< Yeremia 28 >

1 Ilitokea katika mwaka ule, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne na mwezi wa tano, Hanania mwana wa Azuri nabii, alikuwa wa Gibeoni, alisema kwangu katika nyumba ya Yahwe mbele za makuhani na watu wote. Alisema,
Katika mwezi wa tano wa mwaka ule ule, yaani mwaka wa nne, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, nabii Hanania mwana wa Azuri, ambaye alitoka Gibeoni, akaniambia katika nyumba ya Bwana mbele ya makuhani na watu wote:
2 “Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimeivunja nira iliyowekwa na mfalme wa Babeli.
“Hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli asemalo: ‘Nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.
3 Ndani ya miaka miwili nitavirudisha katika sehemu hii vyombo vyote vya nyumba ya Yahwe ambavyo Nebukadreza mfalme wa Babeli livichukua kutoka sehemu hii na kuvisafirisha hadi Babeli.
Katika muda wa miaka miwili nitavirudisha mahali hapa vyombo vyote vya nyumba ya Bwana ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli aliviondoa kutoka hapa na kuvipeleka Babeli.
4 Kisha nitawarudisha katika sehemu hii Yekonia mwana wa Yehotakimu, mfalme wa Yuda, na mateka wote wa Yuda ambao walipelekwa Babeli—hili ni tangazo la Yahwe—kwa maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.”
Pia nitamrudisha mahali hapa Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na wote waliohamishwa kutoka Yuda ambao walikwenda Babeli,’ asema Bwana, ‘kwa kuwa nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.’”
5 Kwa hiyo Yeremia nabii akasema kwa Hanania nabii mbele ya makuhani na kwa watu wote waliosimama katika nyumba ya Yahwe.
Ndipo nabii Yeremia akamjibu nabii Hanania mbele ya makuhani na watu wote waliokuwa wamesimama ndani ya nyumba ya Bwana.
6 Yeremia nabii akasema, “Yahwe afanye hivi! Yahwe ayathibitishe maneno ambayao ulitabiri na kuvirudisha katika sehemsu hii vyombo vya nyumb a ya Yahwe, na mateka wote kutoka Babeli.
Akasema, “Amen! Bwana na afanye hivyo! Bwana na ayatimize maneno uliyotoa unabii kwa kuvirudisha mahali hapa kutoka Babeli vyombo vya nyumba ya Bwana pamoja na wote waliohamishwa.
7 Vile vile, sikilizeni neno ambaloo ninalitangaza katika masikio yenu na katika masikio ya watu wote.
Hata hivyo, nisikilize nikuambie yale nitakayoyasema masikioni mwako na masikioni mwa watu hawa wote:
8 Manabii ambao walikuwepo mbele yangu na na mbele yenu muda mrefu uliopita pia walitabiri kuhusu mataifa mengi na juu ya falme kuu, kuhusu vita, njaa, na mapigo.
Tangu mwanzo, manabii waliokutangulia wewe na mimi walitabiri vita, maafa na tauni dhidi ya nchi nyingi na falme kubwa.
9 Kwa hiyo nabii anayetabiri kwamba kutakuwa na amani—kama neno lake litatimia, basi itajulikana kwamba yeye ni nabii kweli aliyetumwa na Yahwe.”
Lakini nabii atakayetabiri amani atatambuliwa kuwa kweli ametumwa na Bwana ikiwa unabii wake utatimia.”
10 Lakini Hanania nabii akaichukua nira kutoka kwenye shingo ya Yeremia na kuivunja.
Kisha nabii Hanania akaiondoa nira iliyokuwa shingoni mwa Yeremia na kuivunja,
11 Kisha Hanania akanena mbele ya watu wote na kusema, “Yahwe anasema hivi: Kama hivi tu, ndani ya miaka miwili nitaivunja nira iliyowekwa na Nebukadreza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo ya kila taifa.” Kisha Yeremia nabii akaenda njia yake.
naye akasema mbele ya watu wote, “Hili ndilo asemalo Bwana: ‘Vivi hivi ndivyo nitakavyoivunja nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo za mataifa katika muda huu wa miaka miwili.’” Alipofanya hivi, nabii Yeremia akaondoka zake.
12 Baada ya Hanania nabii kuivunja nira kutoka kwenye shingo ya Yeremia nabii, neno la Yahwe likamjia Yeremia. likisema,
Kitambo kidogo baada ya nabii Hanania kuivunja nira kutoka shingo ya nabii Yeremia, neno la Bwana likamjia Yeremia:
13 Nenda na ukaseme kwa Hanania na useme, Yahwe anasema hivi: Uliivunja nira ya mbao, lakini badala yake nitafanya nira ya chuma.'
“Nenda ukamwambie Hanania, ‘Hili ndilo asemalo Bwana: Umevunja nira ya mti, lakini badala yake utapata nira ya chuma.
14 Kwa maana Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimeweka nira ya chuma shingoni mwa mataifa haya yote ili wamtumikea Nebukadreza mfalme wa Babeli, na watamtumikia. Pia nimempa wanyama wa mashambani awatawale.”
Hili ndilo asemalo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli: Nitaweka nira ya chuma kwenye shingo za mataifa haya yote ili kufanya yamtumikie Nebukadneza mfalme wa Babeli, nao watamtumikia. Nitampa kutawala hata wanyama wa mwituni.’”
15 Kisha nabii Yeremia akamwambia Hanania nabii, “Sikiliza Hanania! Yahwe hajakutuma, bali wewe mwenyewe umewasababisha watu hawa kuamini katika uongo.
Kisha nabii Yeremia akamwambia nabii Hanania, “Sikiliza Hanania! Bwana hajakutuma, lakini wewe umelishawishi taifa hili kuamini uongo.
16 Kwa hiyo Yahwe anasema hivi: Angalia, niko karibu kukutuma nje ya dunia. Mwaka huu utakufa.”
Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Bwana: ‘Hivi karibuni nitakuondoa kutoka juu ya uso wa dunia. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi ya Bwana.’”
17 Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, Hanania nabii akafa.
Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, nabii Hanania akafa.

< Yeremia 28 >