< 2 Petro 2 >
1 Manabii wa uongo walijitokeza kwa Waisraeli, na walimu wa uongo watakuja pia kwenu. Kwa siri wataleta mafundisho ya uongo nao watamkana Bwana aliyewanunua. Wanajiletea uharibifu wa haraka juu yao wenyewe.
2 Wengi watafuata njia zao za aibu na kupitia wao wataikufuru njia ya ukweli.
3 Kwa uchoyo watawanyonya watu wakitumia maneno ya uongo Hukumu yao haitachelewa, uharibifu utawafuata.
4 Maana Mungu hakuwaacha malaika waliokengeuka. Bali aliwatupa kuzimu ili wafungwe minyororo mpaka hukumu itakapowajilia. (Tartaroō )
5 Wala Mungu hakuuvumilia ulimwengu wa zamani. Bali, alimhifadhi Nuhu, mwenye wito wa haki, pamoja na wengine saba, wakati alipoachila gharika juu ya ulimwengu ulioasi.
6 Mungu aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kiasi cha kuwa majivu na uharibifu ili iwe mfano kwa ajili ya waovu katika siku za usoni
7 Lakini alipofanya hilo, alimwokoa Lutu mtu wa haki, aliyekuwa amehuzunishwa na tabia chafu za wasiofuata sheria za Mungu.
8 Kwa kuwa huyo mtu wa haki, aliyeishi nao siku kwa siku akiitesa nafsi yake kwa ajili ya yale aliyoyasikia na kuyaona.
9 Kwa hiyo Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa watu wake wakati wa mateso na jinsi ya kuwavumilia waovu kwa ajili ya hukumu katika siku ya mwisho.
10 Kwa hakika huu ndio ukweli kwa wale wanoendelea kuishi katika tamaa za mwili huu na kuyadharau mamlaka. Watu wa jinsi hii wana ujasiri katika dhamiri zao, Hawaogopi kuwakufuru watukufu.
11 Ingawa malaika wana uwezo na nguvu kuliko wanadamu, lakini hawawezi kuleta hukumu dhidi yao kwa Bwana
12 Lakini hawa wanyama wasio na akili wametengenezwa kwa asili ya kukamatwa na kuangamizwa.
13 Wanaumizwa kwa ujira wa maovu yao. Mchana kutwa huishi kwa anasa. Wamejaa uchafu na maovu. Hufurahia anasa za udanganyifu wanaposherehekea na wewe.
14 Macho yao yamefunikwa na uzinzi; hawatosheki kutenda dhambi. Huwalaghai na kuwaangusha waumini wachanga katika dhambi. Wana mioyo iliyojaa tamaa, ni watoto waliolaaniwa.
15 Wameiacha njia ya kweli. wamepotoka na wameifuata njia ya Balaam mwana wa Beori, aliyependa kupata malipo ya udhalimu.
16 Lakini alikemewa kwa ajili ya ukosai wake. Punda aliyekuwa bubu akiongea katika sauti ya binadamu, alizuia wazimu wa nabii.
17 Watu hawa ni kama chemichemi zisizo na maji. Ni kama mawingu yanayotoweshwa na upepo. Wingu zito limehifadhiwa kwa ajili yao.
18 Huongea kwa majivuno matupu. Huwaangusha watu kwa tamaa ya mwili. Huwalaghai watu wanaojaribu kuwakimbia wale waishio katika ukosaji.
19 Huwaahidi watu uhuru wakati wao wenyewe ni watumwa wa dhambi ya ufisadi. Maana mwanadamu hufanywa kuwa mtumwa wa kile kinachomtawala.
20 Yeye ajiepushaye na uchafu wa ulimwengu kwa kutumia maarifa ya Bwana na mwokozi Yesu Kristo, na kisha akarudia uchafu huo tena, hali yake huwa mbaya kuliko ile ya mwanzo.
21 Ingefaa watu hao kama wasingeifahamu njia ya haki kuliko kuifahamu na kisha tena kuziacha amri takatifu walizopewa.
22 Mithali hii huwa na ukweli kwao. “mbwa huyarudia matapishi yake. Na nguruwe aliyeoshwa hurudi tena kwenye matope.”