< Ezekieli 45 >
1 “‘Mtakapogawa nchi kuwa urithi, mtaitoa sehemu ya nchi kwa Bwana kuwa eneo takatifu, urefu wake dhiraa 25,000, upana wake dhiraa 20,000 eneo hili lote litakuwa takatifu.
Wakati mtakapogawanya nchi kama urithi, mtafanya sadakwa kwa Yahwe; sadaka hiyo itakuwa sehemu takatifu ya nchi, dhiraa elfu ishirini na tano urefu, na dhiraa elfu kumi upana. Patakuwa patakatifu, ndani ya mipaka yake yote.
2 Katika hiyo, itakuwepo sehemu mraba ambayo ni mahali patakatifu kila upande dhiraa 500 ikiwa imezungukwa na eneo la wazi lenye upana wa dhiraa hamsini.
Kutoka hapa kutakuwa na dhiraa mia tano kwa dhiraa mia tano za mraba kuzunguka mahali patakatifu, kwa kuuzunguka mpaka dhiraa hamsini upana.
3 Katika eneo takatifu, pima sehemu yenye urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000. Ndani ya hilo eneo kutakuwa mahali patakatifu, Patakatifu pa Patakatifu.
Kutoka hili eneo utapima fungu ambalo ni dhiraa elfu ishirini na tano urefu na elfu kumi upana; patakuwa patakatifu; mahali patakatifu palipo tukuka.
4 Itakuwa sehemu takatifu ya nchi kwa ajili ya makuhani, wale wanaohudumu ndani ya mahali patakatifu na ambao hukaribia ili kuhudumu mbele za Bwana. Patakuwa mahali pa nyumba zao pamoja na sehemu kwa ajili ya mahali patakatifu.
Patakuwa patakatifu katika nchi kwa ajili ya makuhani wanaomtumikia Yahwe, ajaye kwa Yahwe kumtumikia. Patakuwa mahali kwa ajili ya nyumba na eneo takatifu kwa ajili mahali patakatifu.
5 Eneo la urefu wa dhiraa 25,000 na upana wa dhiraa 10,000 litakuwa la Walawi wale wanaotumika hekaluni, kama milki yao kwa ajili ya miji ya kuishi.
Hivyo itakuwa dhiraa elfu ishirini na tano urefu na elfu kumi upana, patakuwa kwa ajili ya miji ya Walawi wanaotumika kwenye nyumba.
6 “‘Utatoa mji kama mali yao wenye upana wa dhiraa 5,000 na urefu wa dhiraa 25,000, karibu na sehemu takatifu, itakuwa mali ya nyumba yote ya Israeli.
Mtadhihirisha eneo moja kwa ajili ya mji, dhiraa elfu tano na urefu ishirini na tano, hapo patakuwa kando kando ya eneo lililohifadhiwa kwa ajili ya mahali patakatifu; huu mji utakuwa wa mali ya nyumba yote ya Israeli.
7 “‘Mkuu anayetawala atakuwa na lile eneo linalopakana na lile eneo lililowekwa wakfu upande huu na upande huu na eneo la mji. Eneo la mji litaenea upande wa magharibi kuanzia upande wa magharibi na upande wa mashariki kuanzia upande wa mashariki, likiendelea kwa urefu kutoka magharibi hadi mpaka wa mashariki sambamba na mojawapo ya sehemu za makabila.
Nchi ya mwana mfalme itakuwa kwa pande zote za eneo lililohifadhiwa kwa ajili ya mahali patakatifu na mji. Patakuwa kwa upande wao wa magaharibi na upande wa mashariki. Urefu utalingana na urefu wa moja ya hayo mafungu, kutoka magaribi hata mashariki.
8 Nchi hii itakuwa milki yake katika Israeli. Nao wakuu wangu hawataonea tena watu wangu bali watairuhusu nyumba ya Israeli kuimiliki nchi kulingana na makabila yao.
Hii nchi itakuwa mali ya mwana mfalme katika Isaraeli. Wana wafalme hawatawakandamiza watu wangu; badala yake, watawapatia nchi kwa nyumba ya Israeli, kwa ajili ya makabila yao.
9 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Yatosha, enyi wakuu wa Israeli! Acheni mbali ukatili wenu na uonevu wenu mkafanye lile lililo haki na sawa. Acheni kuwatoza watu wangu isivyo haki, asema Bwana Mwenyezi.
Bwana Yahwe asema hivi: Inatosha kwa ajili yenu, mwana mfalme wa Israeli! Ondoa dhuluma na mgogoro; fanya hukumu na haki! Usiwafukuze wapangaji wa watu wangu! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
10 Tumieni mizani sahihi na vipimo sahihi vya efa na bathi.
Mtakuwa na mzani sahihi, efa sahihi, na bathi sahihi!
11 Efa na bathi viwe sawa, bathi iwe sehemu ya kumi ya homeri na efa iwe sehemu ya kumi ya homeri, homeri itakuwa ndicho kiwango cha kukubalika kwa vyote viwili.
Efa na bathi zitakuwa kiasi kile kile, ili kwamba bathi iwe zaka ya homeri; efa itakuwa zaka ya hamori moja. Vipimo vyao vitakuwa vinafanana na homeri.
12 Shekeli moja itakuwa gera ishirini. Shekeli ishirini, jumlisha na shekeli ishirini na tano, jumlisha na shekeli kumi na tano zitakuwa mina moja.
Shekeli zitakuwa gera ishirini, shekeli sita zitakuwa mane yenu.
13 “‘Hili ndilo toleo maalum mtakalotoa: moja ya sita ya efa kutoka kila homeri ya ngano na moja ya sita ya efa kutoka kila homeri ya shayiri.
Hili ndilo toleo mtakalotoa: efa sita kwa kila homeri ya ngano, na mtatoa efa sita kwa kila homeri ya shayiri.
14 Sehemu ya mafuta iliyoamriwa, yaliyopimwa kwa bathi, ni sehemu ya kumi ya bathi kutoka kila kori moja (ambayo ina bathi kumi au homeri moja.)
Sadaka ya kawaida ya mafuta itakuwa zaka ya bathi kwa kila kori (ambazo ni bathi), au kwa kila hamori, kwa kuwa hamori moja ni bathi kumi pia.
15 Pia kondoo mmoja atachukuliwa kutoka kwenye kila kundi la kondoo mia mbili kutoka kwenye malisho yaliyonyeshewa vizuri ya Israeli. Hivi vitatumika kwa ajili ya sadaka ya nafaka, sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani ili kufanya upatanisho kwa ajili ya watu, asema Bwana Mwenyezi.
Kondoo mmoja au mbuzi kutoka mifugo kwa kila wanyama mia mbili kutoka malisho ya maji ya mikoa ya Israeli yatatumika kwa sadaka ya kuteketezwa yoyote au sadaka ya amani kufanya upatanisho kwa ajili ya watu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
16 Watu wote wa nchi wataungana pamoja na mkuu anayetawala Israeli ili kutoa hii sadaka maalum.
Watu wote wa nchi watatoa hii sadaka kwa mwana mfalme wa Israeli.
17 Huu utakuwa ndio wajibu wa mkuu anayetawala kutoa sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kwenye sikukuu, Mwezi Mwandamo na Sabato, kwenye sikukuu zote zilizoamriwa za nyumba ya Israeli. Atatoa sadaka za dhambi, sadaka za nafaka, sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nyumba ya Israeli.
Utakuwa wajibu wa mwana mfalme kutoa wanyama kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka ya unga, sadaka ya kinywaji, katika siku za sikukuu na sherehe za mwezi mpya, na katika siku za Sabato-sikukuu zote za kudumu za nyumba ya Israeli. Ataandaa kwa ajili ya sadaka za dhambi, sadaka za unga, sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani kwa ajili ya upatanisho badala ya nyumba ya Israeli.
18 “‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya huo mwezi utamchukua fahali mchanga asiye na dosari na kutakasa mahali patakatifu.
Bwana Yahwe asema hivi: Katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, utachukua ng'ombe mmoja asiyekuwa na dosari kutoka kwenye kundi na kufanya sadaka ya dhambi kwa ajili ya patakatifu.
19 Kuhani itampasa achukue sehemu ya hiyo damu ya sadaka ya dhambi na kuipaka kwenye miimo ya Hekalu, kwenye pembe nne za juu za ukingo wa hayo madhabahu na juu ya miimo ya lango la ukumbi wa ndani.
Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi na kuiweka juu ya miimo ya mlango na kwenye pembe nne za mpaka wa madhabahu, na miimo ya lango la uzio wa ndani.
20 Itakupasa kufanya vivyo hivyo katika siku ya saba ya mwezi huo kwa ajili ya mtu yeyote ambaye hutenda dhambi bila kukusudia au bila kujua, hivyo utafanya upatanisho kwa ajili ya Hekalu.
Utafanya hivyo siku ya saba ya mwezi kwa dhambi ya kila mtu kwa ajali au ujinga; katika njia hii mtaipatanisha hekalu.
21 “‘Katika mwezi wa kwanza siku ya kumi na nne utaadhimisha Pasaka. Sikukuu itaendelea kwa siku saba, wakati huo wa hizo siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu.
Katika siku ya mwezi siku ya kumi na nne ya mwezi, mtakuwa na sikukuu, sikukuu ya siku saba. Matakula makate usiotiwa chachu.
22 Katika siku hiyo mkuu anayetawala atatoa fahali kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu wote wa nchi.
Siku hiyo, mwana mfalme ataandaa ng'ombe kwa ajili yake na kwa ajili ya watu wote wa nchi kama sadaka ya dhambi.
23 Kila siku wakati wa hizo siku saba za sikukuu atatoa mafahali saba na kondoo dume saba wasio na dosari kuwa sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana na beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi.
Kwa siku saba za sikukuu, mwana wa mfalme ataandaa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Yahwe: ng'ombe saba na kondoo dume saba zisizokuwa na dosari kila siku kwa mda wa siku saba, na mbuzi dume kila siku kama sadaka ya dhambi.
24 Pia atatoa sadaka ya nafaka efa moja kwa kila fahali na efa moja kwa kila kondoo dume, pamoja na hini moja ya mafuta kwa kila efa.
Kisha mwana mfalme atatengeneza sadaka ya chakula ya efa moja kwa kila ng'ombe na efa moja kwa kila kondoo dume pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.
25 “‘Wakati wa hizo siku saba za sikukuu, ambayo huanza katika mwezi wa saba kwenye siku ya kumi na tano, mkuu anayetawala atatoa mahitaji yale yale kwa ajili ya sadaka za dhambi, sadaka za kuteketezwa, sadaka za nafaka na mafuta.
Katika siku ya saba ya mwezi siku ya kumi na tano ya mwezi, katika sikukuu, mwana wa mfalme atafanya matoleo katika siku hizi saba: sadaka za dhambi, sadaka za kuteketezwa, sadaka za chakula, na sadaka za mafuta.