< Amosi 9 >
1 Nilimwona Bwana amesimama karibu na madhabahu, na akasema, “Vipige vichwa vya nguzo ili kwamba misingi itikisike. Vivunje vipande vipande juu ya vichwa vyao vyote, nami nitamwua kwa upanga wa mwisho wao. Hakuna hata mmoja wao atakaye kimbia, hakuna hata mmoja wao atakayekimbia.
Nilimwona Bwana akiwa amesimama kando ya madhabahu, naye akasema: “Piga vichwa vya nguzo ili vizingiti vitikisike. Viangushe juu ya vichwa vya watu wote; na wale watakaosalia nitawaua kwa upanga. Hakuna awaye yote atakayekimbia, hakuna atakayetoroka.
2 Hata kama watachimba kwenye Sheoli, kuna mkono wangu utawachukua. Hata kama watapanda juu kwenda mbingunu, huko nitawaleta chini. (Sheol )
Wajapojichimbia chini mpaka kwenye vina vya kuzimu, kutoka huko mkono wangu utawatoa. Wajapopanda juu hadi kwenye mbingu, kutoka huko nitawashusha. (Sheol )
3 Hata kama watajificha juu ya Karmeli, nitawatafuta huko na kuwachukua. Hata kama watajificha kwenye vilindi vya bahari nisiwaone, nimwagiza joka, na atawang'ata.
Wajapojificha juu ya kilele cha Karmeli, huko nitawawinda na kuwakamata. Wajapojificha kutoka kwenye uso wangu katika vilindi vya bahari, huko nako nitaamuru joka kuwauma.
4 Hata kama wataenda kwenye utumwa, watabanwa na maadui zao mbele yao, nitauagiza upanga huko, na utawau. Nitaelekeza macho yangu juu yao kwa ubaya sio kwa uzuri.”
Wajapopelekwa uhamishoni na adui zao, huko nako nitaamuru upanga uwaue. Nitawakazia macho yangu kwa mabaya wala si kwa mazuri.”
5 Bwana Mungu wa majeshi ndiye agusaye nchi na ikayeyuka; wote waishio humo wataomboleza; yote yatainuka kama Mto, na itadidimia tena kama mto wa Misri.
Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, yeye agusaye dunia nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani mwake wakaomboleza: nayo nchi yote huinuka kama Naili, kisha hushuka kama mto wa Misri;
6 Ni yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuanzisha kuba yake juu ya dunia. Yeye huita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa dunia, Yahwe ndiye jina lake.
yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu na kuisimika misingi yake juu ya dunia, yeye aitaye maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi: Bwana ndilo jina lake.
7 “Je ninyi sio kama watu wa Kushi kwangu, wana wa Israeli? -hivi ndivyo Yahwe asemavyo. Je sikuwapandisha Israeli kutoka nchi ya misri, Wafilisti kutoka Krete, na Washami kutoka Kiri?
“Je, Waisraeli, ninyi si sawa kwangu kama Wakushi?” asema Bwana. “Je, sikuleta Israeli kutoka Misri, Wafilisti kutoka Kaftori, na Washamu kutoka Kiri?
8 Tazama, macho ya Bwana Yahwe yako juu ya ufalme wenye dhambi, na nitauharibu kutoka kwenye uso wa dunia, isipokuwa kwamba sintoiharibu kabisa nyumba ya Yakobo -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
“Hakika macho ya Bwana Mwenyezi yako juu ya ufalme wenye dhambi. Nami nitauangamiza kutoka kwenye uso wa dunia: hata hivyo sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo,” asema Bwana.
9 Tazama, nitaamuru, na nitaipepeta nyumba ya Israeli miongoni mwa mataifa yote, kama mtu apepetaye ngano kwenye ungo, hivyo basi hakuna hata chembe ya jiwe itakayoanguka kwenye aridhi.
“Kwa kuwa nitatoa amri, na nitaipepeta nyumba ya Israeli miongoni mwa mataifa yote, kama vile nafaka ipepetwavyo katika ungo, na hakuna hata punje moja itakayoanguka chini.
10 Watenda dhambi wote katika watu wangu watakufa kwa upanga, wale wasemao, 'Majanga hayatatupita au kukutana nasi.'
Watenda dhambi wote miongoni mwa watu wangu watauawa kwa upanga, wale wote wasemao, ‘Maafa hayatatupata wala kutukuta.’
11 Katika siku hiyo nitainua hema ya Daudi iliyokuwa imeanguka, na kuyafunga matawi yake. Nitayainua magofu yake, na kuijenga tena kama katika siku za zamani,
“Katika siku ile nitaisimamisha hema ya Daudi iliyoanguka. Nitakarabati mahali palipobomoka na kujenga upya magofu yake, na kuijenga kama ilivyokuwa awali,
12 Kwamba wamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote ambayo yameitwa kwa jina langu -hivi ndivyo Yahwe asemavyo-afanyayo haya.
ili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote yale yanayobeba Jina langu,” asema Bwana ambaye atafanya mambo haya.
13 Tazama, siku zitakuja-hivi ndivyo Yahwe asemavyo-wakati mlimaji atampita mvunaji, na akanyagaye zabibu atampita yeye apandaye mbegu. Milima itadondosha divai tamu, na milima yote itabubujika kwa nayo.
“Siku zinakuja,” asema Bwana, “wakati mvunaji atatanguliwa na mkulima, naye mpanzi atatanguliwa na yeye akamuaye zabibu. Divai mpya itadondoka kutoka milimani, na kutiririka kutoka vilima vyote.
14 Nitawarudisha kutoka utumwani watu wangu Israeli. Watajenga magofu ya miji na kuishi humo, watapanda bustani za mizabibu na kunywa divai, na watafanya bustani na kula matunda yao.
Nitawarejesha tena watu wangu Israeli waliohamishwa; wataijenga tena miji iliyoachwa magofu, nao wataishi ndani mwake. Watapanda mizabibu na kunywa divai yake; watalima bustani na kula matunda yake.
15 Nitaipanda hadi kwenye nchi yao, na hawataing'oa tena kutoka kwenye nchi ambayo niliyowapatia,” asema Yahwe Mungu wako.
Nitaipanda Israeli katika nchi yao wenyewe, hawatangʼolewa tena kutoka nchi ambayo nimewapa,” asema Bwana Mungu wenu.