< Yohana 5 >
1 Baadae pabile ni sikukuu ya Ayahudi, ni Yesu aboi kuyenda Yerusalemu.
Baada ya haya, kulikuwa na Sikukuu ya Wayahudi, naye Yesu akapanda kwenda Yerusalemu.
2 Kolyo Yerusalemu pabile ni birika pa'nnyango wa ngondolo, lyabile likemelwa kwa lugha ya Baebrania Bethzatha, nalo lyabile ni matao matano.
Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, palikuwa na bwawa moja lililoitwa kwa Kiebrania Bethzatha, ambalo lilikuwa limezungukwa na kumbi tano.
3 Idadi ngolo ya atamwe babile, ipofu, iwete, au babile batipooza babile bagonjite mu'matao ago. (Uzingatie: Maneno ga mstari wa 3 kabaonekana kwaa mu'nakala inoite ya kale. “Batikugasubiri mase kutibuliwa.”)
Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani, vipofu, viwete, na waliopooza [wakingojea maji yatibuliwe.
4 Kwa hakika muda fulani malaika auluka nkati ya Ngwana ni kuyatibua mase. Kwa nyoo. yolo ywabile wa kwanza kujingya nkati yake baada ya mase kutibuliwa apangilwe nkoti bokana na chochote chabile kintabile kwa muda woo.
Kwa maana malaika alikuwa akishuka wakati fulani, akayatibua maji. Yule aliyekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao].
5 Ni mundu yumo ywabile ntamwe kwa miaka thelathini na minane abile nkati ya matao.
Mtu mmoja alikuwako huko ambaye alikuwa ameugua kwa miaka thelathini na minane.
6 Yesu paamweni agonjike nkati ya matao ni baada ya kutanga kuwa agonjike kwa muda mrefu Yesu kammakiya, “Je wapala kuwa nkoto.”
Yesu alipomwona akiwa amelala hapo, naye akijua kuwa amekuwa hapo kwa muda mrefu, akamwambia, “Je, wataka kuponywa?”
7 Yolo ntamwe kannyangwa, “Ngwana nabile kwaa na mundu, wa kunibeka mu'birika muda yabile yatitibulilwa. Muda kabanijaribu jingya mundu ywenge atikuntangulia.”
Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana, mimi sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Nami ninapotaka kutumbukia bwawani, mtu mwingine huingia kabla yangu.”
8 Yesu aamkiye, “Uluka ulipotwe litandiko lyako na uyende.”
Yesu akamwambia, “Inuka! Chukua mkeka wako na uende.”
9 Mara yolo mundu aponywile, alitweti kindanda sake no yenda. Lelo labibe lisoba lya sabato.
Mara yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea. Basi siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato.
10 Nga Ayahudi bammakiuye, yolo mundu ywaponywile, “leno ni lisoba lya sabato, ni halalli kwaa kupotwa litandiko lyako.”
Kwa hiyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni Sabato, si halali wewe kubeba mkeka wako.”
11 Kayangwa, ywembe ywaniponyile animakiye, “Tola litandiko lyako no uyende.”
Yeye akawajibu, “Yule mtu aliyeniponya aliniambia, ‘Chukua mkeka wako na uende.’”
12 Kabanlaluya, “Nyai ywakumakiye,'tola litandiko lyako no uyende.”
Wakamuuliza, “Ni mtu gani huyo aliyekuambia uchukue mkeka wako uende?”
13 Ingawa, yolo ywaponywile antangite kwaa mana Yesu aboi kwa siri. Kwa mana pabile ni bandu banyansima.
Basi yule mtu aliyeponywa hakufahamu ni nani aliyemponya, kwa sababu Yesu alikuwa amejiondoa katika ule umati wa watu uliokuwa hapo.
14 Baada ya ago Yesu amkolile yolo mundu mu'lihekalu ni kummakiya, “Linga upangite nkoto! kana upange sambi kae kana likupate likowe libaya muno.”
Baadaye Yesu akamkuta yule mtu aliyemponya ndani ya Hekalu na kumwambia, “Tazama umeponywa, usitende dhambi tena. La sivyo, lisije likakupata jambo baya zaidi.”
15 Mundu yolo kayenda ni kuamakiya Ayahudi kuwa Yesu nga amponyile.
Yule mtu akaenda, akawaambia wale Wayahudi kuwa ni Yesu aliyemponya.
16 Kwa mwanja wa makowe ago Ayahudi bantesike Yesu, kwa mana apangite makowe aga lisoba lya sabato.
Kwa hiyo Wayahudi wakaanza kumsumbua Yesu, kwa sababu alikuwa anafanya mambo kama hayo siku ya Sabato.
17 Yesu kaamakiya, “Tate bango apanga kazi nambeambea ni nenga napanga kazi.”
Yesu akawajibu, “Baba yangu anafanya kazi yake daima hata siku hii ya leo, nami pia ninafanya kazi.”
18 Kwa sababu yee Ayahudi kabampala muno ili kumulaga yapanga kwaa kae atekwile Sabato, ila kwa kunkema Nnongo Tate bake, kuipanga abile sawa ni Nnongo.
Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate jinsi ya kumuua, kwani si kwamba alivunja Sabato tu, bali alikuwa akimwita Mungu Baba yake, hivyo kujifanya sawa na Mungu.
19 Yesu kabayangwa, “Amini, amini, mwana aweza kwaa panga ilebe yeyoti ila chelo amweni Tate bake apangite, kwa mana chochote Tate akipangite nga mwana akipanga.
Yesu akawaambia, “Amin, amin nawaambia, Mwana hawezi kufanya jambo lolote peke yake, yeye aweza tu kufanya lile analomwona Baba yake akifanya, kwa maana lolote afanyalo Baba, Mwana pia hufanya vivyo hivyo.
20 Kwa kuwa Tate ampenda mwana, ni kunlolekeya kila kilebe akipangite ni kunlolekea makowe makolo kuliko aga ili muzidi shangala.
Baba ampenda Mwana na kumwonyesha yale ambayo yeye Baba mwenyewe anayafanya, naye atamwonyesha kazi kuu kuliko hizi ili mpate kushangaa.
21 Kwa kuwa kati Tate atikwafufua bandu mu kiwo ni kuwapea ukoto, nga mwana umpeya yeyote ywampendae.
Hakika kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale anaopenda.
22 Kwa kuwa Tate amuhukumu kwaa yeyote, ila umpeya mwana hukumu yoti
Wala Baba hamhukumu mtu yeyote, lakini hukumu yote amempa Mwana,
23 ili kwamba boti bamweshimu Mwana kati yo panga Mwana atikumweshimu Tate. Ywembe ywamuheshimu kwaa Mwana amuheshimu kwaa ni Tate ywantumite.
ili wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Yeyote asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyemtuma.
24 Amini, amini, ywembe ywaliyowine neno lyango ni kuliaminiya abile ni ukoto wangayomoka ni aukumilwa kwaa. Badala yake, atipeta boka mu'kiwo no jingya mu'ukoto. (aiōnios )
“Amin, amin nawaambia, yeyote anayesikia maneno yangu na kumwamini yeye aliyenituma, anao uzima wa milele, naye hatahukumiwa, bali amepita kutoka mautini, na kuingia uzimani. (aiōnios )
25 Amini, amini, naabakiya muda waisa nambeambe ubile ambapo bandu ba mu'kiwo balowa kuiyowa sauti ya Mwana wa Nnongo, ni boti baiyowine walowa tama.
Amin, amin nawaambia, saa yaja, nayo saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu, nao watakaoisikia watakuwa hai.
26 Kwa mana kati Tate abile ni ukoto nkati yake mwene,
Kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake, vivyo hivyo amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake.
27 pia ampei Mwana kuwa ni ukoto nkati yake, Tate ampei mwana mamlaka ili ahukumu kwa kuwa ni Mwana wa Adamu.
Naye amempa Mwanawe mamlaka ya kuhukumu kwa kuwa yeye ni Mwana wa Adamu.
28 Kana mshangae lelo, kwa mana muda waisa ambao bandu bote baabile mu'makaburi walowa kuliyowa lilobe lyake
“Msishangae kusikia haya, kwa maana saa inakuja ambapo wale walio makaburini wataisikia sauti yake.
29 nabo baboite panja: kwa balo bapangite mema kwa ufufuo wa ukoto, na balo bapangite mabaya kwa ufufuo wa hukumu.
Nao watatoka nje, wale waliotenda mema watafufuka wapate uzima na wale waliotenda maovu, watafufuka wahukumiwe.
30 Naweza kwaa kupanga chochote boka kwango mwene. Kati niyowine, nga nalowa kuhukumu na hukumu yango ni ya haki kwa mana nipalike kwaa mapenzi yango, ila mapenzi yake ywanitumile.
“Mimi siwezi kufanya jambo lolote peke yangu. Ninavyosikia ndivyo ninavyohukumu, nayo hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti kufanya mapenzi yangu mwenyewe, bali mapenzi yake yeye aliyenituma.
31 Kati ya panga nishuhudia mwene, ushuhuda wango wabile kwaa wa kweli.
“Kama ningejishuhudia mimi mwenyewe, ushuhuda wangu si kweli.
32 Kwabile ni ywenge ywanishuhudia nenga na nitangite kwa hakika kuwa ushuhuda waaushudie ni wa kweli.
Lakini yuko mwingine anishuhudiaye na ninajua kwamba ushuhuda wake ni wa kweli.
33 Mumtumile kwa Yohana ni ywembe atikwashuhudia kweli.
“Mlituma wajumbe kwa Yohana, naye akashuhudia juu ya kweli.
34 Hata nyoo, ushuhuda waniupokeile uboka kwaa ka mundu. Niabaya aga ili muweze kulopolelwa.
Si kwamba naukubali ushuhuda wa mwanadamu, la, bali ninalitaja hili kusudi ninyi mpate kuokolewa.
35 Yohana abile taa yaiyaka na ng'ara, na mwabile tayari kuipuraia kwa muda nkolo bweya yake.
Yohana alikuwa taa iliyowaka na kutoa nuru, nanyi kwa muda mlichagua kuifurahia nuru yake.
36 Ushuhuda wanibile nao ni nkolo kuliko wolo wa Yohana kwa kasi ambazo Tate anipei kuikamilisha, izo kazi nizipangite kwa ushuhuda kuwa Tate anitumile.
“Lakini ninao ushuhuda mkuu zaidi kuliko wa Yohana. Kazi zile nizifanyazo, zinashuhudia juu yangu, zile ambazo Baba amenituma nizikamilishe, naam, ishara hizi ninazofanya, zinashuhudia kuwa Baba ndiye alinituma.
37 Tate ywanitumile ywembe mwene atikwashuhudia kuhusu nenga. Muyowine kwaa lilobe lyake wala kubonekeya liumbo lyake wakati wowote.
Naye Baba mwenyewe ameshuhudia juu yangu. Hamjapata kamwe kuisikia sauti yake wala kuona umbo lake,
38 Ntopo neno lyake nkati yinu kwa mana mumwaminiye kwaa ywembe ywanitumile.
wala hamna neno lake ndani yenu, kwa sababu hamkumwamini yeye aliyetumwa naye.
39 Mugachunguza maandiko mkidhani mwabile ni ukoto wangeyomoka nkati yake, na maandiko ago yaashuhudia habari yango na (aiōnios )
Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele, maandiko haya ndiyo yanayonishuhudia Mimi. (aiōnios )
40 mukani kuisa kwango ili mpate ukoto wangeyomoka.
Lakini mnakataa kuja kwangu ili mpate uzima.
41 Nenga nipokya kwaa sifa boka kwa bandu.
“Mimi sitafuti kutukuzwa na wanadamu.
42 Lakini nitangite kuwa ntopo upendo wa Nnongo yinu mwenga mwabene.
Lakini ninajua kwamba hamna upendo wa Mungu mioyoni mwenu.
43 Nenga niisile kwa lina lya Tate bango, muweza kwaa kunipokya. Kati ywenge aisa kwa lina lyake mwalowa kumpokya.
Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei, lakini mtu mwingine akija kwa jina lake mwenyewe, mtampokea.
44 Je muweza kwaa kuamini mwenga ambao mpala kwaa sifa iboka kwa Nnongo wa pekee?
Ninyi mwawezaje kuamini ikiwa mnapeana utukufu ninyi kwa ninyi, lakini hamna bidii kupata utukufu utokao kwa Mungu?
45 Kana muwaze nenga nitabashitaki nnonge ya Tate. Ywaabashitakiya mwenga ni Musa, ambaye mwenga mubekite matumaini yinu kwake.
“Lakini msidhani kuwa mimi nitawashtaki mbele za Baba, mshtaki wenu ni Mose, ambaye mmemwekea tumaini lenu.
46 Kati mwatikumwamini Musa, mwalowa kuniamini nenga kwa kuwa ywembe aandikile habari zangu nenga.
Kama mngelimwamini Mose, mngeliniamini na mimi kwa maana aliandika habari zangu.
47 Muyaamini kwaa maandiko gake, mwaweza kwaa kugaamini maneno yango?
Lakini ikiwa hamwamini aliyoandika Mose, mtaaminije ninayoyasema?”