< Yoshua 16 >
1 Mgawanyo wa Yosefu ulianzia Yordani ya Yeriko, mashariki mwa miji ya Yeriko na kutoka hapo ulipanda kupitia jangwani na kuingia katika nchi ya vilima ya Betheli.
Nchi waliyopewa kabila la Yusufu ilianzia katika Yordani huko Yeriko, mashariki mwa chemichemi za Yeriko, kupitia nyikani, kupanda kutoka Yeriko kupitia nchi ya milima ya Betheli.
2 Ukaendelea kutoka Betheli (ndiyo Luzu), ukavuka kuingia eneo la Waariki huko Atarothi,
Kisha uliendelea kutoka Betheli hadi Luzi na kupita hata Atarothi, iliyo miliki ya Waarkiti.
3 ukateremkia kuelekea magharibi hadi eneo la Wayafleti ukienea hadi eneo la Beth-Horoni ya Chini hadi Gezeri, ukiishia baharini.
Kisha ilishuka chini upande wa magharibi kuelekea himaya ya Wayafuleti, hadi kufika miliki ya Loweri Bethi Horoni, na kisha iliendelea hadi Gezeri; na ilikomea katika bahari.
4 Kwa hiyo Manase na Efraimu, wazao wa Yosefu, walipokea urithi wao.
Ilikuwa ni kwa njia hii makabila ya Yusufu, yaani Manase na Efraimu yalipata urithi wao.
5 Hili ndilo lilikuwa eneo la Efraimu, ukoo kwa ukoo: Mpaka wa urithi wao ulianzia Ataroth-Adari upande wa mashariki hadi Beth-Horoni ya Juu,
Eneo la kabila la Efraimu ambalo lilikuwa limegawanya kwa koo zao lilikuwa kama ifuatavyo: mpaka wa urithi wao katika upande wa mashariki ulikuwa Atarothi Ada uliopanda kuelekea Bethi Horoni ya juu,
6 na kuendelea mpaka baharini. Kutoka Mikmeta upande wa kaskazini ulipinda kuelekea mashariki hadi Taanath-Shilo, ukiupita hadi Yanoa upande wa mashariki.
na kutoka pale uliendelea hadi katika bahari. Kutoka Mikimethathi katika upande wa Kasikazini ulipinda upande wa mashariki kuelkea Taanathi Shilo na kupita ng'ambo yake katika upande wa mashariki kukabili Yanoa.
7 Kisha uliteremka kutoka Yanoa hadi Atarothi na Naara, ukagusa Yeriko na kutokea katika Mto Yordani.
Kisha ulishuka kutoka Yanoa hadi Atarothi na hata Naara, na kisha ukafika Yeriko, na kuishia katika Yordani.
8 Kutoka Tapua mpaka ulikwenda magharibi hadi Bonde la Kana na kuishia baharini. Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Waefraimu, ukoo kwa ukoo.
Kutoka Tapua, mpaka uliendelea katika upande wa magharibi hata kijito cha Kana na ulikomea katika bahari. Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Efraimu, uliogawanywa katika koo zao,
9 Pia ulijumuisha miji yote na vijiji vyake ambavyo vilitengwa kwa ajili ya Waefraimu ndani ya urithi wa kabila la Manase.
pamoja na miji yao iliyochaguliwa kwa ajili ya kabila la Efraimu iliyokuwa ndani ya urithi wa kabila la Manase - miji yote pamoja na vijiji vyao.
10 Hawakuwatoa Wakanaani waishio Gezeri; mpaka leo Wakanaani wanaishi miongoni mwa watu wa Efraimu lakini wanatakiwa kufanya kazi ngumu za kulazimishwa.
Lakini hawakuwafukuza Wakanaani walioishi katika Gezeri, hivyo basi Wakanaani wanaishi ndani ya Efraimu hadi leo, lakini watu hawa walifanywa kuwa watumwa.