< 詩篇 88 >

1 わがすくひの神ヱホバよわれ晝も夜もなんぢの前にさけべり
Wimbo. Zaburi ya wana wa Kora. Kwa mwimbishaji. Mtindo wa mahalathi leanothi. Utenzi wa Hemani Mwezrahi. Ee Bwana, Mungu uniokoaye, nimelia mbele zako usiku na mchana.
2 願くはわが祈をみまへにいたらせ汝のみみをわが號呼のこゑにかたぶけたまへ
Maombi yangu yafike mbele zako, utegee kilio changu sikio lako.
3 わがたましひは患難にてみち我がいのちは陰府にちかづけり (Sheol h7585)
Kwa maana nafsi yangu imejaa taabu, na maisha yangu yanakaribia kaburi. (Sheol h7585)
4 われは穴にいるものとともにかぞへられ依仗なき人のごとくなれり
Nimehesabiwa miongoni mwa wale waendao shimoni, niko kama mtu asiye na nguvu.
5 われ墓のうちなる殺されしもののごとく死者のうちにすてらる汝かれらを再びこころに記たまはず かれらは御手より斷滅されしものなり
Nimetengwa pamoja na wafu, kama waliochinjwa walalao kaburini, ambao huwakumbuki tena, ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako.
6 なんぢ我をいとふかき穴 くらき處 ふかき淵におきたまひき
Umenitupa katika shimo lenye kina kirefu sana, katika vina vya giza nene.
7 なんぢの怒はいたくわれにせまれり なんぢそのもろもろの浪をもて我をくるしめ給へり (セラ)
Ghadhabu yako imekuwa nzito juu yangu, umenigharikisha kwa mawimbi yako yote.
8 わが相識ものを我よりとほざけ我をかれらに憎ませたまへり われは錮閉されていづることあたはず
Umenitenga na rafiki zangu wa karibu na kunifanya chukizo kwao. Nimezuiliwa, wala siwezi kutoroka;
9 わが眼はなやみの故をもておとろへぬ われ日ごとに汝をよべり ヱホバよなんぢに向ひてわが兩手をのべたり
nuru ya macho yangu imefifia kwa ajili ya huzuni. Ee Bwana, ninakuita kila siku, ninakunyooshea wewe mikono yangu.
10 なんぢ死者にくすしき事跡をあらはしたまはんや 亡にしもの立てなんぢを讃たたへんや (セラ)
Je, wewe huwaonyesha wafu maajabu yako? Je, wale waliokufa huinuka na kukusifu?
11 汝のいつくしみは墓のうちに汝のまことは滅亡のなかに宣傳へられんや
Je, upendo wako hutangazwa kaburini, uaminifu wako katika Uharibifu?
12 汝のくすしきみわざは幽暗になんぢの義は忘失のくにに知るることあらんや
Je, maajabu yako hujulikana mahali pa giza, au matendo yako ya haki katika nchi ya usahaulifu?
13 されどヱホバよ我なんぢに向ひてさけべり わがいのりは朝にみまへに達らん
Lakini ninakulilia wewe, Ee Bwana, unisaidie; asubuhi maombi yangu huja mbele zako.
14 ヱホバよなんぢ何なればわが霊魂をすてたまふや何なればわれに面をかくしたまふや
Ee Bwana, kwa nini unanikataa na kunificha uso wako?
15 われ幼稚よりなやみて死るばかりなり我なんぢの恐嚇にあひてくるしみまどへり
Tangu ujana wangu nimeteseka, nikakaribia kifo; nimepatwa na hofu zako, nami nimekata tamaa.
16 汝のはげしき怒わがうへをすぐ汝のおびやかし我をほろぼせり
Ghadhabu yako imepita juu yangu; hofu zako zimeniangamiza.
17 これらの事ひねもす大水のごとく我をめぐり ことごとく來りて我をかこみふさげり
Mchana kutwa zinanizunguka kama mafuriko; zimenimeza kabisa.
18 なんぢ我をいつくしむ者とわが友とをとほざけ わが相識るものを幽暗にいれたまへり
Umeniondolea marafiki na wapendwa wangu; giza limekuwa ndilo rafiki yangu wa karibu kuliko wote.

< 詩篇 88 >