< Kutoka 39 >

1 Na kutokana na ule uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Basi wakafanya yale mavazi matakatifu yaliyokuwa kwa ajili ya Aruni, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
And of the blue, and purple, and scarlet, they made plaited garments, for ministering in the holy place, and made the holy garments for Aaron, as the LORD commanded Moses.
2 Basi akaifanya ile naivera ya dhahabu, uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa.
And he made the ephod of gold, blue, and purple, and scarlet, and fine twined linen.
3 Kisha wakafua mabamba ya dhahabu yawe mabamba membamba, naye akakata nyuzi za kufuma pamoja na ule uzi wa bluu na ile sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kile kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kile kitani bora, kama kazi ya mjenzi.
And they did beat the gold into thin plates, and cut it into threads, to work it in the blue, and in the purple, and in the scarlet, and in the fine linen, the work of the skilful workman.
4 Wakaifanyia vipande vya begani vilivyounganishwa. Iliunganishwa kwenye miisho yake miwili.
They made shoulder-pieces for it, joined together; at the two ends was it joined together.
5 Nao mshipi, uliokuwa juu yake ili kuifunga, ulikuwa wa kitambaa kilekile kulingana na ufundi wake, wa dhahabu, uzi wa bluu, na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
And the skilfully woven band, that was upon it, wherewith to gird it on, was of the same piece and like the work thereof: of gold, of blue, and purple, and scarlet, and fine twined linen, as the LORD commanded Moses.
6 Kisha wakafanya mawe ya shohamu yaliyopangwa kwenye mapambo ya dhahabu, yaliyochongwa kwa michoro ya muhuri kulingana na majina ya wana wa Israeli.
And they wrought the onyx stones, inclosed in settings of gold, graven with the engravings of a signet, according to the names of the children of Israel.
7 Bezaleli akayaweka kwenye vile vipande vya begani vya naivera yawe mawe ya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli, kama vile Yehova alivyokuwa amemwamuru Musa.
And he put them on the shoulder-pieces of the ephod, to be stones of memorial for the children of Israel, as the LORD commanded Moses.
8 Kisha akafanya kile kifuko cha kifuani kwa ufundi wa mjenzi, kama ule ufundi wa naivera, kutokana na dhahabu, uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa.
And he made the breastplate, the work of the skilful workman, like the work of the ephod: of gold, of blue, and purple, and scarlet, and fine twined linen.
9 Kilikuwa mraba kilipokunjwa. Walikifanya kile kifuko cha kifuani, kinapokunjwa, shubiri moja urefu wake na shubiri moja upana wake.
It was four-square; they made the breastplate double; a span was the length thereof, and a span the breadth thereof, being double.
10 Kisha wakakijaza kwa mistari minne ya mawe. Mstari wa zabarijadi, topazi na zumaridi ulikuwa mstari wa kwanza.
And they set in it four rows of stones: a row of carnelian, topaz, and smaragd was the first row.
11 Nao mstari wa pili ulikuwa feruzi, yakuti na yaspi.
And the second row, a carbuncle, a sapphire, and an emerald.
12 Nao mstari wa tatu ulikuwa jiwe la leshemi, akiki na amethisti.
And the third row, a jacinth, an agate, and an amethyst.
13 Nao mstari wa nne ulikuwa krisolito na shohamu na yashefi. Yaliwekwa katika mapambo ya dhahabu katika mahali pake.
And the fourth row, a beryl, an onyx, and a jasper; they were inclosed in fittings of gold in their settings.
14 Na mawe hayo yalikuwa kulingana na majina ya wana wa Israeli. Yalikuwa kumi na mawili kulingana na majina yao, kwa michongo ya muhuri, kila moja kulingana na jina lake kwa ajili ya yale makabila kumi na mawili.
And the stones were according to the names of the children of Israel, twelve, according to their names, like the engravings of a signet, every one according to his name, for the twelve tribes.
15 Nao wakafanya juu ya kile kifuko cha kifuani minyororo yenye mashada, msokoto wa kamba, wa dhahabu safi.
And they made upon the breastplate plaited chains, of wreathen work of pure gold.
16 Kisha wakafanya mapambo mawili ya dhahabu na pete mbili za dhahabu na kuziweka hizo pete mbili kwenye ile miisho miwili ya kile kifuko cha kifuani.
And they made two settings of gold, and two gold rings; and put the two rings on the two ends of the breastplate.
17 Baada ya hilo wakapitisha zile kamba mbili za dhahabu kwenye zile pete mbili zilizo kwenye miisho ya kile kifuko cha kifuani.
And they put the two wreathen chains of gold on the two rings at the ends of the breastplate.
18 Nao wakapitisha ile miisho miwili ya zile kamba mbili kwenye yale mapambo mawili. Halafu wakaiweka juu ya vile vipande vya begani vya naivera, mbele yake.
And the other two ends of the two wreathen chains they put on the two settings, and put them on the shoulder-pieces of the ephod, in the forepart thereof.
19 Kisha wakafanya pete mbili za dhahabu na kuziweka kwenye ile miisho miwili ya kile kifuko cha kifuani kwenye upindo wake ulio upande unaoelekea ile efodi upande wa ndani.
And they made two rings of gold, and put them upon the two ends of the breastplate, upon the edge thereof, which was toward the side of the ephod inward.
20 Halafu wakafanya pete mbili za dhahabu na kuziweka juu ya vile vipande viwili vya begani vya efodi upande wake wa chini, sehemu yake ya mbele, karibu na mahali pake pa kuungania, juu ya ule mshipi wa naivera.
And they made two rings of gold, and put them on the two shoulder-pieces of the ephod underneath, in the forepart thereof, close by the coupling thereof, above the skilfully woven band of the ephod.
21 Mwishowe wakakifunga kile kifuko cha kifuani kwa pete zake kwenye zile pete za efodi kwa uzi wa bluu, ili kipate kuwa juu ya mshipi wa efodi na kile kifuko cha kifuani kisiondoke juu ya efodi, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
And they did bind the breastplate by the rings thereof unto the rings of the ephod with a thread of blue, that it might be upon the skilfully woven band of the ephod, and that the breastplate might not be loosed from the ephod; as the LORD commanded Moses.
22 Bezaleli akafanya lile koti la naivera, lote la uzi wa zambarau, kazi ya mshonaji.
And he made the robe of the ephod of woven work, all of blue;
23 Na sehemu wazi ya hilo koti ilikuwa katikati yake, kama sehemu wazi ya vazi la chuma. Sehemu hiyo iliyo wazi ilikuwa na ukingo kuizunguka pande zote ili isiraruke.
and the hole of the robe in the midst thereof, as the hole of a coat of mail, with a binding round about the hole of it, that it should not be rent.
24 Halafu wakafanya kwenye upindo wa hilo koti makomamanga ya uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili, vilivyosokotwa pamoja.
And they made upon the skirts of the robe pomegranates of blue, and purple, and scarlet, and twined linen.
25 Wakafanya kengele za dhahabu safi na kuziweka kengele hizo katikati ya makomamanga kwenye upindo wa lile koti kuzunguka pande zote, katikati ya makomamanga;
And they made bells of pure gold, and put the bells between the pomegranates upon the skirts of the robe round about, between the pomegranates:
26 kengele na komamanga, kengele na komamanga kwenye upindo wa hilo koti kuzunguka pande zote, kwa ajili ya kuhudumu, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
a bell and a pomegranate, a bell and a pomegranate, upon the skirts of the robe round about, to minister in; as the LORD commanded Moses.
27 Kisha wakafanya zile kamba za kitani bora, kwa ajili ya Haruni na wanawe.
And they made the tunics of fine linen of woven work for Aaron, and for his sons,
28 Na kile kilemba cha kitani bora na yale mavalio ya kichwani ya mapambo ya kitani bora na zile suruali za kitani bora kilichosokotwa,
and the mitre of fine linen, and the goodly head-tires of fine linen, and the linen breeches of fine twined linen,
29 na ule ukumbuu wa kitani bora kilichosokotwa na uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili, kazi ya mfumaji, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
and the girdle of fine twined linen, and blue, and purple, and scarlet, the work of the weaver in colours; as the LORD commanded Moses.
30 Mwishowe wakafanya lile bamba linalong’aa, ishara takatifu ya wakfu, kutokana na dhahabu safi na kuandika juu yake maandishi kwa mchongo wa muhuri: “Utakatifu kwa Yahweh.”
And they made the plate of the holy crown of pure gold, and wrote upon it a writing, like the engravings of a signet: HOLY TO THE LORD.
31 Kisha wakalitia uzi wa bluu ili waliweke juu ya kile kilemba upande wa juu. Kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.
And they tied unto it a thread of blue, to fasten it upon the mitre above; as the LORD commanded Moses.
32 Basi kazi ya ile maskani ya hema la mkutano ikafikia mwisho wake. Kwa maana wana wa Israeli waliendelea kufanya kulingana na yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa.
Thus was finished all the work of the tabernacle of the tent of meeting; and the children of Israel did according to all that the LORD commanded Moses, so did they.
33 Nao wakaileta maskani kwa Musa, lile hema pamoja na vyombo vyake vyote, kulabu zake, viunzi vyake vya mbao, miti yake na nguzo zake na vikalio vyake,
And they brought the tabernacle unto Moses, the Tent, and all its furniture, its clasps, its boards, its bars, and its pillars, and its sockets;
34 na kifuniko chake cha ngozi za kondoo-dume zilizotiwa rangi nyekundu na kifuniko chake cha ngozi za sili na pazia la kisitiri,
and the covering of rams' skins dyed red, and the covering of sealskins, and the veil of the screen;
35 na sanduku la ushuhuda na miti yake na kifuniko.
the ark of the testimony, and the staves thereof, and the ark-cover;
36 Wakaleta meza, vyombo vyake vyote, na ule mkate wa wonyesho,
the table, all the vessels thereof, and the showbread;
37 kile kinara cha taa cha dhahabu safi, taa zake, ule mstari wa taa, na vyombo vyake vyote na yale mafuta ya kuangazia taa,
the pure candlestick, the lamps thereof, even the lamps to be set in order, and all the vessels thereof, and the oil for the light;
38 na madhabahu ya dhahabu na yale mafuta yanayotumiwa kutia mafuta na ule uvumba uliotiwa manukato na kile kisitiri kwa ajili ya mwingilio wa hema,
and the golden altar, and the anointing oil, and the sweet incense, and the screen for the door of the Tent;
39 ile madhabahu ya shaba na kile kiunzi chake cha shaba, miti yake na vyombo vyake vyote, ile beseni na kinara chake,
the brazen altar, and its grating of brass, its staves, and all its vessels, the laver and its base;
40 Wakaleta mapazia ya ua, nguzo zake na vikalio vyake na kile kisitiri kwa ajili ya lango la ua, kamba zake za hema na misumari yake ya hema na vyombo vyote kwa ajili ya utumishi wa maskani, kwa ajili ya hema ya kukutania.
the hangings of the court, its pillars, and its sockets, and the screen for the gate of the court, the cords thereof, and the pins thereof, and all the instruments of the service of the tabernacle of the tent of meeting;
41 Wakaleta yale mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika patakatifu, yale mavazi matakatifu kwa ajili ya Aruni kuhani na mavazi ya wanawe ya kutumikia wakiwa makuhani.
the plaited garments for ministering in the holy place; the holy garments for Aaron the priest, and the garments of his sons, to minister in the priest's office.
42 Kulingana na yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa, hivyo ndivyo wana wa Israeli walivyoufanya utumishi wote.
According to all that the LORD commanded Moses, so the children of Israel did all the work.
43 Naye Musa akaiona ile kazi yote, na, tazama, walikuwa wameifanya kama vile Yahweh alivyokuwa ameamuru. Hivyo ndivyo walivyokuwa wamefanya. Basi Musa akawabariki.
And Moses saw all the work, and, behold, they had done it; as the LORD had commanded, even so had they done it. And Moses blessed them.

< Kutoka 39 >