< 2 Wafalme 5 >
1 Wakati huu, Naamani alikuwa jemadari wa jeshi la mfalme wa Aramu. Alikuwa mtu mkuu mbele ya bwana wake na aliyeheshimiwa sana, kwa sababu kupitia kwake, Bwana alikuwa amewapa Aramu ushindi. Alikuwa askari shujaa, lakini alikuwa na ukoma.
Basi Naamani, amri jeshi wa mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa na mtu mwenye kuheshimiwa mbele ya bwana wake, kwa sababu kwa ajili yake Yahwe aliwapa ushindi Washami. Pia alikuwa hodari, mtu shujaa, lakini alikuwa anaukoma.
2 Siku hizo vikosi kutoka Aramu vilikuwa vimekwenda na vikawa vimemteka msichana kutoka Israeli, naye akamtumikia mkewe Naamani.
Washami walikuwa wametoka kuongoza kikosi na kumchukua kijana mdogo wa kike kutoka nchi ya Israeli. Akamuhudumia mke wa Naamani.
3 Akamwambia bibi yake, “Kama bwana wangu angelimwona nabii aliyeko Samaria! Angemponya ukoma wake.”
Yule binti akamwambia bibi yake, “Natamani kwamba bwana wangu angelikuwa na nabii ambaye yupo Samaria! Halafu angelimponya bwana wangu ukoma wake.
4 Naamani akaenda kwa bwana wake na kumwambia alichosema yule msichana kutoka Israeli.
Hivyo Naamani akaingia na kumwambia mfalme kile ambacho yule binti kutoka nchi ya Israeli alichokuwa amekisechosema.
5 Mfalme wa Aramu akamjibu, “Hakika, nenda. Nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Kwa hiyo Naamani akaondoka, akiwa amechukua talanta kumi za fedha, shekeli 6,000 za dhahabu, na mivao kumi ya mavazi.
Kisha mfalme wa Shamu akase, “Nenda sasa, na nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Naamani akaondoka na kuchukua talanta zake kumi za fedha, vipande elfu sita vya dhahabu, na nguo kumi za kubadilisha.
6 Barua aliyopelekea mfalme wa Israeli iliandikwa hivi: “Pamoja na barua hii ninamtuma mtumishi wangu, Naamani, kwako ili uweze kumponya ukoma wake.”
Pia alichukua barua ya kumpelekea mfalme wa Israeli inayosema, “Sasa wakati hii barua itakapoletwa kwako, utaona kwamba nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, hivyo basi utamponya ukoma wake.”
7 Mara mfalme wa Israeli alipomaliza kuisoma ile barua, akararua mavazi yake na kusema, “Je, mimi ni Mungu? Je, mimi naweza kuua na kufufua tena? Kwa nini huyu mtu anamtuma mtu ili mimi nipate kumponya ukoma wake? Tazama jinsi anavyotafuta kuanzisha ugomvi nami!”
Wakati mfalme wa Israeli alipoisoma ile barua, alichana mavazi yake na kusema, “Je mimi ni Mungu, niue na nirudishe uhai, kwamba huyu mtu anataka nimponye mtu ukoma wake? Inaonekana anatafuta mashindano na mimi.”
8 Elisha mtu wa Mungu aliposikia kwamba mfalme wa Israeli alikuwa amerarua mavazi yake, akamtumia ujumbe huu: “Kwa nini umerarua mavazi yako? Mwamuru mtu huyo aje kwangu, naye atajua ya kuwa yuko nabii katika Israeli.”
Ikawa wakati Elisha mtu wa Mungu aliposikia kwamba mfalme wa Israeli alichana nguo zake, akatuma neno kwa mfalme akisema, “Kwa nini umechana nguo zako? Muache aje kwangu sasa, na atajua kwamba kuna nabii katika Israeli.”
9 Kwa hiyo Naamani akaenda, akiwa na farasi zake na magari yake, na kusimama mlangoni mwa nyumba ya Elisha.
Basi Naamani akaja na farasi wake na mikokoteni yake ya kukokotwa na farasi na kusimama kwenye mlango wa nyumba ya Elisha.
10 Elisha akamtuma mjumbe kumwambia, “Nenda uoge katika Yordani mara saba, na nyama ya mwili wako itapona, nawe utatakasika.”
Elisha akamtumia mjumbe, akisema, “Nenda na ukazame mwenyewe katika Yordani mara saba, na ngozi ya mwili wako itajirudi; utakuwa msafi.”
11 Lakini Naamani akaondoka akiwa amekasirika, akasema, “Hakika nilidhani kwamba angetoka nje, asimame na kuliitia jina la Bwana Mungu wake, na kuweka mkono wake juu ya mahali pagonjwa, aniponye ukoma wangu.
Lakini Naamani alikasirika na kuondoka na kusema, “Tazama, Nilidhani bila shaka angekuja kwangu na kusimama na kuliita jina la Yahwe Mungu wake, na kupitisha mkono wake kwenye sehemu ya ugonjwa na kuponya ukoma wangu.
12 Je, Abana na Farpari, mito ya Dameski, si bora zaidi kuliko mito yoyote ya Israeli? Je, nisingeweza kuoga ndani ya hiyo mito na kutakasika?” Basi akageuka na kuondoka kwa hasira kuu.
Je sio Abana na Faepari, mito ya Damaskasi, bora kuliko maji yote ya Israeli?” Je siwezi kuoga ndani yao na kuwa safi?” Hivyo akageuka na kwenda kwa hasira.
13 Watumishi wa Naamani wakamwendea na kumwambia, “Baba yangu, kama huyo nabii angekuambia kufanya jambo lililo kubwa, je, usingelifanya? Je, si zaidi sana basi, anapokuambia, ‘Oga na utakasike!’”
Ndipo watumishi wa Naamani wakaja karibbu na kumwambia, “Baba yangu, kama yule nabii alikuamuru kufanya kitu kigumu, singelifanya? Je si zaidi basi, atakapokwambia rahisi, 'Zama mwenyewe na uwe safi?”
14 Hivyo akashuka na kujizamisha ndani ya Yordani mara saba, kama vile huyo mtu wa Mungu alivyokuwa amemwambia, nayo nyama ya mwili wake ikapona na kutakasika kama ya mwili wa mvulana mdogo.
Ndipo akashuka chini na kuzama mwenyewe mara saba kwenye Yordani, akitii maelekezo ya mtu wa Mungu. Nyama ya mwili wake ikarudi tena kama nyama ya mwili ya mtoto mdogo, na alikuwa amepona.
15 Kisha Naamani na wahudumu wake wote wakarudi kwa yule mtu wa Mungu. Akasimama mbele yake na kusema, “Sasa najua kwamba hakuna Mungu katika ulimwengu wote isipokuwa katika Israeli. Tafadhali sasa upokee zawadi kutoka kwa mtumishi wako.”
Naamani akarudi kwa yule mtu wa Mungu, yeye na watu wake wengine, na kuja na kusimama mbele yake. Akasema, “Tazama, sasa najua kwamba hakuna Mungu katika Dunia nzima isipokuwa katika Israeli. Kwa hiyo basi, chukua zawadi kutoka kwa mtumishi wako tafadhali.”
16 Nabii akajibu, “Hakika kama Bwana aishivyo, ambaye ninamtumikia, sitapokea kitu hata kimoja.” Ingawa Naamani alimsihi sana, yeye alikataa.
Lakini Elisha akajibu, “Kama Yahwe aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sintopokea chochote.”Naamani akamsihi Elisha apokee zawadi, lakini alikataa.
17 Naamani akasema, “Ikiwa hutapokea, tafadhali mtumishi wako na apewe udongo kiasi cha mzigo wa kuweza kubebwa na punda wawili, kwa sababu mtumishi wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa na dhabihu kwa mungu mwingine isipokuwa Bwana.
Hivyo Naamani akasema, “Kama sivyo, nakuomba ache apewe mtumishi wako pale mzigo wa baghala mbili za aridhi, kwa kuwa kuanzia sasa, mtumishi wako hatotoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa mungu yeyote isipokuwa Yahwe.
18 Lakini Bwana na amsamehe mtumishi wake kwa kitu hiki kimoja: Wakati bwana wangu atakapoingia kwenye hekalu la Rimoni ili kusujudu, naye akiwa anauegemea mkono wangu, nami nikasujudu huko pia, wakati nitakaposujudu ndani ya hekalu la Rimoni, Bwana na amsamehe mtumishi wako kwa ajili ya jambo hili.”
Katika jambo hili moja Yahwe anaweza kumsamehe mtumishi wako, hii ni, wakati mfalme wangu atakapoenda kwenye nyumba ya Rimoni kuabudu pale, na kujifunza kwenye mikono yangu na kumuinamia mwenyewe kwenye nyumba ya Rimoni, Yahwe aweze kumsamehe mtumishi wako katika hili jambo.”
19 Elisha akamwambia, “Nenda kwa amani.” Baada ya Naamani kusafiri umbali fulani,
Elisha akamwambia, “Nenda kwa amani.” Hivyo Naamani akaondoka.
20 Gehazi, mtumishi wa Elisha mtu wa Mungu, akajiambia mwenyewe, “Bwana wangu amemwachia kirahisi sana Naamani, huyu Mwaramu, kwa kutokupokea kutoka kwake vile alivyovileta. Hakika kama Bwana aishivyo, nitamkimbilia na kupata kitu kutoka kwake.”
Alikuwa amesafiri lakini umbali mfupi, wakati Gehazi mtumishi wa Elisha mtumishi wa Mungu alisema mwenyewe, “Tazama, bwana wangu amemuandaa huyu Naamani Mshami kwa kuacha kupokea zawadi kutoka kwenye mikono yake ambazo alizileta. Kama Yahwe aishivyo, Nitakimbia nikimfuata na kupokea kitu kutoka kwake.
21 Hivyo Gehazi akaharakisha kumfuatilia Naamani. Naamani alipomwona akikimbia kumwelekea, akashuka chini kutoka kwenye gari lake na kwenda kumlaki. Akauliza, “Je, mambo yote ni sawa?”
Hivyo Gehazi akamfuata Naamani. Wakati Naamani alipomuona mtu mmoja anakimbia akimfuata, aliruka chini kutoka kwenye gari yake kuonana naye na kusema, “Je kila kitu kiko sawa?”
22 Gehazi akajibu, “Mambo yote ni sawa. Bwana wangu amenituma nikuambie, ‘Vijana wawili kutoka kwa wana wa manabii wamenijia kutoka nchi ya vilima ya Efraimu. Tafadhali wape talanta ya fedha na mivao miwili ya mavazi.’”
Gehazi akasema, “kila kitu kiko sawa. Bwana wangu amenituma, akisema, 'Tazama, sasa wamekuja kwangu kutoka nchi ya mlima ya Efraimu vijana wawili wa watoto wa manabii. Tafadhali, wapatie talanta ya fedha na nguo mbili za kubadilisha.”
23 Naamani akasema, “Hakika, chukua talanta mbili za fedha.” Akamsihi Gehazi azipokee, kisha akafunga talanta mbili za fedha katika mifuko miwili pamoja na mivao miwili ya mavazi. Akawapa watumishi wake wawili mizigo hiyo, nao wakaibeba wakitangulia mbele ya Gehazi.
Naamani akajibu, “Ninafuraha kubwa kukupatia talanta mbili.” Naamani akamsihi Gehazi na kujaribu talanta mbili za fedha kwenye mifuko miwili ya kubebea, pamoja na nguo mbili za kubadilisha, na kutandaza kwa wafanyakazi wake wawili, ambao walikuwa wamebebea ile mifuko miwili ya fedha mbele ya Gehazi.
24 Gehazi alipofika kwenye kilima, akavichukua vile vitu kutoka kwa wale watumishi na kuvificha ndani ya nyumba. Akawaaga wale watu, nao wakaondoka.
Wakati Gehazi alipokuja kwenye ule mlima, alichukua ile mifuko ya fedha kutoka kwenye mikono yao na kuificha kwenye nyumba; akawatuma wale watu, na wakaondoka.
25 Kisha akaingia ndani na kusimama mbele ya Elisha bwana wake. Elisha akamuuliza, “Gehazi, ulikuwa wapi?” Gehazi akajibu, “Mtumishi wako hakwenda popote.”
Wakati Gehazi alipoingia na kusimama mbele ya bwana wake, Elisha akamwambia, “Umetokea wapi, Gehazi?” Akajibu, “Mtumishi wako hakwenda mahali.”
26 Lakini Elisha akamwambia, “Je, roho yangu haikuwa pamoja nawe wakati yule mtu aliposhuka kutoka kwenye gari lake ili kukulaki? Je, huu ni wakati wa kupokea fedha au kupokea nguo, mashamba ya mizeituni, mashamba ya mizabibu, makundi ya kondoo na mbuzi, makundi ya ngʼombe, au watumishi wa kiume na wa kike?
Elisha akamwambia Gehazi, “Je roho yangu haikuwa na wewe wakati yule mtu alipoyarudisha magari yake ya farasi ili kukutana na wewe? Je uu ni mda wa kupokea pesa na nguo, mashamba ya mzaituni na mizabibu, na kondoo na Ng'ombe, na watumishi wakiume na watumishi wakike?
27 Ukoma wa Naamani utakushika wewe na wazao wako milele.” Kisha Gehazi akaondoka mbele ya Elisha, mwenye ukoma, mweupe kama theluji.
Basi ukoma wa Naamani utakuwa kwenye uzao wako daima.” Basi Gehazi akatoka kwenye uwepo wake, mwenye ukoma kama theluji.