< 箴言 知恵の泉 9 >

1 智慧はその家を建て その七の柱を砍成し
Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo saba kutoka katika miamba.
2 その畜を宰り その酒を混和せ その筵をそなへ
Ameandaa wanyama wake kwa chakula cha usiku; ameichanganya divai yake; na kuandaa meza yake.
3 その婢女をつかはして邑の高處に呼はりいはしむ
Amewatuma watumishi wake kupeleka mialiko na kutoka mahali pa juu sana kwenye mji anaita:
4 拙者よここに來れと また智慧なき者にいふ
“Wale wasiofunzwa waje hapa!” anawaambia wale wasionaufahamu.
5 汝等きたりて我が糧を食ひ わがまぜあはせたる洒をのみ
Njoo, ule chakula, na unywe divai nimeshaichanganya.
6 拙劣をすてて生命をえ 聡明のみちを行め
Acheni njia zenu za kijinga, na mkaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.
7 嘲笑者をいましむる者は恥を己にえ 惡人を責むる者は疵を己にえん
Yeyote amrekebishaye mwenye dhihaka hukaribisha matusi na yeyote anayemshutumu mtu mbaya atapata madhara.
8 嘲笑者を責むることなかれ 恐くは彼なんぢを惡まん 智慧ある者をせめよ 彼なんぢを愛せん
Usimshutumu mwenye dhihaka, ama atakuchukia; mshutumu mtu mwenye busara, naye atakupenda.
9 智慧ある者に授けよ 彼はますます智慧をえん 義者を教へよ 彼は知識に監まん
Mpe mafundisho mtu mwenye busara, naye atakuwa na busara zaidi; mfundishe mtu mwenye haki, naye ataongeza elimu.
10 ヱホバを畏るることは智慧の根本なり 聖者を知るは聡明なり
Hofu ya Mungu ni chanzo cha hekima na maarifa ya Mtakatifu ni ufahamu.
11 我により汝の日は多くせられ 汝のいのちの年は増べし
Maana kwa njia yangu siku zako zitazidishwa na uzima wako utaongezewa miaka.
12 汝もし智慧あらば自己のために智慧あるなり 汝もし嘲らば汝ひとり之を負ん
Kama unahekima, unahekima kwako mwenyewe, lakini ukidharau, utaibeba peke yako.
13 愚なる婦は嘩しく且つたなくして何事をも知らず
Mwanamke mpumbavu anakelele nyingi- hajafunzwa wala haelewi chochote.
14 その家の門に坐し邑のたかき處にある座にすわり
Anakaa kwenye mlango wa nyumba yake, kwenye kiti cha sehemu ya juu sana ya mji.
15 道をますぐに過る往來の人を招きていふ
Anawaita kwa sauti wanaopita karibu, watu wale wanaotembea wima katika njia zao.
16 拙者よここに來れと また智慧な在りき人にむかひては之にいふ
Wale ambao hamjafunzwa njoni hapa ndani!” anawaambia wale wasio na akili. “
17 竊みたる水は甘く密かに食ふ糧は美味ありと
Maji ya kuiba ni matamu na mkate unaoliwa kwa siri unapendeza.”
18 彼處にある者は死し者その客は陰府のふかき處にあることを是等の人は知らざるなり (Sheol h7585)
Lakini hajui kwamba wafu wapo pale, wageni wake wapo kwenye vina vya kuzimu. (Sheol h7585)

< 箴言 知恵の泉 9 >