< 1 Nyakati 3 >

1 Sasa hawa ndio wana wa Daudi waliozaliwa kwake huko Hebroni: mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu kutoka Yezreeli; wa pili alikuwa Danieli, kwa Abigaili kutoka Karmeli;
David vero hos habuit filios qui ei nati sunt in Hebron primogenitum Amnon ex Achinaam Iezrahelitide secundum Danihel de Abigail Carmelitide
2 watatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa ni Maaka, binti wa Talmai mfalme wa Geshuri. Wanne alikuwa ni Adoniya mwana wa Hagithi;
tertium Absalom filium Maacha filiae Tholmei regis Gessur quartum Adoniam filium Aggith
3 watano alikuwa ni Shefatia kwa Abitali, wasita alikuwa ni Ithraeamu kwa Egla mkewe.
quintum Saphatiam ex Abital sextum Iethraam de Egla uxore sua
4 Hawa sita walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni, alipo tawala miaka saba na miezi sita. Kisha akatawala miaka thelathini na mitatu huko Yerusalemu.
sex ergo nati sunt ei in Hebron ubi regnavit septem annis et sex mensibus triginta autem et tribus annis regnavit in Hierusalem
5 Hawa wana wa nne, kwa Bathshua binti wa Amieli, walizaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Nathani, na Sulemani.
porro in Hierusalem nati sunt ei filii Samaa et Sobab et Nathan et Salomon quattuor de Bethsabee filia Amihel
6 Wana tisa wengine wa Daudi walikuwa ni: Ibhari, Elishua, Elipeleti,
Iebaar quoque et Elisama
7 Noga, Nefegi, Yafia,
et Eliphalet et Noge et Napheg et Iaphie
8 Elishama, na Elifeleti.
necnon Elisama et Heliade et Eliphalet novem
9 Hawa walikuwa wana wa Daudi, pasipo kuwehesababu wana wa masuria wake. Tamari alikuwa dada yao.
omnes hii filii David absque filiis concubinarum habuerunt sororem Thamar
10 Mwana wa Sulemani alikuwa ni Rehoboamu. Mwana wa Rehoboamu alikuwa Abiya. Mwana wa Abiya alikuwa Asa. Mwana wa Asa alikuwa Yehoshafati.
filius autem Salomonis Roboam cuius Abia filius genuit Asa de hoc quoque natus est Iosaphat
11 Mwana wa Yehoshafati alikuwa Yoramu. Mwana wa Yoramu alikuwa Ahazia. Mwana wa Ahazia alikuwa Yoashi.
pater Ioram qui Ioram genuit Ohoziam ex quo ortus est Ioas
12 Mwana wa Yoashi alikuwa Amazia. Mwana wa Amazia alikuwa Azaria. Mwana wa Azaria alikuwa Yothamu.
et huius Amasias filius genuit Azariam porro Azariae filius Ioatham
13 Mwana wa Yothamu alikuwa Ahazi. Mwana wa Ahazi alikuwa Hezekia. Mwana wa Hezekia alikuwa Manase.
procreavit Achaz patrem Ezechiae de quo natus est Manasses
14 Mwana wa Manase alikuwa Amoni. Mwana wa Amoni alikuwa Yosia.
sed et Manasses genuit Amon patrem Iosiae
15 Wana wa Yosia aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza ni Yohana, wapili Yehoyakimu, mwanae watatu Sedekia, na mwanae wanne Shalumu.
filii autem Iosiae fuerunt primogenitus Iohanan secundus Ioacim tertius Sedecias quartus Sellum
16 Wana wa Yehoyakimu walikuwa Yehoyakini na Sedekia.
de Ioacim natus est Iechonias et Sedecias
17 Wana wa YehoYakini, mateka, walikuwa Shealtieli,
filii Iechoniae fuerunt Asir Salathihel
18 Malkiramu, Pedaya, Shenezari, Yekamia, Hoshama, na Nedabia.
Melchiram Phadaia Sennaser et Iecemia Sama et Nadabia
19 Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Wana wa Zerubabeli walikuwa Meshulamu na Hanania; Shelomithi alikuwa dada yao.
de Phadaia orti sunt Zorobabel et Semei Zorobabel genuit Mosollam Ananiam et Salomith sororem eorum
20 Wanae watano walikuwa Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia, na Yushabu Hesedi.
Asabamque et Ohol et Barachiam et Asadiam Iosabesed quinque
21 Wana wa Hanania walikuwa Pelatia na Yeshaya. Mwanawe alikuwa Refaya, na uzao wake zaidi walikuwa ni Arnani, Obadia, na Shekania.
filius autem Ananiae Phaltias pater Ieseiae cuius filius Raphaia huius quoque filius Arnam de quo natus est Obdia cuius filius fuit Sechenia
22 Mwana wa Shekania alikuwa Shemaya. Wana wa Shemaya walikuwa Hatushi, Igali, Baria, Nearia, na Shafati.
filius Secheniae Semeia cuius filii Attus et Iegal et Baria et Naaria et Saphat sex numero
23 Wana watatu wa Nearia walikuwa Elioenai, Hizekia, na Azrikamu.
filius Naariae Helioenai et Ezechias et Ezricam tres
24 Wana saba wa Elioenai walikuwa Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohana, Delaya, na Anani.
filii Helioenai Oduia et Heliasub et Pheleia et Accub et Iohanan et Dalaia et Anani septem

< 1 Nyakati 3 >