< Yeremia 49 >

1 Juu ya watu wa Amoni, Yahwe asema hivi, “Je Israeli hana watoto? Je hakuna mtu wa kurithi chochote katika Israeli? Kwa nini Moleki aikalie Gadi, na watu wake kukaa katika miji yake?
關於阿孟子民:上主這樣說:「難道以色列沒有子孫,沒有後嗣﹖為什麼米耳公佔據了加得,而他的人民竟住在加得的城中﹖
2 Hivyo angalia, siku zinakuja - asema Yahwe - nitakapo sikizisha ishara ya vita juu ya Raba miongoni mwa watu wa Amoni, hivyo itakuwa rundo lililoachwa na binti zake watawasha moto. Maana Israeli atawamiliki wanaommiliki,” asema Yahwe.
為此,看,時日將到──上主的斷語──我必使阿孟子民的辣巴聽到戰爭的吶喊;她要成為一堆廢墟,她的附屬城市要為火燒盡;以色列終歸要繼承自己的產業──上主說。
3 Piga kelele kwa maombolezo, Heshboni, maana Ai utaangamizwa! Piga kelele, Binti za Raba! Vaeni nguo za magunia. Ombolezeni na kukimbia kwa kuchanganyikiwa, maana Moleki anakwenda matekani, pamoja na makuhani na viongozi wake.
赫市朋,哀號罷! 因為破壞者已來近了;辣巴的女郎! 你們該哭泣,穿上苦衣哀傷,割傷自己的身體,因為米耳公要與自己的司祭和公卿,同去充軍。
4 Kwa nini mnajivunia nguvu zenu? Nguvu zenu zitakwisha, binti wasioamini, ninyi mnaotumaini utajiri wenu. Mwasema, “Nani atakayekuja kinyume changu?'
失節的女郎! 你為什麼要誇耀你的山谷是富裕的山谷,仗恃你的寶藏說:「有誰敢來與我對抗﹖
5 Tazama, nitaleta kitisho juu yenu - hili ni tamko la Yahwe, Bwana wa majeshi - kitisho hiki kitatoka kwao wote wanaowazunguka. Kila mmoja wenu atatawanyika mbele yake. Hakutakuwa na wa kuwakusanya wanaotawanyika.
看,我從各方給你召來恐怖──我主萬軍上主的斷語──你們必被驅逐,各自奔逃,再沒人來聚集逃散的人。
6 Lakini baada ya haya nitarejesha mema ya watu wa Amoni - hili ni tamko la Yahwe.”
雖然如此,日後我仍要轉變阿孟子民的命運──上主的斷語。」
7 Juu ya Edomu, Yahwe wa majeshi asema hivi, Je hakuna tena hekima katika Temani? Je ushauri mwema umepotea kutoka kwa wenye ufahamu? Je hekima yao imeharibika?
關於厄東,萬軍的上主這樣說:「難道在特曼已沒有智慧,聰敏的人已計窮才盡了嗎﹖
8 Kimbieni! Rudini nyuma! Bakini katika mashimo katika ardhi, wenyeji wa Dedani. Maana naleta maafa ya Esau juu yake wakati ninaomwadhibu.
德丹的居民! 你們該轉身逃遁,藏居深處,因為我要給厄撒烏招來災禍,已到了懲罰他的時候。
9 Ikiwa wavunaji wa zabibu walikuja kwako, je wasinge acha kidogo? Ikiwa wezi walikuja usiku, je wasingeiba kiasi walichotaka?
如果收葡萄的人來到你這裏,決不會留下殘餘;如果盜賊夜間來襲,必要盡力搶取;
10 Lakini nimempiga Esau kwa ukiwa. Nimefunua maficho yao. Hivyo hataweza kujificha mwenyewe. Watoto wake, ndugu zake, na jirani zake wameharibiwa, wamepotea.
我就要這樣暴露厄撒烏,揭發他的隱處,使他無法躲藏;他的後裔,必被消滅,不再存於自己的鄰邦中。
11 Acha nyuma yatima wako. Nitachukua uhai wao, na wajane wako wanaweza kuniamini.”
請留下你的孤兒,我必使他們生存,你的寡婦也可託付給我。
12 Maana Yahwe asema hivi, “Tazama, wasiostahili ni lazima wanywe sehemu ya kikombe. Je mnadhani mtaachwa bila kuhadhibiwa? Hapana, maana hakika mtakunywa.
因為上主這樣說:看,那原來不該飲苦爵的,一定要飲,你要想完全免罰嗎﹖你決不致於免罰,你也該痛飲!
13 Maana nimekwisha apa kwangu mimi mwenyewe - asema Yahwe - Hiyo Bozra itakuwa hofu, aibu, magofu, na kitu cha laana. Miji yake yote itakuwa magofu daima.
因為,我曾指自己起誓──上主的斷語──波責辣必成為一片荒涼,受人憎恨、侮辱和詛咒;她所有的城市,必要永遠變為荒野。
14 Nimesikia habari kutoka kwa Yahwe, na mjumbe ametumwa katika mataifa, 'Kusanyikeni na kumpiga. Jiandaeni kwa vita.'
我從上主聽得了一個消息,在萬民間傳開了一個號令:「你們該聯盟向她進攻! 你們該起來交戰! 」
15 “Maana tazama, nimekufanya kuwa mdogo kulinganisha na mataifa mengine, yenye kudharauliwa na watu.
因為,看,我已使你成為萬民中最小的,成為人間最可輕賤的。
16 Na kwa hofu yenu, kiburi cha moyo wako kimekudanganya, wakaaji wa maeneo ya mwinuko, ninyi mliomiliki vilele vya vilima ili mfanye viota vyenu kama tai. Nitawashusha kutoka huko - asema Yahwe.
你高居在石縫的隱處,盤據在峻嶺的山巔。你自以為驚異,你心卷的驕傲欺騙了你。即使你像老鷹一樣高結你的巢穴,我也要從那裏將你推下──上主的斷語。
17 Edomu atakuwa kitisho kwa kila aipitaye. Kila mtu atatetemeka na kutoa sauti kwa sababu ya maafa yake.
厄東必變成荒野,凡由她那裏經過的人,見了她的種種慘狀,必要唏噓嘆。
18 Kama maangamizi ya Sodoma na Gomora na jirani zake,” asema Yahwe, “hakuna atakayeishi pale; hakuna mtu atakayekaa huko.
她必要像毀滅的索多瑪、哈摩辣及附近的城市一樣──上主說──再沒有人居住,再沒有人在那裏寄宿。
19 Tazama, nitapanda kama simba kutoka katika misitu ya Yordani hata eneo la malisho mabichi. Maana nitaharakisha kumfanya Edomu kumkimbia, nami nitamweka mwingine atakayekuwa amechaguliwa kwa usimamizi huo. Maana ni nani aliyekama mimi, ni nani atakayeniagiza kuja? Mchungaji gani awezaye kunizuia?
看,好像一隻雄獅,從約但的叢林上來,走向常綠的牧場;同樣,我也要突然將他們趕走,派我選定的人民來統治。誠然,誰是我的對手﹖誰敢向我提出質問﹖誰是能對抗我的牧人﹖
20 Hivyo sikiliza mipango ambayo Yahwe ameamua dhidi ya Edom, mipango aliyoifanya kinyume cha wakaao Temani. Bila shaka wataondolewa, hata kundi dogo kuliko yote. Nchi yao yenye malisho yao mabichi itageuzwa kuwa sehemu zenye magofu.
為此,請你們聽上主對厄東設計的計謀,對特曼居民策劃的策略:連最弱小的羊也要被人牽去,他們的牧楊也必陷於戰慄中。
21 Kwa kishindo cha kuanguka kwao nchi hutikisika. Sauti ya milio ya kukata tamaa inasikika katika Bahari ya Shamu.
他們倒塌的響聲,震撼大地;哀號之聲,直達紅海。
22 Tazama, mtu fulani atapiga kama tai, na kushuka chini kwa kasi na kueneza mabawa yake juu ya Bozra. Kisha katika siku hiyo, mioyo ya askari wa Edomu itakuwa kama moyo wa mwanamke katika kuzaa.”
看,他好像老鷹飛升翱翔,在波責辣上展開自己的翅膀;在那一日,厄東的勇士必心志頹喪,有如臨產的婦女。
23 Juu ya Dameski: “Hamathi na Arpadi zitaaibika, maana wamesikia habari ya madhara. Wanayeyuka! Wamesumbuka kama bahari, isiyotulia.
關於大馬士革:哈瑪特和阿爾帕得聽到了不好的消息,大起恐慌,像海洋一樣動盪,愁苦得不能安寧。
24 Dameski umekuwa dhaifu sana. Unageuka kukimbia; hofu imeushika, Maangaiko na maumivu yameupata, kama uchungu wa mwanamke ajifunguaye.
大馬士革失去勇氣,轉身逃遁,極感戰慄,備受憂慮痛苦,好像一臨產的婦女。
25 Watu wake wanasema, “Umekuwaje mji maarufu, mji ambao nimeufurahia, kabla haujaachwa?
哀哉,有的城邑,享樂的都市,已被摒棄!
26 Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika mitaa yake na askari wake wote watateketea siku hiyo - hili ni tamko la Yahwe wa majeshi.”
她的少年將倒斃在廣場,她的戰士在那一日內要悉數滅亡──萬軍上主的斷語──
27 “Maana nitawasha moto katika kuta za Dameski, nami nitazivunja ngome za Beni Hadadi.”
我必在大馬士革城牆上放火,吞滅本哈達得的宮闕。
28 Juu ya Kedari na falme za Hazori, Yahwe amwambia hivi Nebukadneza (Basi Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa akienda kuyashambulia maeneo haya): “Inuka na uipige Kedari na kuwaharibu wale watu wa mashariki.
關於刻達爾和巴比倫王拿步高克服了的哈祚爾諸國,上主這樣說:「起來! 進攻刻達爾,蹂躪東方子民!
29 Jeshi lake litachukua hema zao na makundi yao, nguzo za hema yao, na vitu vyao vyote. Watachukua ngamia wao kutoka kwa watu wa Kedari na kuwambia, 'Hofu ipo pande zote!”
奪取他們的帳幕和牲畜,帷幔和所有的器具;牽走他們的駱駝,向他們吶喊:四面恐怖。
30 Kimbia, Tangatanga mbali! Kaa katika maandaki ardhini, mkaao Hazori - asema Yahwe - maana Nebukadneza mfalme wa Babeli amepanga mpango kinyume chenu. Kimbieni! Geukeni!
哈祚爾的居民! 你們應逃遁遠去,藏匿深處──上主的斷語──因為巴比倫王拿步高已設計謀害你們,已策畫攻擊你們。
31 Simama! lishambulie taifa lililokatika amani, waishio salama,” asema Yahwe. Hawana malango wala nguzo ndani yao, na watu wake wanakaa wenyewe.
起來,進攻優游閒居,不設門閂,孑然獨居的民族──上主的斷語──
32 Maana farasi wao watakuwa mateka, na wingi wa mali zao utakuwa mateka wa vita. Kisha nitawatawanya katika kila upepo wanaonyoa pembe za nywele zao, nami nitaleta madhara juu yao kutoka kila upande - hili ni tamko ya Yahwe.
因為搶奪他們的駱駝,劫掠他們成群的牲畜;凡剃去鬢髮的,我必叫他們隨風飄散,由四面八方給他們招來災禍──上主的斷語──
33 Hazori utakuwa makao ya mbwea, nchi isiyofaa daima. Hakuna atakayeishi huko; hakuna mwanadamu atakayekaa huko.”
哈祚爾要變為豺狼的巢穴,永遠荒涼,留下一人,不會再有人居住。」
34 Hili ni neno la Yahwe lililomwijia Yeremia nabii kuhusu Elamu. Ilikuwa wakati wa mwanzo wa kutawala kwake Sedekia mfalme wa Yuda, naye akasema,
猶大王漆德克雅初年,關於厄藍有上主的話傳給耶肋米亞先知說:「
35 “Yahwe wa majeshi asema hivi: Tazama, ninakaribia kumvunja mpiga upinde wa Elamu, sehemu kuu ya nguvu zao.
萬軍的上主這樣說:看,我要折斷厄藍的弓弩,稱雄的勢力;
36 Maana nitaleta pepo nne kutoka katika pande nne za mbingu, nami nitawatawanya watu wa Elamu katika pepo hizo zote. Hakuta kuwa na taifa ambalo kwalo waliotawanywa kutoka Elamu hawatakwenda.
我要從天下四面八方,給厄藍召來四方的風,使他們隨風飄散,以致沒有一個民族,沒有厄藍的難民。
37 Hivyo nitawavunjavunja Elamu mbele ya adui zao na mbele ya watafutao uhai wao. Maana nitaleta maangamizo dhidi yao, hasira ya gadhabu yangu - hili ni tamko la Yahwe - nami nitapeleka upanga nyuma yao hata nitakapowafuta wote.
我必使厄藍在自己性命的人前,驚惶失措;給他們招來災禍,我忿怒的火焰──上主的斷語──派出刀劍追迫他們,直至將他們完全消滅。
38 Kisha nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu na kumwangamiza mfalme na viongozi wao kutoka huko - asema Yahwe -
我必在厄藍設立我的寶座,殲滅其中的君王將帥──上主的斷語──
39 na itakuwa siku zijazo kwamba nitarejesha mema ya Elamu - asema Yahwe.”
雖然如此,在末日我仍要轉變厄藍的命運──上主的斷語。」

< Yeremia 49 >