< Zaburi 134 >

1 Wimbo wa kwenda juu. Msifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana, ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana. 2 Inueni mikono yenu katika pale patakatifu na kumsifu Bwana. 3 Naye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia, awabariki kutoka Sayuni.

< Zaburi 134 >