< 예레미야 52 >
1 시드기야가 위에 나아갈 때에 나이 이십일 세라 예루살렘에서 십일 년을 치리하니라
Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu. Jina la mamaye lilikuwa Hamutali; alikuwa binti Yeremia wa Libna.
2 시드기야가 여호야김의 모든 행위를 본받아 여호와 보시기에 악을 행한지라
Akafanya maovu machoni pa Yahwe; akafanya kila alichokifanya Yehoyakimu.
3 여호와께서 예루살렘과 유다를 진노하심이 그들을 그 앞에서 쫓아내시기까지 이르렀더라 시드기야가 바벨론 왕을 배반하매
Kwa hasira ya Yahwe, matukio haya yote yalitukia Yerusalemu na Yuda, hata alipowatoa mbele yake mwenyewe. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.
4 시드기야 구년 시월 십일에 바벨론 왕 느부갓네살이 그 모든 군대를 거느리고 예루살렘을 치러 올라와서 그 성을 대하여 진을 치고 사면으로 흉벽을 쌓으매
Ikawa katika mwaka wa tisa wa utawala wa mfalme Sedeki, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alikuja na jeshi lake lote dhidi ya Yerusalem. Wakapiga kambi kuukabili, nao wakajenga ukuta wa kuusuria kuuzunguka.
Hivyo mji ukausuriwa mpaka mwaka wa kumi na moja wa utawala wa mfalme Sedekia.
6 그 사월 구일에 성중에 기근이 심하여 그 땅 백성의 식물이 진하였더라
Katika mwezi wa nne, siku ya tisa ya mwaka huo, njaa ikawa kali sana mjini hata hakukuwa na chakula kwa watu wa nchi.
7 갈대아인이 그 성읍을 에워쌌더니 성벽을 깨뜨리매 모든 군사가 밤 중에 두 성벽 사이 왕의 동산 곁문 길로 도망하여 아라바 길로 가더니
Kisha mji ukatobolewa, na wapiganaji wote wakakimbia nje ya mji wakati wa usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya kuta mbili, kwa bustani ya mfalme, japokuwa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Hivyo wakaenda kwa njia ya Araba.
8 갈대아인의 군대가 시드기야 왕을 쫓아가서 여리고 평지에서 미치매 왕의 모든 군대가 그를 떠나 흩어진지라
Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme na kumpata Sedekia katika tambarare za bonde la Mto Yordani karibu na Yeriko. Jeshi lote lilikuwa limetawanyika mbali naye.
9 그들이 왕을 잡아가지고 하맛 땅 립나에 있는 바벨론 왕에게로 끌고가매 그를 신문하니라
Wakamkamata mfalme na kumleta hadi kwa mfalme wa Babeli huko Ribla katika nchi ya Hamathi, alipotoa hukumu juu yake.
10 바벨론 왕이 시드기야의 아들들을 그의 목전에서 죽이고 또 립나에서 유다의 모든 방백을 죽이며
Mfalme wa Babeli akawachinja wana wa Sedekia mbele ya macho yake, na huko Ribla akawachinja viongozi wote wa Yuda.
11 시드기야의 두 눈을 빼고 사슬로 결박하여 바벨론으로 끌어다가 그 죽는 날까지 옥에 두었더라
Kisha akayaondoa macho ya Sedekia, akamfunga katika vifungo vya shaba, na kumleta Babeli. Mfalme wa Babeli akamweka kifungoni hata siku ya kufa kwake.
12 바벨론 왕 느부갓네살의 십구년 오월 십일에 바벨론 왕의 어전 시위대 장관 느부사라단이 예루살렘에 이르러
Basi mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, ambao ulikuwa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa mfalme Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani akaja Yerusalemu. Alikuwa jemedari wa walinzi wa mfalme na mtumishi wa mfalme wa Babeli.
13 여호와의 전과 왕궁을 불사르고 예루살렘의 모든 집을 귀인의 집까지 불살랐으며
Akaiteketeza nyumba ya Yahwe, kasiri, na nyumba zote za Yerusalemu; pia kila jengo mhimu mjini alilichoma.
14 시위대 장관을 좇는 갈대아인의 온 군대가 예루살렘 사면 성벽을 헐었으며
Kama kwa kuta za kuuzunguka Yerusalemu, jeshi lote la Wababeli lililokuwa pamoja na jemedari wa mlinzi wakaviaribu.
15 시위대 장관 느부사라단이 백성 중 빈한한 자와 성중에 남아있는 백성과 바벨론 왕에게 항복한 자와 무리의 남은 자를 사로잡아 옮겨가고
Kama kwa watu maskini sana, watu waliosalia walioachwa katika mji, waliokuwa wamemwendea mfalme wa Babeli, na baadhi ya watu wenye ujuzi - Nebuzaradan, jemedari wa askari walinzi, akawachukua baadhi yao uhamishoni.
16 비천한 국민을 남겨두어 포도원을 다스리는 자와 농부가 되게 하였더라
Lakini Nebuzaradani, jemedari wa mlinzi, akawaacha baadhi ya maskini sana wa nchi kuitunza mizabibu na mashamba.
17 갈대아인이 또 여호와의 전의 두 놋기둥과 받침들과 여호와의 전의 놋바다를 깨뜨려 그 놋을 바벨론으로 가져갔고
Lakini kwa nguzo za shaba lilizokuwa katika nyumba ya Yahwe, mishikio na bahari ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya Yahwe, Wakaldayo wakaivunja vipande wakaondoka navyo kurudi Babeli.
18 또 가마들과 부삽들과 불집게들과 주발들과 숟가락들과 섬길 때에 쓰는 모든 놋그릇을 다 가져 갔으며
Vyungu, makoleo, kinara cha taa, mabakuri, na vitu vyote vya shaba ambavyo makuhani walikuwa wakivitumia hekaluni - Wakaldayo wakavichukua vyote.
19 시위대 장관이 또 잔들과 화로들과 주발들과 솥들과 촛대들과 숟가락들과 바리들 곧 금물의 금과 은물의 은을 가져갔는데
Makalai na chetezo cha uvumba, mabakuri, vyungu, kinara cha taa, vikaango, makalai zilizotengenezwa kwa dhahabu, na zilizotengenezwa kwa dhahabu - kapteni wa mlinzi wa mfalme akazichukua pia.
20 솔로몬 왕이 여호와의 전을 위하여 만든 두 기둥과 한 바다와 그 받침 아래 있는 열두 놋소 곧 이 모든 기구의 놋 중수를 헤아릴 수 없었더라
Nguzo mbili, bahari, na ng'ombe kumi na wawili wa shaba waliokuwa chini yake, vitu Selemani alivyokuwa amevifanya kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vikiwa na shaba nyingi sana isiyoweza kupimwa.
21 그 기둥은 한 기둥의 고가 십팔 규빗이요 그 주위는 십이 규빗이며 그 속이 비었고 그 두께는 사지놓이며
Nguzo zilikuwa na urefu wa dhiraha kumi na nane kila moja, na mstari kuzunguka kila moja wenye urefu wa dhiraha kumi na mbili. Kila moja ilikuwa na unene wa vidole vinne na tundu.
22 기둥 위에 놋머리가 있어 그 고가 다섯 규빗이요 머리 사면으로 돌아가며 꾸민 그물과 석류가 다 놋이며 또 다른 기둥에도 이런 모든 것과 석류가 있었으며
Kichwa cha shaba kilikuwa juu yake. Kichwa kilikuwa dhiraha tano urefu wake, kazi ya waya zinazokingamana na makomamanga kukizunguka. Chote kilitengenezwa kwa shaba. Na nguzo nyingine ilikuwa na makomamanga yake vilikuwa kama ya kwanza.
23 그 사면에 있는 석류는 구십륙이요 그 기둥에 둘린 그물 위에 있는 석류는 도합이 일백이었더라
Hivyo kulikuwa na makomamanga tisini na sita ubavuni mwa kila kichwa, na makomamanga mia moja juu ya nyaya zilizokingamana kukizunguka.
24 시위대 장관이 대제사장 스라야와 부제사장 스바냐와 전 문지기 세 사람을 잡고
Jemedari wa mlinzi akamchukua Seraya mfungwa, kuhani mkuu, pamoja na Sefania, kuhani wa pili, na wale mabawaba watatu.
25 또 성중에서 사람을 잡았으니 곧 군사를 거느린 장관 하나와 또 성중에서 만난 바 왕의 시종 칠 인과 국민을 초모하는 군대장관의 서기관 하나와 성중에서 만난 바 국민 육십 명이라
Kutoka mjini akamchukua mfungwa afsa aliyekuwa juu ya askari, na watu saba wa wale waliomshauri mfalme, waliokuwa wamesalia mjini. Akamchukua mfungwa afsa wa jeshi la mfalme aliyekuwa na wajibu wa kuwaingiza watu katika jeshi, pamoja na watu mashuhuri sitini kutoka katika nchi waliokuwamo mjini.
26 시위대 장관 느부사라단이 그들을 잡아가지고 립나 바벨론 왕에게 나아가매
Kisha Nebuzaradani, jemedari wa mlinzi, akawachukuwa na kuwaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla.
27 바벨론 왕이 하맛 땅 립나에서 다 쳐죽였더라 이와 같이 유다가 사로잡혀 본토에서 떠났더라
Mfalme wa Babeli akawaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Kwa njia hii, Yuda akaondoka katika nchi yake na kwenda uhamishoni.
28 느부갓네살의 사로잡아 옮긴 백성이 이러하니라 제칠년에 유다인이 삼천이십삼이요
Hawa walikuwa watu Nebukadneza aliwaamisha: katika mwaka wa saba, Wayudea 3, 023.
29 느부갓네살의 십팔년에 예루살렘에서 사로잡아 옮긴 자가 팔백삼십이 인이요
Katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadneza alichukuwa 832 kutoka Yerusalemu.
30 느부갓네살의 이십삼년에 시위대 장관 느부사라단이 사로잡아 옮긴 유다인이 칠백사십오 인이니 그 총수가 사천육백 인이었더라
Katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadneza, Nebuzaradani, jemedari wa walinzi wa mfalme, aliwahamisha Wayudea 745. Jumla ya watu walioamishwa walikuwa 4, 600.
31 유다 왕 여호야긴이 사로잡혀간지 삼십칠년 곧 바렙론 왕 에윌므로닥의 즉위 원년 십이월 이십오일에 그가 유다 왕 여호야긴을 옥에서 내어놓아 그 머리를 들게 하고
Ikawa baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa kufungwa kwake Yohoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evili Merodaki, mfalme wa Babeli akamfungua Yehoyakini mfalme wa Yuda kutoka kifungoni. Ilikuwa mwaka ambao Evili Merodaki alianza kutawala.
32 그에게 선히 말하고 그의 위를 그와 함께 바벨론에 있는 왕들의 위보다 높이고
Akaongea naye kwa upole na akampa kiti cha heshima kuliko cha wafalme wengine aliokuwa pamoja nao huko Babeli.
33 그 죄수의 의복을 바꾸게 하고 그 일평생에 항상 왕의 앞에서 먹게 하였으며
Evili Merodaki akaondoa mavazi ya gerezani ya Yehoyakini, na Yehoyakini akala chakula cha daima katika meza ya mfalme siku zote zilizosalia za maisha yake.
34 그의 쓸 것은 날마다 바벨론 왕에게서 받는 정수가 있어서 죽는 날까지 곧 종신토록 끊이지 아니하였더라
Na alipewa posho ya chakula cha kila siku kwa maisha yake yote yaliyosalia mpaka siku ya kufa kwake.