< Waamuzi 5 >

1 Ndipo Debora na Baraka mwana wa Abinoamu wakaimba wimbo huu:
ותשר דבורה וברק בן אבינעם ביום ההוא לאמר
2 “Wakuu katika Israeli wanapoongoza, wakati watu wanapojitoa kwa hiari yao wenyewe: mhimidini Bwana!
בפרע פרעות בישראל בהתנדב עם ברכו יהוה
3 “Sikieni hili, enyi wafalme! Sikilizeni, enyi watawala! Nitamwimbia Bwana, nitaimba; kwa wimbo nitamhimidi Bwana, Mungu wa Israeli.
שמעו מלכים האזינו רזנים אנכי ליהוה אנכי אשירה אזמר ליהוה אלהי ישראל
4 “Ee Bwana, ulipotoka katika Seiri, ulipopita katika mashamba ya Edomu, nchi ilitetemeka, mbingu nazo zikamwaga, naam, mawingu yakamwaga maji.
יהוה בצאתך משעיר בצעדך משדה אדום ארץ רעשה גם שמים נטפו גם עבים נטפו מים
5 Milima ilitetemeka mbele za Bwana, hata ule wa Sinai, mbele za Bwana, Mungu wa Israeli.
הרים נזלו מפני יהוה זה סיני--מפני יהוה אלהי ישראל
6 “Katika siku za Shamgari mwana wa Anathi, katika siku za Yaeli, barabara kuu hazikuwa na watu; wasafiri walipita njia za kando.
בימי שמגר בן ענת בימי יעל חדלו ארחות והלכי נתיבות--ילכו ארחות עקלקלות
7 Mashujaa walikoma katika Israeli, walikoma mpaka mimi, Debora, nilipoinuka, nilipoinuka kama mama katika Israeli.
חדלו פרזון בישראל חדלו-- עד שקמתי דבורה שקמתי אם בישראל
8 Walipochagua miungu migeni, vita vilikuja katika malango ya mji, hapakuonekana ngao wala mkuki miongoni mwa mashujaa 40,000 katika Israeli.
יבחר אלהים חדשים אז לחם שערים מגן אם יראה ורמח בארבעים אלף בישראל
9 Moyo wangu u pamoja na wakuu wa Israeli, pamoja na wale wanaojitoa wenyewe kwa hiari yao miongoni mwa watu. Mhimidini Bwana!
לבי לחוקקי ישראל המתנדבים בעם ברכו יהוה
10 “Nanyi mpandao punda weupe, mkiketi juu ya matandiko ya thamani, nanyi mtembeao barabarani, fikirini
רכבי אתנות צחרות ישבי על מדין והלכי על דרך--שיחו
11 juu ya sauti za waimbaji mahali pa kunyweshea maji. Wanasimulia matendo ya haki ya Bwana, matendo ya haki ya mashujaa wake katika Israeli. “Ndipo watu wa Bwana walipoteremka malangoni pa mji.
מקול מחצצים בין משאבים שם יתנו צדקות יהוה צדקת פרזונו בישראל אז ירדו לשערים עם יהוה
12 ‘Amka, amka! Debora! Amka, amka, uimbe! Ee Baraka! Inuka, chukua mateka wako uliowateka, ee mwana wa Abinoamu.’
עורי עורי דבורה עורי עורי דברי שיר קום ברק ושבה שביך בן אבינעם
13 “Ndipo mabaki ya watu wakashuka dhidi ya wenye nguvu, watu wa Bwana, wakashuka dhidi ya mashujaa wenye nguvu.
אז ירד שריד לאדירים עם יהוה ירד לי בגבורים
14 Kutoka Efraimu wakaja watu, ambao chimbuko lao ni Amaleki; Benyamini akiwa miongoni mwa watu waliokufuata. Kutoka Makiri wakashuka viongozi, na kutoka Zabuloni wale washikao fimbo ya jemadari.
מני אפרים שרשם בעמלק אחריך בנימין בעממיך מני מכיר ירדו מחקקים ומזבולן משכים בשבט ספר
15 Wakuu wa Isakari walikuwa pamoja na Debora; naam, Isakari alikuwa pamoja na Baraka, wakija nyuma yake kwa mbio wakielekea bondeni. Katika jamaa za Reubeni, palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.
ושרי ביששכר עם דברה ויששכר כן ברק בעמק שלח ברגליו בפלגות ראובן גדלים חקקי לב
16 Kwa nini ulikaa katikati ya mazizi ya kondoo kusikiliza sauti ya filimbi zinazoita makundi? Kwa jamaa za Reubeni, palikuwa na kujihoji kukubwa moyoni.
למה ישבת בין המשפתים לשמע שרקות עדרים לפלגות ראובן גדולים חקרי לב
17 Gileadi alikaa ngʼambo ya Yordani. Naye Dani, kwa nini alikaa kwenye merikebu siku nyingi? Asheri alikaa kwa utulivu ufuoni mwa bahari, akikaa kwenye ghuba zake ndogo.
גלעד בעבר הירדן שכן ודן למה יגור אניות אשר ישב לחוף ימים ועל מפרציו ישכון
18 Watu wa Zabuloni walihatarisha maisha yao, vilevile nao watu wa Naftali.
זבלון עם חרף נפשו למות-- ונפתלי על מרומי שדה
19 “Wafalme walikuja na kufanya vita; wafalme wa Kanaani walipigana huko Taanaki karibu na maji ya Megido, lakini hawakuchukua fedha wala nyara.
באו מלכים נלחמו אז נלחמו מלכי כנען בתענך על מי מגדו בצע כסף לא לקחו
20 Kutoka mbinguni nyota zilipigana, nyota kutoka njia zake zilipigana na Sisera.
מן שמים נלחמו הכוכבים ממסלותם נלחמו עם סיסרא
21 Mto wa Kishoni uliwasomba, ule mto wa zamani, mto wa Kishoni. Songa mbele, ee nafsi yangu, kwa ujasiri!
נחל קישון גרפם נחל קדומים נחל קישון תדרכי נפשי עז
22 Ndipo kwato za farasi zikafanya mshindo: farasi wake wenye nguvu huenda mbio kwa kurukaruka.
אז הלמו עקבי סוס מדהרות דהרות אביריו
23 Malaika wa Bwana akasema, ‘Merozi alaaniwe. Walaaniwe watu wake kwa uchungu, kwa kuwa hawakuja kumsaidia Bwana, kumsaidia Bwana dhidi ya hao wenye nguvu.’
אורו מרוז אמר מלאך יהוה--ארו ארור ישביה כי לא באו לעזרת יהוה לעזרת יהוה בגבורים
24 “Yaeli abarikiwe kuliko wanawake wote, mkewe Heberi, Mkeni, abarikiwe kuliko wanawake wote waishio kwenye mahema.
תברך מנשים--יעל אשת חבר הקיני מנשים באהל תברך
25 Aliomba maji, naye akampa maziwa; kwenye bakuli la heshima akamletea maziwa mgando.
מים שאל חלב נתנה בספל אדירים הקריבה חמאה
26 Akanyoosha mkono wake akashika kigingi cha hema, mkono wake wa kuume ukashika nyundo ya fundi. Akampiga Sisera kwa nyundo, akamponda kichwa chake, akamvunjavunja na kumtoboa paji lake la uso.
ידה ליתד תשלחנה וימינה להלמות עמלים והלמה סיסרא מחקה ראשו ומחצה וחלפה רקתו
27 Aliinama miguuni pa Yaeli, akaanguka; akalala hapo. Pale alipoinama miguuni pake, alianguka; pale alipoinamia, ndipo alipoanguka, akiwa amekufa.
בין רגליה כרע נפל שכב בין רגליה כרע נפל באשר כרע שם נפל שדוד
28 “Kupitia dirishani mamaye Sisera alichungulia; nyuma ya dirisha alilia, akasema, ‘Mbona gari lake linachelewa kufika? Mbona vishindo vya magari yake vimechelewa?’
בעד החלון נשקפה ותיבב אם סיסרא בעד האשנב מדוע בשש רכבו לבוא-- מדוע אחרו פעמי מרכבותיו
29 Wanawake wenye busara kuliko wengine wote wakamjibu; naam, husema moyoni mwake,
חכמות שרותיה תענינה אף היא תשיב אמריה לה
30 ‘Je, hawapati na kugawanya nyara: msichana mmoja au wawili kwa kila mtu, mavazi ya rangi mbalimbali kwa Sisera kuwa nyara, mavazi ya rangi mbalimbali yaliyotariziwa, mavazi yaliyotariziwa vizuri kwa ajili ya shingo yangu: yote haya yakiwa nyara?’
הלא ימצאו יחלקו שלל רחם רחמתים לראש גבר-- שלל צבעים לסיסרא שלל צבעים רקמה צבע רקמתים לצוארי שלל
31 “Adui zako wote na waangamie, Ee Bwana! Bali wote wakupendao na wawe kama jua lichomozavyo kwa nguvu zake.” Hivyo nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.
כן יאבדו כל אויביך יהוה ואהביו כצאת השמש בגברתו ותשקט הארץ ארבעים שנה

< Waamuzi 5 >