bwana.
11 Mnafurahi, mnasherehekea kuteka urithi wangu; mnarukaruka kama ndama anayekanyaga katika malisho yake; mnalia kama farasi mwenye nguvu.
“Kwa sababu hushangilia na kufurahi, wewe utekaye urithi wangu, kwa sababu unachezacheza kama mtamba anayepura nafaka, na kulia kama farasi dume,
12 Hivyo mama yenu ataaibika sana; aliyewazaa atafadhaika. Tazama, atakuwa wa mwisho katika mataifa, nyika, nchi kame, na jangwa.
mama yako ataaibika mno, yeye aliyekuzaa atatahayari. Atakuwa mdogo kuliko mataifa mengine yote, atakuwa nyika, nchi kame na jangwa.
13 Kwa sababu ya hasira ya Yahwe, Babeli haitakaliwa, lakini itakuwa ukiwa mtupu. Kila apitaye kando ataogopa kwa sababu ya Babeli na atatoa sauti kwa sababu ya majeraha yake.
Kwa sababu ya hasira ya Bwana hatakaliwa na mtu, lakini ataachwa ukiwa kabisa. Wote watakaopita Babeli watatiwa hofu na kudhihaki kwa sababu ya majeraha yake yote.
14 Jipangeni wenyewe kumzunguka Babeli kinyume chake. Kila apindaye upinde na ampige. Msizuie mshale wenu wowote, maana amemtenda dhambi Yahwe.
“Shikeni nafasi zenu kuzunguka Babeli, enyi nyote mvutao upinde. Mpigeni! Msibakize mshale wowote, kwa kuwa ametenda dhambi dhidi ya Bwana.
15 Pigeni kelele za ushindi kinyume chake ninyi nyote mmzungukao. Amesalimu mamlaka yake; minara yake imeanguka. Kuta zake zimebomolewa, maana hiki ni kisasi cha Yahwe. Jilipizeni kisasi juu yake! Mtendeeni kama alivyoyatenda mataifa mengine.
Piga kelele dhidi yake kila upande! Anajisalimisha, minara yake inaanguka, kuta zake zimebomoka. Kwa kuwa hiki ni kisasi cha Bwana, mlipizeni kisasi; mtendeeni kama alivyowatendea wengine.
16 Waaribuni wote mkulima apandaye mbegu naye atumiaye mundu wakati wa mavuno katika Babeli. Haya kila mtu na arudi kwa watu wake kutoka upanga wa mtesaji; na wakimbilie katika nchi yao wenyewe.
Katilieni mbali mpanzi kutoka Babeli, pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna. Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe, kila mmoja na akimbilie kwenye nchi yake mwenyewe.
17 Israeli ni kondoo aliyetawanywa na kupelekwa na simba mbali. Kwanza mfalme wa Ashuru alimrarua; kisha baadaye, Nebukadneza mfalme wa Babeli akavunja mifupa yake.
“Israeli ni kundi lililotawanyika ambalo simba wamelifukuzia mbali. Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru, wa mwisho kuponda mifupa yake alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.”
18 Kwa hiyo Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake, kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.
Kwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.
19 Nitamrudisha Israeli katika nchi yake; atajilisha katika Karmeli na Bashani. Kisha atajishibisha katika nchi ya kilima ya Efraimu na Gileadi.
Lakini nitamrudisha Israeli katika malisho yake mwenyewe naye atalisha huko Karmeli na Bashani; njaa yake itashibishwa juu ya vilima vya Efraimu na Gileadi.
20 Siku hizo na wakati huo, asema Yahwe, uovu utatafutwa katika Israeli, lakini hautaonekana. Nitauliza kuhusu dhambi za Yuda, lakini hazitaonekana, maana nitawasamehe mabaki niliowaacha.”
Katika siku hizo, wakati huo,” asema Bwana, “uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli, lakini halitakuwepo, kwa ajili ya dhambi za Yuda, lakini haitapatikana hata moja, kwa kuwa nitawasamehe mabaki nitakaowaacha.
21 Inuka dhidi ya nchi ya Merathaimu, kinyume chake nao waishio Pekodi. Wapigeni kwa makali ya upanga na mwatenge kwa ajili ya maangamizo - asema Yahwe - fanyeni kila ninachowaamru.
“Shambulieni nchi ya Merathaimu na wale waishio huko Pekodi. Wafuatieni, waueni na kuwaangamiza kabisa,” asema Bwana. “Fanyeni kila kitu nilichowaamuru.
22 Sauti ya vita na maangamizi ya kustaajabisha yamo katika nchi.
Kelele ya vita iko ndani ya nchi, kelele ya maangamizi makuu!
23 Jinsi gani nyundo ya mataifa yote imekatiliwa mbali na kuharibiwa. Jinsi Babeli amekuwa kitu cha kushangaza kati ya mataifa.
Tazama jinsi nyundo ya dunia yote ilivyovunjika na kuharibika! Tazama jinsi Babeli ilivyokuwa ukiwa miongoni mwa mataifa!
24 Nimetega mtego dhidi yako. Umenaswa, Babeli, nawe haukutambua! Ulionekana na kukamatwa, tangu uliponidhihaki, Yahwe.
Nimetega mtego kwa ajili yako, ee Babeli, nawe ukakamatwa kabla haujafahamu; ulipatikana na ukakamatwa kwa sababu ulimpinga Bwana.
25 Yahwe amefungua ghala lake la silaha na anachukua silaha kwa ajili ya kutekekeleza hasira yake. Kuna kazi kwa ajili ya Yahwe wa majeshi katika nchi ya Wakaldayo.
Bwana amefungua ghala lake la silaha na kuzitoa silaha za ghadhabu yake, kwa kuwa Bwana Mwenyezi Mwenye Nguvu Zote anayo kazi ya kufanya katika nchi ya Wakaldayo.
26 Mshambulie kutokea mbali. Fungua maghala yake ya chakula na kumrundika kama marundo ya nafaka. Mtenge mbali na maangamizi. Usimbakizie masalia.
Njooni dhidi yake kutoka mbali. Zifungueni ghala zake za nafaka; mlundikeni kama lundo la nafaka. Mwangamizeni kabisa na msimwachie mabaki yoyote.
27 Ua madume wake wote wa ng'ombe. Washushe sehemu ya machinjio. Ole wao, maana siku yao imefika - wakati wa kuadhibiwa kwao.
Waueni mafahali wake wachanga wote; waacheni washuke machinjoni! Ole wao! Kwa kuwa siku yao imewadia, wakati wao wa kuadhibiwa.
28 Kuna sauti ya wale wanaokimbia, walionusurika, katika nchi ya Babeli. Hawa watatoa taarifa ya kisasi cha Yahwe Mungu wetu kwa Sayuni, kisasi kwa hekalu lake.”
Wasikilizeni watoro na wakimbizi kutoka Babeli wakitangaza katika Sayuni jinsi Bwana, Mungu wetu alivyolipiza kisasi, kisasi kwa ajili ya Hekalu lake.
29 Ita wapiga pinde dhidi ya Babeli - wale wote wapindao pinde zao. Piga kambi kinyume chake, na msimwache yeyote kutoroka. Mlipeni kwa kile alichofanya. Mfanyieni kwa kipimo alichotumia. Maana amemdharau Yahwe, Mtakatifu wa Israeli.
“Waiteni wapiga mishale dhidi ya Babeli, wote wale wavutao upinde. Pigeni kambi kumzunguka kabisa, asitoroke mtu yeyote. Mlipizeni kwa matendo yake; mtendeeni kama alivyotenda. Kwa kuwa alimdharau Bwana, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
30 Hivyo vijana wake wataanguka katika viwanja vya mji, na wapiganaji wake wote wataangamizwa siku hiyo - hili ni tamko la Yahwe.”
Kwa hiyo, vijana wake wanaume wataanguka barabarani; askari wake wote watanyamazishwa siku ile,” asema Bwana.
31 Tazama, mimi ni kunyume chako, mwenye majivuno - hili ni tamko la Bwana Yahwe wa majeshi - maana siku yako imefika, mwenye kiburi, wakati nitakapokuadhibu.
“Tazama, niko kinyume nawe, ewe mwenye majivuno,” asema Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, “kwa kuwa siku yako imewadia, yaani, wakati wako wa kuadhibiwa.
32 Hivyo wenye kiburi watajikwaa na kuanguka. Hakuna atakaye wainua. Nitawasha moto katika miji yao; utateketeza kila kitu kati yake.
Mwenye majivuno atajikwaa na kuanguka, wala hakuna yeyote atakayemuinua; nitawasha moto katika miji yake, utakaowateketeza wote wanaomzunguka.”
33 Yahwe wa majeshi asema hivi: watu wa Israeli wamenyanyaswa, pamoja na watu wa Yuda. Wate waliowateka bado wanawashikilia; wanakataa kuwaacha waondoke.
Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote: “Watu wa Israeli wameonewa, nao watu wa Yuda pia. Wote waliowateka wamewashikilia sana, wanakataa kuwaachia waende.
34 Yeye awaokoaye ni mwenye nguvu. Yahwe wa majeshi ni jina lake. Kwa hakika atalitetea shitaka lao, ili kuleta pumziko katika nchi, na kuwapiga wakaao Babeli.
Lakini Mkombozi wao ana nguvu; Bwana Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake. Atatetea kwa nguvu shauri lao ili alete raha katika nchi yao, lakini ataleta msukosuko kwa wale waishio Babeli.
35 Upanga u juu ya Wakalidayo - asema Yahwe - na juu ya wakaao Babeli, viongozi wake, na wenye hekima wake.
“Upanga dhidi ya Wakaldayo!” asema Bwana, “dhidi ya wale waishio Babeli na dhidi ya maafisa wake na watu wenye busara!
36 Upanga unakuja juu ya waganga, ili wajione kuwa wajinga. Upanga utakuwa juu ya askari wake, hivyo watajaa hofu.
Upanga dhidi ya manabii wake wa uongo! Watakuwa wapumbavu. Upanga dhidi ya mashujaa wake! Watajazwa na hofu kuu
37 Upanga utakuwa juu ya farasi wake, vibandawazi vyao na na watu wote waliomo Babeli, hivyo watakuwa kama wanawake. Upanga utakuwa juu ya ghala zake, nazo zitatekwa.
Upanga dhidi ya farasi na magari yake ya vita pamoja na askari wake wote wa kigeni katika safu zake! Wao watakuwa kama wanawake. Upanga dhidi ya hazina zake! Hizo zitatekwa nyara.
38 Ukame unakuja juu ya maji yake, hivyo yatakauka. Maana ni nchi ya miungu wasiofaa, na wanafanya kama watu waliofanywa punguani kwa miungu yao isiyosaidia.
Ukame juu ya maji yake! Nayo yatakauka. Kwa kuwa ni nchi ya sanamu, wao wanaenda wazimu kwa ajili ya sanamu.
39 Hivyo wanyama wa jangwani wakaishi na mbwea wataishi huko, na watoto wa mbuni wataishi ndani yake. Kwa muda wote, hatakaliwa tena. Kutoka kizazi hata kizazi, hatakaliwa tena na watu.
“Kwa hiyo, viumbe vya jangwani na fisi wataishi humo, nao bundi watakaa humo. Kamwe haitakaliwa tena wala watu hawataishi humo kutoka kizazi hadi kizazi.
40 Kama vile Mungu alivyoziangamiza Sodoma na Gomora na majirani zake - asema Yahwe - hakuna atakayeishi huko; hakuna mtu atakayekaa ndani yake.”
Kama vile Mungu alivyoangamiza Sodoma na Gomora pamoja na miji iliyokuwa jirani nayo,” asema Bwana, “vivyo hivyo hakuna mtu yeyote atakayeishi humo. Naam, hakuna mtu yeyote atakayekaa humo.
41 “Tazama, watu wanakuja kutoka kaskazini, maana taifa kubwa na wafalme wengi wamemtikisa kutokea mbali.
“Tazama! Jeshi linakuja kutoka kaskazini; taifa kubwa na wafalme wengi wanaamshwa kutoka miisho ya dunia.
42 Watachukua pinde na mishale. Ni wakatili na hawana huruma. Sauti yao ni kama mngurumo wa bahari, na wamepanda farasi katika mpangilio kama watu wapiganao, dhidi yako, bindi Babeli.
Wamejifunga pinde na mikuki; ni wakatili na wasio na huruma. Wanatoa sauti kama bahari inayonguruma wanapoendesha farasi zao; wanakuja kama watu waliojipanga tayari kwa vita ili kukushambulia, ee Binti Babeli.
43 Mfalme wa Babeli amesikia habari yao na mikono yake imelegea kwa huzuni. Mashaka yamemshika kama mwanamke katika utungu.
Mfalme wa Babeli amesikia habari kuwahusu, nayo mikono yake imelegea. Uchungu umemshika, maumivu kama ya mwanamke katika utungu wa kuzaa.
44 Tazama! Anakwenda juu kama simba atokaye katika miinuko ya Yordani kuelekea katika eneo la malisho ya uvumilivu. Maana kwa haraka nitawafanya wakimbie kutoka humo, nami nitamweka mtu aliyechaguliwa kwa uangalizi wake. Maana ni nani aliye kama mimi, na ni nani atakayeniagiza? Mchungaji gani awezaye kunizuia?
Kama simba anayepanda kutoka vichaka vya Yordani kuja kwenye nchi ya malisho mengi, ndivyo nitamfukuza Babeli kutoka nchi yake ghafula. Ni nani aliye mteule, nitakayemweka kwa ajili ya jambo hili? Ni nani aliye kama mimi, na ni nani awezaye kunipinga? Tena ni mchungaji yupi awezaye kusimama kinyume nami?”
45 Sikilizeni mipango ambayo Yahwe ameamua juu ya Babeli, mipango aliyonayo dhidi ya nchi ya Wakaldayo. Kwa hakika wataondolewa, hata kundi dogo zaidi. Eneo lao la malisho litageuzwa kuwa sehemu zenye magofu.
Kwa hiyo, sikia kile Bwana alichokipanga dhidi ya Babeli, kile alichokusudia dhidi ya nchi ya Wakaldayo: Aliye mchanga katika kundi ataburutwa mbali. Yeye ataharibu kabisa malisho yao kwa sababu yao.
46 Kwa sauti ya kuangushwa kwa Babeli nchi inatikisika, na sauti ya mateso yao inasikiwa kati ya mataifa.”
Kwa sauti ya kutekwa kwa Babeli, dunia itatetemeka; kilio chake kitasikika pote miongoni mwa mataifa.