< Исход 4 >
1 Отвеща же Моисей и рече: аще не уверуют ми, ниже послушают гласа моего, рекут бо, яко не явися тебе Бог, что реку к ним?
Musa akajibu, “Lakini itakuwaje wasiponiamini mimi au wasiponisikiliza na kusema, 'Yahwe hajakutokea wewe?”
2 И рече к нему Господь: что сие есть в руце твоей? Он же рече: жезл.
Yahwe akamwambia, “Hicho ni nini mkononi mwako?” Musa aksema, “Ni fimbo.”
3 И рече: поверзи его на землю. И верже и на землю, и бысть змий: и отбеже Моисей от него.
Yahwe akasema, “Itupe chini.” Musa akaitupa chini ile fimbo, nayo ikageuka na kuwa nyoka. Musa akarudi nyumba.
4 И рече Господь к Моисею: простри руку и ими за хвост. Простер убо руку, взя за хвост, и бысть жезл в руце его.
Yahwe akamwambia Musa, “Mchukue kwa kumshikia mkia wake.” Hivyo alimchukua yule nyoka. Mara ikaggeuka na kuwa fimbo mkononi mwake tena.
5 Да уверуют ти, яко явися тебе Господь Бог отец твоих, Бог Авраамов и Бог Исааков и Бог Иаковль.
“Hii ni ili wapate kuamini ya kuwa Yahwe, Mungu wa baba zao, Mungu wa wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amekutokea wewe.”
6 Рече же ему Господь паки: вложи руку твою в недро твое. И вложи руку в недро свое, и изят ю от недра своего, и бысть рука его прокажена яко снег.
Yahwe pia alimwambia, “Sasaingiza mkono wako ndani ya vazi lako.” Hivyo Musa akaingiza mkono wake ndani ya vazi lake. Na alipoutoa nje, tazama, mkono wake ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji.
7 И рече паки ему Господь: вложи руку твою в недро твое. И вложи руку свою в недро свое, и изят ю от недра своего, и бысть паки в румянстве плоти своея.
Yahwe akasema, “Ingiza mkono wako ndani ya vazi lako tena.” Hivyo akaingiza mkono wake ndani ya vazi lake, na alipoutoa nje aliona ukiwa mzima tena kama ulivyo mwili wake wote.
8 Аще же не уверуют тебе, ниже послушают гласа знамения перваго, уверуют тебе ради гласа знамения втораго:
Yahwe akasema, “Kama hawatakuamini wewe - kama hawatazingatia ishara yanggu ya kwanza ya nguvu zangu au kuziamini, basi wataamini ishara ya pili.
9 и будет аще не уверуют тебе двема знамениями сими, ниже послушают гласа твоего, да возмеши от воды речныя, и пролиеши на сухо: и будет вода, юже возмеши от реки, кровию на сусе.
Na ikiwa hawataamini hata ishara hizi zote mbili za nguvu zangu, au wasipokusikiliza wewe, basi chota maji kutoka katika mto na uyamwage katika nchi kavu. Maji utakayoyamwaga yatakuwa damu katika nchi kavu.”
10 Рече же Моисей ко Господу: молюся ти, Господи: недоброречив есмь прежде вчерашняго и третияго дне, ниже отнележе начал еси глаголати рабу Твоему: худогласен и косноязычен аз есмь.
Ndipo Musa akamwambia Yahwe, “Bwana, mimi ni mzuri wa kuongea, si hapo kwanza au hata baada ya kuwa umeongea na mtumishi wako. Mimi ni mdhaifu wa kuongea na nina kigugumizi.”
11 И рече Господь к Моисею: кто даде уста человеку? И кто сотвори нема и глуха, и видяща и слепа? Не Аз ли Господь Бог?
Yahwe akamwambia, “Ni nani anayeumba mdomo wa mwanadamu? Ni nani amfanyaye mwanadamu kuwa bubu au aone au kipofu? Je si mimi Yahwe?
12 И ныне иди, и Аз отверзу уста твоя и устрою тебе, еже имаши глаголати.
Sasa nenda, nami nitauongoza mdomo wako na nitakufundisha cha kusema.”
13 Рече же Моисей: молюся ти, Господи, избери могуща иного, егоже послеши.
Lakini Musa akasema, “Bwana, tafadhali mtume mtu mwingine, yeyote unayependa kumtuma.”
14 И разгневався яростию Господь на Моисеа, рече: не се ли брат твой Аарон Левитин? Вем, яко глаголя возглаголет он вместо тебе: и се, той изыдет во сретение тебе, и узрев тя, возрадуется в себе:
Kisha Yahwe akamkasirikia Musa. Akasema, “Vipi kuhusu Aroni kaka yako yule Mlawi? Najua ya kuwa anaweza kuongea vizuri. Hata hivyo, anakuja kukutana na wewe, na atakapokuona moyo wake utajawa na furaha.
15 и речеши к нему, и вдаси словеса Моя во уста его: Аз же отверзу уста твоя и уста его, и устрою вам яже имате творити:
Wewe utaongea naye na utaweka maneno ya kusema kinywani mwake. Nami nitakiongoza kinywa chako na kinywa chake pia, nami nitaonesha ninyi nyote yawapasayo kutenda.
16 и той возглаголет от тебе к людем, и той будет уста твоя: ты же будеши ему в тех, яже к Богу:
Yeye ataongea na watu kwa niaba yako. Yeye atakuwa msemaji wako, na wewe utakuwa kama Mungu kwake.
17 и жезл сей обращенный в змию, возми в руку твою, сим сотвориши знамения.
Utachukua hii fimbo pamoja nawe mkononi mwako. Kwa fimbo hii utafanya ishara.”
18 Пойде же Моисей, и возвратися ко Иофору тестю своему и рече: пойду и возвращуся ко братии моей, иже во Египте, и увижду, аще еще живи суть. И рече Иофор к Моисею: иди здрав. По днех же оных многих, умре царь Египетский.
Hivyo Musa alirudi kwa Yethro - baba mkwe wake na kumwambia, “Niruhusu nipate kurudi kwa ndugu zangu walioko Misri ili niweze kuona kama bado wako hai.” Yethro akwambia Musa, “Nenda kwa amani.”
19 И рече Господь к Моисею в земли Мадиамстей: иди, отиди во Египет: измроша бо вси ищущии души твоея.
Yahwe akamwambia Musa kule Midiani, “Nenda, rudi Misri, kwa kuwa watu wote waliotaka kukuua wameshakufa.”
20 Поим же Моисей жену свою и отрочата, всади я на ослята, и возвратися во Египет. И взя Моисей жезл, иже от Бога, в руку свою.
Musa akamchukua mke wake na watoto wake wa kiume na kuwapandisha kwenye punda. Akarudi mpaka nchi ya Misri, naye alichukua fimbo ya Mungu pamoja naye mkononi mwake.
21 Рече же Господь к Моисею: идущу тебе и возвращающуся во Египет, зри вся чудеса, яже дах в руце твои, да сотвориши Я пред фараоном: Аз же ожесточу сердце его, и не отпустит людий:
Yahwe akamwambia Musa, “Utakaporudi Misri, jitahidi kufanya ishara zote nilizokupa kufanya mbele ya Farao. Lakini nitaufanya moyo wake kuwa mgumu, naye hawatawaacha watu waende.
22 ты же возглаголеши фараону: сия глаголет Господь Бог Еврейский: сын Мой первенец Израиль:
Lazima umwambie Farao, 'Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: Israeli ni mtoto wangu, mzaliwa wa kwanza wangu,
23 рех же тебе: отпусти люди Моя, да Ми послужат: аще убо не хощеши отпустити их, блюди убо, Аз убию сына твоего первенца.
nami nakuamuru, “Mwache mwanangu aende ili apate kuniabudu mimi.” Lakini kwa kuwa umekataa kumwachia, hakika nitamuua mtoto wako wa kiume, mzaliwa wa kwanza wako.”'
24 Бысть же на пути на стану, срете его Ангел Господнь и искаше его убити.
Sasa wakiwa njiani, wakati wa usiku walipopumzika, Yahwe alikutana na Musa na kutaka kumuua.
25 И вземши Сепфора камень, обреза конечную плоть сына своего, и припаде к ногам его и рече: ста кровь обрезания сына моего.
Kisha Zipora akachukua kisu kikali na kukata govi la mtoto wake wa kiume na kuligusisha miguuni pake. Kisha akasema, “Hakika wewe ni bwana harusi wangu kwa njia ya damu.”
26 И отиде от него Ангел, занеже рече: ста кровь обрезания сына моего.
Hivyo Yahwe akamwachia. Akasema, “Wewe ni bwana harusi wa damu” kwa sababu ya kutahiriwa.
27 Рече же Господь ко Аарону: изыди во сретение Моисею в пустыню. И иде, и срете его в горе Божии: и целовастася оба.
Yahwe akamwambia Aroni, “Nenda nyikani ukutane na Musa.” Aroni akaenda na kukutana naye katika mlima wa Mungu, na kumbusu.
28 И поведа Моисей Аарону вся словеса Господня, яже посла, и вся знамения, яже заповеда ему.
Musa akwambia Aroni maneno yote ya Yahwe ambayo alimtuma kusema na kwa habari za ishara zote za nguvu za Yahwe ambazo alimwagiza kutenda.
29 Иде же Моисей и Аарон, и собраша вся старцы сынов Израилевых:
Kisha Musa na Aroni wakaenda na kuwakusanya wazee wote wa Israeli.
30 и глагола им Аарон вся словеса сия, яже глагола Бог к Моисею: и сотвори знамения пред людьми.
Aroni akawaambia maneno yote ambayo Yahwe alimwambia Musa. Pia alionesha ishara na miujiza ya nguvu za Yahwe mbele ya watu.
31 И вероваша людие, и возрадовашася, яко посети Бог сыны Израилевы и яко призре на их скорбение: и преклоншеся людие поклонишася.
Watu waliamini. Waliposikia ya kuwa Yahwe aliwaona Waisraeli na ya kwamba aliyaona mateso yao, waliinamisha vichwa vyao na kumwabudu.