< Isaya 61 >

1 Roho ya Bwana Yahwe i juu yangu, maana Yahwe amenipaka mafuta mimi kuhiubiri habari njema kwa wenye taabu. Amenituma mimi kuwaponywa waliopondeka mioyo, kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kufungua gereza ili waliofungwa waweze kutoka.
Roho wa Bwana Mwenyezi yu juu yangu, kwa sababu Bwana amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao;
2 Amenituma mimi kuutangaza mwaka wa Yahwe uliokubalika, siku ya kisasi cha Mungu wetu, na kuwafariji wale wote wanaomboleza.
kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi ya Mungu wetu, kuwafariji wote waombolezao,
3 Amenituma mimi - kuwapa wale waoombolezao katika Sayuni -kuwapa wao kilemba cha majivu, mafuta ya furaha badala ya kuomboleza, vazi la kusifu katika eneo la roho ya ubutu, kuwaita mialoni ya haki, iliyooteshwa na Yahwe, ili aweze kutukuzwa.
na kuwapa mahitaji wale wanaohuzunika katika Sayuni, ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa. Nao wataitwa mialoni ya haki, pando la Bwana, ili kuonyesha utukufu wake.
4 Wataijenga tena mahali pa kale palipohaibiwa; wataparejesha mahali palipokuwa na ukiwa. Watairejesha miji iliyoharibiwa, Mahali penye ukiwa kutoka vizazi vingi vilivyopita.
Watajenga upya magofu ya zamani na kupatengeneza mahali palipoachwa ukiwa zamani; watafanya upya miji iliyoharibiwa, iliyoachwa ukiwa kwa vizazi vingi.
5 Wageni watasimama na kulisha makumdi yako, na watoto wa wageni watafanya kazi kwenye mashamba yako na mizabu.
Wageni watayachunga makundi yenu, wageni watafanya kazi katika mashamba yenu, na kutunza mashamba yenu ya mizabibu.
6 Mtaitwa makuhani wa Yahwe; watawaita watumishi wa Mungu wetu. Mtakula utajiri wa mataifa, na utajivuinia katika utajiri wake.
Nanyi mtaitwa makuhani wa Bwana, mtaitwa watumishi wa Mungu wetu. Mtakula utajiri wa mataifa, nanyi katika utajiri wao mtajisifu.
7 Badala yake aibu yenu itaongezeka; na badala ya fedhea walifurahia juu ya sehemu yao. Hivyo basi sehemu yao itaongezeka mara mbili katika nchi na furaha ya milele itakuwa yao.
Badala ya aibu yao watu wangu watapokea sehemu maradufu, na badala ya fedheha watafurahia katika urithi wao; hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao, nayo furaha ya milele itakuwa yao.
8 Maana Mimi, Yahwe, ninapenda haki, na ninachukia wizi na vurugu zisizo za haki. Nitawalipa wao kataka haki na Nitafanya agano la milele na wao.
“Kwa maana Mimi, Bwana, napenda haki, na ninachukia unyangʼanyi na uovu. Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao na kufanya agano la milele nao.
9 Uzao wao utajulikana miongoni mwa mataifa, na watoto wao miongoni mwa watu. Wote watakaowaona watawakubali wao, kwamba ni watu wangu ambao Yahwe amewabariki.
Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa, na uzao wao miongoni mwa kabila za watu. Wale wote watakaowaona watatambua kuwa ni taifa ambalo Bwana amelibariki.”
10 Nitafurahia sana katika Yahwe; Katika Mungu nitafurahia. Maana amenivika mimi kwa vazi la wokovu; amenivika mimi kwa vazi la haki, kama bwana harusi aliyejipamba mwenywe kwa kilemba, na kama bibi harusi aliyejipamba kwa vito.
Ninafurahia sana katika Bwana, nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu. Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu, na kunipamba kwa joho la haki, kama vile bwana arusi apambavyo kichwa chake kama kuhani, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vito vyake vya thamani.
11 Maana kama nchi inavyozalisha miti inayochipukia na kama bustani inavyofanya miti yake ikuie, hivyo Bwana atasasbabisha haki na sifa kuchipukia mbele ya mataifa yote.
Kwa maana kama vile ardhi ifanyavyo chipukizi kuota, na bustani isababishavyo mbegu kuota, ndivyo Bwana Mwenyezi atafanya haki na sifa zichipuke mbele ya mataifa yote.

< Isaya 61 >