< Lucam 17 >

1 et ad discipulos suos ait inpossibile est ut non veniant scandala vae autem illi per quem veniunt
Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha.
2 utilius est illi si lapis molaris inponatur circa collum eius et proiciatur in mare quam ut scandalizet unum de pusillis istis
Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa.
3 adtendite vobis si peccaverit frater tuus increpa illum et si paenitentiam egerit dimitte illi
Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, mwonye; akitubu, msamehe.
4 et si septies in die peccaverit in te et septies in die conversus fuerit ad te dicens paenitet me dimitte illi
Na kama akikukosea mara saba kwa siku, na kila mara akarudi kwako akisema Nimetubu, lazima umsamehe.”
5 et dixerunt apostoli Domino adauge nobis fidem
Mitume wakamwambia Bwana, “Utuongezee imani.”
6 dixit autem Dominus si haberetis fidem sicut granum sinapis diceretis huic arbori moro eradicare et transplantare in mare et oboediret vobis
Naye Bwana akajibu, “Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: Ng'oka ukajipandikize baharini, nao ungewatii.
7 quis autem vestrum habens servum arantem aut pascentem qui regresso de agro dicet illi statim transi recumbe
“Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia: Haraka, njoo ule chakula?
8 et non dicet ei para quod cenem et praecinge te et ministra mihi donec manducem et bibam et post haec tu manducabis et bibes
La! Atamwambia: Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na unywe.
9 numquid gratiam habet servo illi quia fecit quae sibi imperaverat non puto
Je utamshukuru huyo mtumishi kwa sababu ametimiza aliyoamriwa?
10 sic et vos cum feceritis omnia quae praecepta sunt vobis dicite servi inutiles sumus quod debuimus facere fecimus
Hali kadhalika na ninyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya.”
11 et factum est dum iret in Hierusalem transiebat per mediam Samariam et Galilaeam
Yesu akiwa safarini kwenda Yerusalemu alipitia mipakani mwa Samaria na Galilaya.
12 et cum ingrederetur quoddam castellum occurrerunt ei decem viri leprosi qui steterunt a longe
Alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenye ukoma walikutana naye, wakasimama kwa mbali.
13 et levaverunt vocem dicentes Iesu praeceptor miserere nostri
Wakapaza sauti wakisema, “Yesu Mwalimu, tuonee huruma!”
14 quos ut vidit dixit ite ostendite vos sacerdotibus et factum est dum irent mundati sunt
Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Basi, ikawa walipokuwa wanakwenda, wakatakasika.
15 unus autem ex illis ut vidit quia mundatus est regressus est cum magna voce magnificans Deum
Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kubwa.
16 et cecidit in faciem ante pedes eius gratias agens et hic erat Samaritanus
Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria.
17 respondens autem Iesus dixit nonne decem mundati sunt et novem ubi sunt
Hapo Yesu akasema, “Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi?
18 non est inventus qui rediret et daret gloriam Deo nisi hic alienigena
Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?”
19 et ait illi surge vade quia fides tua te salvum fecit
Halafu akamwambia huyo mtu, “Simama, uende zako; imani yako imekuponya.”
20 interrogatus autem a Pharisaeis quando venit regnum Dei respondit eis et dixit non venit regnum Dei cum observatione
Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, “Ufalme wa Mungu utakuja lini?” Naye akawajibu, “Ufalme wa Mungu hauji kwa namna itakayoweza kuonekana.
21 neque dicent ecce hic aut ecce illic ecce enim regnum Dei intra vos est
Wala hakuna atakayeweza kusema, Uko hapa, au Uko pale. Kwa kweli Ufalme wa Mungu uko kati yenu.”
22 et ait ad discipulos venient dies quando desideretis videre unum diem Filii hominis et non videbitis
Halafu akawaambia wanafunzi wake, “Siku zinakuja ambapo mtatamani kuona mojawapo ya siku za Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona.
23 et dicent vobis ecce hic ecce illic nolite ire neque sectemini
Na watu watawaambieni: Tazameni yuko hapa; ninyi msitoke wala msiwafuate.
24 nam sicut fulgur coruscans de sub caelo in ea quae sub caelo sunt fulget ita erit Filius hominis in die sua
Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku yake.
25 primum autem oportet illum multa pati et reprobari a generatione hac
Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na kukataliwa na kizazi hiki.
26 et sicut factum est in diebus Noe ita erit et in diebus Filii hominis
Kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Mtu.
27 edebant et bibebant uxores ducebant et dabantur ad nuptias usque in diem qua intravit Noe in arcam et venit diluvium et perdidit omnes
Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka wakati ule Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote.
28 similiter sicut factum est in diebus Loth edebant et bibebant emebant et vendebant plantabant aedificabant
Itakuwa kama ilivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendelea kula na kunywa, kununua na kuuza, kupanda mbegu na kujenga.
29 qua die autem exiit Loth a Sodomis pluit ignem et sulphur de caelo et omnes perdidit
Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, moto na kiberiti vikanyesha kama mvua kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote.
30 secundum haec erit qua die Filius hominis revelabitur
Ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa.
31 in illa hora qui fuerit in tecto et vasa eius in domo ne descendat tollere illa et qui in agro similiter non redeat retro
“Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke nyumbani kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma.
32 memores estote uxoris Loth
Kumbukeni yaliyompata mke wa Loti.
33 quicumque quaesierit animam suam salvare perdet illam et qui perdiderit illam vivificabit eam
Yeyote anayetaka kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na yeyote anayeipoteza, ataiokoa.
34 dico vobis illa nocte erunt duo in lecto uno unus adsumetur et alter relinquetur
Nawaambieni, siku ile usiku watu wawili watakuwa wanalala pamoja, mmoja atachukuliwa na yule mwingine ataachwa.
35 duae erunt molentes in unum una adsumetur et altera relinquetur duo in agro unus adsumetur et alter relinquetur
Wanawake wawili watakuwa wakisaga nafaka pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.”
36 respondentes dicunt illi ubi Domine
Watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.
37 qui dixit eis ubicumque fuerit corpus illuc congregabuntur aquilae
Hapo wakamwuliza, “Ni wapi Bwana?” Naye akawaambia, “Ulipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia.”

< Lucam 17 >