< 2 Nyakati 19 >

1 Mfalme Yehoshafati wa Yuda akarudi salama kwenye jumba lake la kifalme huko Yerusalemu.
Yehoshafati mfalme wa Yuda akarudi salama nyumbani kwake Yerusalemu.
2 Yehu mwonaji, mwana wa Hanani, akapanda kwenda kuonana naye akamwambia Mfalme Yehoshafati, “Je, utawasaidia waovu na kuwapenda wale wanaomchukia Bwana? Kwa sababu ya jambo hili, ghadhabu ya Bwana iko juu yako.
Kisha Yehu mwana wa Hanani, mwonaji, akatoka kukutana naye na akasema kwa mfalme Yehoshafati, “Unapaswa kuwa unawasaidia waovu? Unapaswa kuwapenda wanaomchukia Yahwe? Kwa ajili ya tendo hili, ghadhabu toka kwa Yahwe iko juu yako.
3 Hata hivyo, kuna mema yaliyoonekana kwako, kwa kuwa umeondoa katika nchi nguzo za Ashera na umeukaza moyo wako katika kumtafuta Mungu.”
Aidha, kuna baadhi ya mema ya kuonekana ndani yako, kwamba umeziondosha Maashera nje ya nchi, na umeukaza moyo wako kumtafuta Mungu.”
4 Yehoshafati aliishi huko Yerusalemu, naye akatoka akaenda tena miongoni mwa watu, kuanzia Beer-Sheba hadi nchi ya vilima ya Efraimu na kuwageuza wakamrudia Bwana, Mungu wa baba zao.
Yehoshafati akaishi katika Yerusalemu; na akaenda nje tena miongoni mwa watu wa Beer- sheba hadi nchi ya kilima ya Efraimu na akawarudisha kwa Yahwe, Mungu wa baba zao.
5 Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye maboma.
Akaweka waamuzi katika nchi katika miji yote ya Yuda yenye angome, mji kwa mji.
6 Akawaambia, “Angalieni kwa makini yale mtendayo, kwa kuwa hamkuhukumu kwa ajili ya mwanadamu bali kwa ajili ya Bwana ambaye yu pamoja nanyi kila mtoapo hukumu.
Akawaambia waamuzi, “Zingatieni mnachopaswa kufanya, kwa sababu hamuamui kwa ajili ya mwanadamu, bali kwa ajili ya Yahwe; yuko pamoja nanyi katika kazi ya kuamua,
7 Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwa Bwana Mungu wetu hakuna jambo lisilo la haki, upendeleo, wala rushwa.”
Basi sas iacheni hofu ya Mungu iwe juu yenu. Iweni waangaliafu mnapoamua, kwa maana hakuna uovu wa Yahwe Mungu wetu, wala hakuna upendeleo wala hongo.”
8 Pia huko Yerusalemu, Yehoshafati akaweka baadhi ya Walawi, makuhani na viongozi wa jamaa za Waisraeli ili kutoa hukumu kwa ajili ya Bwana na kuamua magomvi. Nao waliishi huko Yerusalemu.
Vile vile, katika Yerusalemu Yehoshafati akateua baadhi ya Walawi na makuhani, na baahdhi ya viongozi wa nyumba za mababu wa Israeli, kwa ajili ya kufanya hukumu kwa ajili ya Yahwe, na kwa ajili ya migogoro. Wakaishi katika Yerusalemu.
9 Akawapa maagizo haya: “Ni lazima mtumike kwa uaminifu na kwa moyo wote katika kicho cha Bwana.
Akawaelekeza, akisema, “Lazima mtumike kwa heshima kwa ajaili ya Yahwe, kwa uaminifu, na na kwa moyo wenu wote.
10 Katika kila shauri lifikalo mbele yenu kutoka kwa ndugu zenu wale waishio katika miji, ikiwa ni la umwagaji wa damu au mambo mengine yahusuyo sheria, amri, hukumu au maagizo, inawapasa ninyi kuwaonya kwamba wasiingie katika hatia dhidi ya Bwana, la sivyo ghadhabu yake itakuja juu yenu na ndugu zenu. Tendeni hivyo, nanyi hamtatenda dhambi.
Kila mgogoro wowote utakapokuja kwenu kutoka kwa ndugu zenu wanaoishi katika miji yao, iwe inahusu mauji, iwe inhusu torati na amri, lazim muwaonye, ili kwamba wasiwe na hatia mbele za Yahwe, la sivyo ghadhabu itakuja juu yenu na juu ya ndugu zenu. Mnapaswa kufanya hivyo na hamtakuwa na hatia
11 “Amaria kuhani mkuu atakuwa juu yenu katika jambo lolote linalomhusu Bwana naye Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa kabila la Yuda, atakuwa juu yenu kwa jambo lolote linalomhusu mfalme, nao Walawi watatumika kama maafisa mbele yenu. Tendeni kwa ujasiri, naye Bwana atakuwa pamoja na wale watendao vyema.”
Ona, Amaria kuhani mkuu yuko juu yenu katika mambo yote ya Yahwe. Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa nyumba ya Yuda, ni kiongozi katika yote katika mambo yote ya mfalme. Pia, Walawi watakuwa wasimamizi wakiwatumikia ninyi. Muwe hodari na tiini maelekezo yenu, na Yahwe awe moja nao walio wema.”

< 2 Nyakati 19 >