< Katuma 8 >
1 Shawulu ma hem inni wano imemee, ronome a tubi u mensi anu tarsa Asere a nyumo u Jerusalem; an dee sa wa kabi tize ta Asere citi pin tu Judiya nan nu Samariya a meki we a samarka, ana ka dira wani wa dii chass.
Saulo naye alikiona kitendo hicho cha kumwua Stefano kuwa sawa. Siku hiyo kanisa la Yerusalemu lilianza kuteswa vibaya. Waumini wote, isipokuwa tu wale mitume, walilazimika kutawanyika katika sehemu za mashambani za Yudea na Samaria.
2 Anu nya ce sa wa vati Sitivin wa buki tize tiririn ani ce nume.
Watu wamchao Mungu, walimzika Stefano na kumfanyia maombolezo makubwa.
3 Shawulu ma ribe u tarsa uti kura unu mensi anu tarsa Asere unu korsuzo ma nan ni Jessi.
Wakati huohuo, Saulo alijaribu kuliangamiza kanisa. Alikwenda katika kila nyumba, akawatoa nje waumini, wanaume kwa wanawake, akawatia gerezani.
4 Vatin ani me anu kaba uti zeeta Asere me sa Asamirkawe wa ri aje uni boo utini.
Wale waumini waliotawanyika, walikwenda kila mahali wakihubiri ule ujumbe.
5 Filibus ma dusa a nyumo ani pin nu Samariya unu boo uwe abanga ukirsti.
Naye Filipo aliingia katika mji wa Samaria na kumhubiri Kristo kwa wenyeji wa hapo.
6 A nabu gbardang sa wa kunna wa kiri wa iri ti mum sa ma zin unu wuza mee wa gamika muriba muwe mee a hira ame.
Watu walijiunga kusikiliza kwa makini ule ujumbe wa Filipo na kuona ile miujiza aliyoifanya.
7 Ani bee izezen gbardang we e unu karsa u hunu, anu wijo uti hihira wa kem u humza.
Maana pepo wachafu waliokuwa wamewapagaa watu wengi waliwatoka wakipiga kelele kubwa; na pia watu wengi waliokuwa wamepooza viungo na waliolemaa waliponywa.
8 Mu riba manu ani pin mee mu runme.
Kukawa na furaha kubwa katika mji ule.
9 Uye mamu rani ani pinme sa atisa me simon, dee sa ma dodonkinon anu Vengizi uwe muriba ini bere na nu bezi ubari.
Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Simoni ambaye alikuwa amekwisha fanya uchawi wake katika mji huo kwa muda na kuwashangaza watu wa Samaria, akijiona kuwa yeye ni mtu maarufu.
10 ASamariyawa a cincin nan a dandang vat, mu riba mu wemee mu kuri ahira ame, unu gusa unu geme mazin ni kara na Asere sa ri ori.
Watu wote, wadogo na wakubwa, walimsikiliza kwa makini wakisema, “Simoni ndiye ile nguvu ya kimungu inayoitwa Nguvu Kubwa.”
11 Wa re aje unu kunna umee barki sa ma dodonkino unu wuza uwe ribere.
Walivutiwa sana naye kwa vile alikuwa amewashangaza kwa uchawi wake kwa muda mrefu.
12 Sa wa hem inka dura ku runtame sa Filibus ma hanawen, ka banga a kura Asere nan Yesu kirsti, a zursowe ana ruma nan na eh.
Lakini walipouamini ujumbe wa Filipo juu ya Habari Njema ya Ufalme wa Mungu na jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanawake na wanaume.
13 Simon me changi ma hem inka durame a zorome, ma dusa more aje inti cuku na Filibus ma ira timum gbardang sa ma wuza ma kunna biyau.
Hata Simoni aliamini; baada ya kubatizwa ilikuwa akiandamana na Filipo, akastaajabia maajabu na miujiza iliyokuwa inafanyika.
14 A dura me sa warani Ujerusalem wa kuma agi anu samariya wa kaba tize ta Asere, wa tuburko Bitrus nan Yohana.
Wale mitume waliokuwa kule Yerusalemu walipopata habari kwamba wenyeji wa Samaria nao wamelipokea neno la Mungu, waliwatuma kwao Petro na Yohane.
15 Sa wa hana wa hana wa wuwe biringara bati wa kabi bibee biririn.
Walipofika waliwaombea hao waumini ili wampokee Roho Mtakatifu;
16 A zorsowe a nyumo ani zaa nu gomo Asere Yesu vati anime daki wa kem bibee biririn.
maana wakati huo Roho Mtakatifu hakuwa ameshukia yeyote kati yao; walikuwa wamebatizwa tu kwa jina la Bwana Yesu.
17 U aye u Bitrus nan Yohana wa tarsawe tari ace waduku kem.
Basi, Petro na Yohane wakawawekea mikono hao waumini, nao wakampokea Roho Mtakatifu.
18 Sa simon ma ira azin unu ninza ubibee biririn una utarsa utari ace ma witiwe ikirfi.
Hapo Simoni aling'amua kwamba kwa kuwekewa mikono ya mitume waumini walipewa Roho Mtakatifu. Hivyo aliwapa Petro na Yohane fedha akisema,
19 Ma gunwe nyanime ni ge nikaramee vat dee sa ma tarame tara anice makem bibee biririn.
“Nipeni na mimi uwezo huo ili yeyote nitakayemwekea mikono, apokee Roho Mtakatifu.”
20 Bitrus ma gunmee cornowe nan ikirfi iwemee, u basa uda kee ukpee u nyanki wa Asere ini kirfi.
Lakini Petro akamjibu, “Potelea mbali na fedha zako kwa vile unafikiri kwamba unaweza kununua karama ya Mungu kwa fedha!
21 Iriba ya Asere izoo na huu, barki anime udaa kemwe baa.
Huna sehemu yoyote wala haki katika kazi hiyo kwa maana moyo wako hauko sawa mbele ya macho ya Mungu.
22 Barki anime ceki imum iburri iweme uwu biringara bati Asere a kpeeciwe.
Kwa hiyo, tubu ubaya wako huu na umwombe Bwana naye anaweza kukusamehe fikira kama hizo.
23 Ma ira uraa anyumo ati kono tigwangwang tucharan.
Ni dhahiri kwangu kwamba umejaa wivu mkali na mfungwa wa dhambi!”
24 Sion ma gu ringirkanme Asere kati timumme sa ya buka tikem.
Simoni akajibu, “Tafadhali, niombeeni kwa Bwana lisije likanipata lolote kati ya hayo mliyosema.”
25 Sa Bitrus nan Yohana wa mara uboo anu tizee tu Ugomo asere, wa kuri u hana Ujerusalem wa haki wa buu ana agiro u Samariya tizee ta Asere.
Baada ya Petro na Yohane kutoa ushuhuda wao na kuutangaza ujumbe wa Bwana, walirudi Yerusalemu. Walipokuwa wanarudi walihubiri Habari Njema katika vijiji vingi vya Samaria.
26 Bire bibee bika dura ka Asere bigun Filibus, hira tarsa ni kira nu kudu una Ujerusalem u hana ugaza (una ubikiki bine).
Malaika wa Bwana alimwambia Filipo, “Jitayarishe uende kusini kupitia njia inayotoka Yerusalemu kwenda Gaza.” (Njia hiyo hupita jangwani.)
27 Ma hiri ma dusa. uru naa katuma a kura usarauniya wani Itopiya sa maaye Ujerusalem bati ma wuzi Ugomo Asere rinonzo.
Basi, Filipo akajiweka tayari, akaanza safari. Wakati huohuo kulikuwa na Mwethiopia mmoja, towashi, ambaye alikuwa anasafiri kuelekea nyumbani. Huyo mtu alikuwa ofisa maarufu wa hazina ya Kandake, malkia wa Ethiopia. Alikuwa amekwenda huko Yerusalemu kuabudu na wakati huo alikuwa anarudi akiwa amepanda gari la kukokotwa.
28 Tantu kuro ma ciki unu hira citi zee ti Tshaya unu kurzo utize ta Asere.
Alipokuwa anasafiri, alikuwa akijisomea kitabu cha nabii Isaya.
29 Bibee bi gun Filibus hana ka benki unu ugenemee.
Basi, Roho Mtakatifu akamwambia Filipo, “Nenda karibu na gari hilo ukafuatane nalo.”
30 Filibus maka kem me unu hira uti Ishaya una tizee ta Asere.
Filipo akakimbilia karibu na gari, akamsikia huyo mtu akisoma katika kitabu cha nabii Isaya. Hapo Filipo akamwuliza, “Je, unaelewa hayo unayosoma?”
31 Indi wuu ani in russi sarki uye sa madiu benkum, aye benkum.
Huyo mtu akamjibu, “Ninawezaje kuelewa bila mtu kunielewesha?” Hapo akamwalika Filipo apande juu, aketi pamoja naye.
32 A hira me sa unu Itopiya maazi unu hirame, a gusa, A hunge mee kassi bitan tantu kaweki nan bizara in ku tikmee sarki u buku tizee.
Basi, sehemu ya Maandiko Matakatifu aliyokuwa anasoma ilikuwa hii: “Alikuwa kama kondoo anayepelekwa kuchinjwa; kimya kama vile mwana kondoo anaponyolewa manyoya, yeye naye hakutoa sauti hata kidogo.
33 A nyumo u yomomee sa wawuza me wacekimee, aveni madi buki uchara umemee, sa a hunamee unee.
Alifedheheshwa na kunyimwa haki. Hakuna atakayeweza kuongea juu ya kizazi chake, kwa maana maisha yake yameondolewa duniani.”
34 Uchukorome ma iki Filibus ma gu kussu, unu kurzo utizee mee mazin anice numee nan ni uyee.
Huyo Mwethiopia akamwambia Filipo, “Niambie, huyu nabii anasema juu ya nani? Anasema mambo haya juu yake yeye mwenyewe au juu ya mtu mwingine?”
35 Filibus ma tubimee tizee ti Yesu unyertike u Ishaya.
Basi, Filipo akianzia na sehemu hiyo ya Maandiko Matakatifu, akamweleza Habari Njema juu ya Yesu.
36 Wa haki unaa wa wa eh a hira mare mei uchokoromee ma gunnme nyanini idi karti a zoron abamee.
Walipokuwa bado wanaendelea na safari walifika mahali penye maji na huyo ofisa akasema, “Mahali hapa pana maji; je, kuna chochote cha kunizuia nisibatizwe?”
37 Inki wa hem anyumo iriba iwemee adi zorowee, ma gu ma hem Yesu Kirsti vana Asere mani.
Filipo akasema, “Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Naye akajibu, “Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.”
38 U nani Itopiya me ma turi kubakura mee, wa dusa na Filibus me maka Zoromee.
Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame; na wote wawili, Filipo na huyo ofisa wakashuka majini, naye Filipo akambatiza.
39 Sa wa suro anyumo a mei mee bibee ba Asere biziki Filibus uchokorome ma nyarimee daki ma iramee, ma dusa ma meki unaa inninonzo.
Walipotoka majini Roho wa Bwana akamfanya Filipo atoweke. Na huyo Mwethiopia hakumwona tena; lakini akaendelea na safari yake akiwa amejaa furaha.
40 Filibus maka suro Azotus, mari aje unu boo ukadura ku runta ati pinpin to watu me chip uka biki casariya.
Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri Habari Njema mpaka alipofika Kaisarea.