< 시편 118 >
1 여호와께 감사하라! 저는 선하시며 그 인자하심이 영원함이로다
Mshukuruni Yahwe, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.
2 이제 이스라엘은 말하기를 그 인자하심이 영원하다 할지로다
Israeli na aseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.”
3 이제 아론의 집은 말하기를 그 인자하심이 영원하다 할지로다
Nyumba ya Haruni na iseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.”
4 이제 여호와를 경외하는 자는 말하기를 그 인자하심이 영원하다 할지로다
Wafuasi waaminifu wa Yahwe na waseme, “Uaminifu wa agano lake wadumu milele.”
5 내가 고통 중에 여호와께 부르짖었더니 여호와께서 답하시고 나를 광활한 곳에 세우셨도다
Katika dhiki yangu nilimuita Yahwe; Yahwe alinijibu na kuniweka huru.
6 여호와는 내 편이시라 내게 두려움이 없나니 내게 어찌할꼬
Yahwe yuko pamoja nami; sitaogopa; mwanadamu atanifanya nini? Yahwe yuko upande wangu kama msaidizi;
7 여호와께서 내 편이 되사 나를 돕는 자 중에 계시니 그러므로 나를 미워하는 자에게 보응하시는 것을 내가 보리로다
nitawatazama kwa ushindi wale walio nichukia.
Ni bora kuwa na makazi katika Yahwe kuliko kumtumainia mwanadamu.
9 여호와께 피함이 방백들을 신뢰함보다 낫도다
Ni bora kukimbilia katika Yahwe kuliko kuamini katika wakuu.
Mataifa yote walinizunguka; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
Walinizunguka; naam, walinizunguka; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
Walinizunguka kama nyuki; walitoweka haraka kama moto kati ya miiba; kwa jina la Yahwe niliwakatilia mbali.
Walinishambulia ili waniangushe, lakini Yahwe alinisaidia.
Yahwe ni nguvu yangu na furaha yangu, na ndiye anaye niokoa.
Kelele za ushindi zimesikika katika maskani ya wenye haki; mkono wa kuume wa Mungu umeshinda.
Mkono wa kuume wa Mungu umetukuka; mkono wa kuume wa Yahwe umeshinda.
Sitakufa, bali nitaishi na kuyatangaza matendo ya Yahwe.
Yahwe ameniadhibu vikali; lakini hajaruhusu nife.
Unifungulie milango ya haki; nitaingia na nitamshukuru Yahwe.
Hili ni lango la Yahwe; wenye haki hupitia kwalo.
Nitakushukuru wewe, kwa kuwa ulinijibu, na umekuwa wokovu wangu.
Jiwe ambalo wajenzi walilikataa wajenzi limekuwa msingi.
Yahwe ndiye afanyaye hili; ni la ajabu machoni petu.
Hii ni siku ambayo Yahwe ametenda; tutaifurahia na kuishangilia.
Tafadhali, Yahwe, utupe ushindi! Tafadhali, Yahwe, utupe mafanikio!
Amebarikiwa yule ajaye katika jina la Yahwe; tunakubariki kutoka katika nyumba ya Yahwe.
Yahwe ni Mungu, na ametupa sisi nuru; ifungeni dhabihu kwa kamba pembeni mwa madhabahu.
Wewe ni Mungu wangu, nami nitakushukuru; wewe ni Mungu wangu; nitakutukuza wewe.
Oh, mshukuruni Yahwe; kwa kuwa ni mwema; kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.