< 1 Wakorintho 1 >

1 Paulo, aliyeitwa na Kristo Yesu kuwa mtume kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,
Paul, called to be an apostle of Jesus Christ through the will of God, and Sosthenes our brother,
2 kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale ambao wamewekwa wakfu katika Yesu Kristo, ambao wameitwa kuwa watu watakatifu. Tunawaandikia pia wale wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo katika mahali pote, Bwana wao na wetu.
Unto the Assembly of God which is at Corinth, to them that are sanctified in Christ Jesus, called to be saints, with all that in every place call upon the name of Jesus Christ our Lord, both theirs and ours:
3 Neema na amani iwe kwenu kutoka kwa Mungu baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.
Grace be unto you, and peace, from God our Father, and from the Lord Jesus Christ.
4 Siku zote namshukru Mungu wangu kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu ambayo Kristo Yesu aliwapa.
I thank my God always on your behalf, for the grace of God which is given you by Jesus Christ;
5 Amewafanya kuwa matajiri katika kila njia, katika usemi na pamoja maarifa yote.
That in every thing ye are enriched by him, in all utterance, and in all knowledge;
6 Amewafanya matajiri, kama ushuhuda kuhusu Kristo ya kwamba amethibitishwa kuwa kweli miongoni mwenu.
Even as the testimony of Christ was confirmed in you:
7 Kwa hiyo hampungukiwi karama za kiroho, kama mlivyo na hamu ya kusubiri ufunuo wa Bwana wetu Yesu Kristo.
So that ye come behind in no gift; waiting for the coming of our Lord Jesus Christ:
8 Atawaimarisha ninyi pia hadi mwisho, ili msilaumiwe siku ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Who shall also confirm you unto the end, that ye may be blameless in the day of our Lord Jesus Christ.
9 Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita ninyi katika ushirika wa mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu.
God is faithful, by whom ye were called unto the fellowship of his Son Jesus Christ our Lord.
10 Sasa nawasihi kaka na dada zangu, kupitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba wote mkubali, na kwamba kusiwe na migawanyiko miongoni mwenu. Nawasihi kwamba muungane pamoja katika nia moja na katika kusudi moja.
Now I beseech you, brethren, by the name of our Lord Jesus Christ, that ye all speak the same thing, and that there be no divisions among you; but that ye be perfectly joined together in the same mind and in the same judgment.
11 Kwani watu wa nyumba ya Kloe wamenitaarifu kuwa kuna mgawanyiko unaoendelea miongoni mwenu.
For it hath been declared unto me of you, my brethren, by them which are of the house of Chloe, that there are contentions among you.
12 Nina maana hii: Kila mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo,” au “Mimi ni wa Apolo”, au “Mimi ni wa Kefa” au “Mimi ni wa Kristo”.
Now this I say, that every one of you saith, I am of Paul; and I of Apollos; and I of Cephas; and I of Christ.
13 Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?
Is Christ divided? was Paul crucified for you? or were ye baptized in the name of Paul?
14 Namshukuru Mungu kuwa sikumbatiza yeyote, isipokuwa Krispo na Gayo.
I thank God that I baptized none of you, but Crispus and Gaius;
15 Hii ilikuwa kwamba hakuna yeyote angesema mlibatizwa kwa jina langu.
Lest any should say that I had baptized in mine own name.
16 (Pia niliwabatiza wa nyumba ya Stephania. Zaidi ya hapo, sijui kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote).
And I baptized also the household of Stephanas: besides, I know not whether I baptized any other.
17 Kwa kuwa, Kristo hakunituma kubatiza bali kuhubiri injili. Hakunituma kuhubiri kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili kwamba nguvu ya msalaba wa Kristo isiondolewe.
For Christ sent me not to baptize, but to preach the gospel: not with wisdom of words, lest the cross of Christ should be made of none effect.
18 Kwa kuwa ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa wale wanaokufa. Lakini kwa wale ambao Mungu anawaokoa, ni nguvu ya Mungu.
For the preaching of the cross is to them that perish foolishness; but unto us which are saved it is the power of God.
19 Kwa kuwa imeandikwa, “Nitaiharibu hekima ya wenye busara. Nitauharibu ufahamu wa wenye akili.”
For it is written, I will destroy the wisdom of the wise, and will bring to nothing the understanding of the prudent.
20 Yuko wapi mtu mwenye busara? Yuko wapi mwenye elimu? Yuko wapi msemaji mshawishi wa dunia hii? Je, Mungu hakuigeuza hekima ya dunia hii kuwa ujinga? (aiōn g165)
Where is the wise? where is the scribe? where is the disputer of this world? hath not God made foolish the wisdom of this world? (aiōn g165)
21 Tangu dunia imekuwa katika hekima yake haikumjua Mungu, ilimpendeza Mungu katika ujinga wao wa kuhubiri ili kuokoa wale wanaoamini.
For after that in the wisdom of God the world by wisdom knew not God, it pleased God by the foolishness of preaching to save them that believe.
22 Kwa Wayahudi huuliza ishara za miujiza na kwa Wayunani hutafuta hekima.
For the Jews require a sign, and the Greeks seek after wisdom:
23 Lakini tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa, aliye kikwazo kwa Wayahudi na ni ujinga kwa Wayunani.
But we preach Christ crucified, unto the Jews a stumblingblock, and unto the Greeks foolishness;
24 Lakini kwa wale ambao waliitwa na Mungu, Wayahudi na Wayunani, tunamhubiri Kristo kama nguvu na hekima ya Mungu.
But unto them which are called, both Jews and Greeks, Christ the power of God, and the wisdom of God.
25 Kwa kuwa ujinga wa Mungu una hekima kuliko ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.
Because the foolishness of God is wiser than men; and the weakness of God is stronger than men.
26 Angalia wito wa Mungu juu yenu, kaka na dada zangu. Si wengi wenu mlikuwa na hekima katika viwango vya kibinadamu. Si wengi wenu mlikuwa na nguvu. Si wengi wenu mlizaliwa katika ukuu.
For ye see your calling, brethren, how that not many wise men after the flesh, not many mighty, not many noble, are called:
27 Lakini Mungu alichagua vitu vijinga vya dunia ili kuviaibisha vyenye hekima. Mungu alichagua kilicho dhaifu katika dunia kukiaibisha chenye nguvu.
But God hath chosen the foolish things of the world to confound the wise; and God hath chosen the weak things of the world to confound the things which are mighty;
28 Mungu alichagua kile kilicho cha hali ya chini na kilichodharauliwa katika dunia. Alichagua hata vitu ambavyo havikuhesabiwa kuwa kitu, kwa kuvifanya si kitu vitu vilivyo na thamani.
And base things of the world, and things which are despised, hath God chosen, yea, and things which are not, to bring to nought things that are:
29 Alifanya hivi ili asiwepo yeyote aliye na sababu ya kujivuna mbele zake.
That no flesh should glory in his presence.
30 Kwa sababu ya kile Mungu alichofanya, sasa mko ndani ya Kristo Yesu, ambaye amefanyika hekima kwa ajili yetu kutoka kwa Mungu. Alikuwa haki yetu, utakatifu na ukombozi.
But of him are ye in Christ Jesus, who of God is made unto us wisdom, and righteousness, and sanctification, and redemption:
31 Kama matokeo, kama andiko lisemavyo, “Anayejisifu, ajisifu katika Bwana.”
That, according as it is written, He that glorieth, let him glory in the Lord.

< 1 Wakorintho 1 >