< I Paralipomenon 1 >
2 Cainan, Malaleel, Iared,
Kenani, Mahalaleli, Yaredi,
3 Henoch, Mathusale, Lamech,
Henoko, Methusela, Lameki.
4 Noe, Sem, Cham, et Iaptheth.
Wana wa Nuhu walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi.
5 Filii Iapheth: Gomer, et Magog, et Madai, et Iavan, Thubal, Mosoch, Thiras.
Wana wa Yafethi walikuwa ni Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki, na Tirasi.
6 Porro filii Gomer: Ascenez, et Riphath, et Thogorma.
Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama.
7 Filii autem Iavan: Elisa et Tharsis, Cethim et Dodanim.
Wana wa Yavani walikuwa ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
8 Filii Cham: Chus, et Mesraim, et Phut, et Chanaan.
Wana wa Hamu walikuwa ni Kushi, Misri, Putu, na Kanaani.
9 Filii autem Chus: Saba, et Hevila, Sabatha, et Regma, et Sabathacha. Porro filii Regma: Saba, et Dadan.
Wana wa Kushi walikuwa ni Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa ni Sheba na Dedani.
10 Chus autem genuit Nemrod: iste coepit esse potens in terra.
Kushi akawa baba wa Nimrodi, aliyekuwa shujaa wa Kwanza katika dunia.
11 Mesraim vero genuit Ludim, et Anamim, et Laabim, et Nephtuim,
Misri akawa babu wa Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
12 Phetrusim quoque, et Casluim: de quibus egressi sunt Philisthiim, et Caphtorim.
Wapathrusi, Wakasluhi (Wafilisti walipotoka), na Wakaftori.
13 Chanaan vero genuit Sidonem primogenitum suum, Hethaeum quoque,
Kanaani akawa baba wa Sidoni, mwanae wa kwanza, na wa Hethi.
14 et Iebusaeum, et Amorrhaeum, et Gergesaeum,
Pia akawa babu wa Myebusi, Mwamori, Mgirgashi,
15 Hevaeumque et Aracaeum, et Sinaeum.
Mhivi, Mwarki, Msini,
16 Aradium quoque, et Samaraeum, et Hamathaeum.
Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi.
17 Filii Sem: Aelam, et Assur, et Arphaxad, et Lud, et Aram, et Hus, et Hul, et Gether, et Mosoch.
Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri, na Mashi.
18 Arphaxad autem genuit Sale, qui et ipse genuit Heber.
Arfaksadi akawa baba wa Sala, na Sala akawa baba wa Eberi.
19 Porro Heber nati sunt duo filii, nomen uni Phaleg, quia in diebus eius divisa est terra; et nomen fratris eius Iectan.
Eberi alikuwa na wana wawili wa kiume. Jina la wa kwanza lilikuwa Pelegi, kwa kuwa katika siku zake dunia ilikuwa imegawanyika. Jina la kaka yake lilikuwa Yoktani.
20 Iectan autem genuit Elmodad, et Saleph, et Asarmoth, et Iare,
Yoktani akawa baba wa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
21 Adoram quoque, et Huzal, et Decla,
Hadoramu, Uzali, Dikla,
22 Hebal etiam, et Abimael, et Saba, necnon
Obali, Abimaeli, Sheba,
23 et Ophir, et Hevila, et Iobab. omnes isti filii Iectan:
Ofiri, Havila, na Yobabu; wote hawa walikuwa uzao wa Yoktani.
27 Abram, iste est Abraham.
Abramu, aliye kuwa Ibrahimu.
28 Filii autem Abraham, Isaac et Ismahel.
Wana wa Ibrahimu walikuwa Isaka na Ishmaeli.
29 Et hae generationes eorum. Primogenitus Ismahelis, Nabaioth, et Cedar, et Adbeel, et Mabsam,
Hawa ndio wanao: mzaliwa wa kwanza alikuwa ni Nebayothi, kisha Kedari, Abdeeli, Mibsamu,
30 et Masma, et Duma, Massa, Hadad, et Thema,
Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema,
31 Iachur, Naphis, Cedma. hi sunt filii Ismahelis.
Yeturi, Nafishi, na Kedama. Hawa ndio wana wa Ishamaeli.
32 Filii autem Ceturae concubinae Abraham, quos genuit: Zamran, Iecsan, Madan, Madian, Iesboc, et Sue. Porro filii Iecsan: Saba, et Dadan. Filii autem Dadan: Assurim, et Latussim, et Laomim.
Wana wa Ketura, suria wa Ibrahimu, walikuwa Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani.
33 Filii autem Madian: Epha, et Epher, et Henoch, et Abida, et Eldaa. omnes hi, filii Ceturae.
Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Wote hawa walikuwa uzaowa Ketura.
34 Genuit autem Abraham Isaac: cuius fuerunt filii Esau, et Israel.
Ibrahimu akawa baba wa Isaka. Wana wa Isaka walikuwa Esau na Israeli.
35 Filii Esau: Eliphaz, Rahuel, Iehus, Ihelom, et Core.
Wana wa Esau walikuwa ni Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu, na Kora.
36 Filii Eliphaz: Theman, Omar, Sephi, Gathan, Cenez, Thamna, Amalec.
Wana wa Elifazi walikuwa ni Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna, na Amaleki.
37 Filii Rahuel: Nahath, Zara, Samma, Meza.
Wana wa Reueli walikuwa ni Nahathi, Zera, Shama, na Miza.
38 Filii Seir: Lotan, Sobal, Sebeon, Ava, Dison, Eser, Disan.
Wana wa Seiri walikuwa ni Lotani, Shobali, Sebioni, Ana, Dishoni, Eseri, na Dishani.
39 Filii Lotan: Hori, Homam. Soror autem Lotan fuit Thamna.
Wana wa Lotani walikuwa ni Hori na Hemamu, na Timna alikuwa dada yake Lotani.
40 Filii Sobal: Alian, et Manahath, et Ebal, Sephi et Onam. Filii Sebeon: Aia et Ana. Filii Ana: Dison.
Wana wa Shobali walikuwa ni Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu. Wana wa Sebeoni walikuwa ni Aya na Ana.
41 Filii Dison: Hamran, et Eseban et Iethran, et Charan.
Mwana wa Ana alikuwa ni Dishoni. Wana wa Dishoni walikuwa Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani.
42 Filii Eser: Balaan, et Zavan, et Iacan. Filii Disan: Hus et Aran.
Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani walikuwa Usi na Arani.
43 Isti sunt reges, qui imperaverunt in Terra Edom antequam esset rex super filios Israel: Bale filius Beor: et nomen civitatis eius, Denaba.
Hawa ndio wafalme walio tawala katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kuwatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori; na jina la mji wake ulikuwa Dinhaba.
44 Mortuus est autem Bale, et regnavit pro eo Iobab filius Zare de Bosra.
Bela alipo kufa, Yohabu mwana wa Zera wa Bosra akatawala badala yake.
45 Cumque et Iobab fuisset mortuus, regnavit pro eo Husam de Terra Themanorum.
Yohabu alipo kufa, Hushamu wa nchi ya Watemani akatawala badala yake.
46 Obiit quoque et Husam, et regnavit pro eo Adad filius Badad, qui percussit Madian in Terra Moab: et nomen civitatis eius Avith.
Hushamu alipo kufa, Hadadi mwana wa Bedadi, aliye washinda Wamidiani katika uwanja wa Moabu, akatawa badala yake. Jina la mji wake ulikuwa Avithi.
47 Cumque et Adad fuisset mortuus, regnavit pro eo Semla de Masreca.
Hadadi alipo kufa, Samla wa Masreka akatawala badala yake.
48 Sed et Semla mortuus est, et regnavit pro eo Saul de Rohoboth, quae iuxta amnem sita est.
Samla alipo kufa, Shauli wa Rehobothi Hanahari akatawala badala yake.
49 Mortuo quoque Saul, regnavit pro eo Balanan filius Achobor.
Shauli alipo kufa, Baal-Hanani mwana wa Akbori akatawala badala yake.
50 Sed et hic mortuus est, et regnavit pro eo Adad: cuius urbis nomen fuit Phau, et appellata est uxor eius Meetabel filia Matred filiae Mezaab.
Baal-Hanani mwana wa Akbori alipo kufa, Hadari akatawala badala yake. Jina la mji wake ni Pau. Jina la mke wake lilikuwa ni Mehetabeli binti wa Matredi binti wa Mezahabu.
51 Adad autem mortuo, duces pro regibus in Edom esse coeperunt: dux Thamna, dux Alva, dux Ietheth,
Hadadi akafa. Wajumbe wa ukoo wa Edomu walikuwa Timna, Alva, Yethethi,
52 dux Oolibama, dux Ela, dux Phinon,
Oholibama, Ela, Pinoni,
53 dux Cenez, dux Theman, dux Mabsar,
Kenazi, Temani, Mibsari,
54 dux Magdiel, dux Hiram. hi duces Edom.
Magdieli, na Iramu. Hawa ndio walikuwa wajumbe wa ukoo wa Edomu.