< תהילים 41 >

למנצח מזמור לדוד אשרי משכיל אל דל ביום רעה ימלטהו יהוה׃ 1
Amebarikiwa mtu yule amkumbukaye mnyonge; katika siku ya taabu, Yahwe atamuokoa.
יהוה ישמרהו ויחיהו יאשר בארץ ואל תתנהו בנפש איביו׃ 2
Yahwe atamuhifadhi na kumuweka hai, naye atabarikiwa duniani; Yahwe hata mrudisha kwenye mapenzi ya adui zake.
יהוה יסעדנו על ערש דוי כל משכבו הפכת בחליו׃ 3
Awapo kwenye kitanda cha mateso Yahwe atamsaidia; nawe utakifanya kitanda cha ugonjwa kuwa kitanda cha uponyaji.
אני אמרתי יהוה חנני רפאה נפשי כי חטאתי לך׃ 4
Nami nilisema, “Yahwe unihurumie! Uniponye, kwa maana nimekutenda dhambi wewe.”
אויבי יאמרו רע לי מתי ימות ואבד שמו׃ 5
Adui zangu huongea maovu dhidi yangu, wakisema, 'Atakufa lini na jina lake lipotee?'
ואם בא לראות שוא ידבר לבו יקבץ און לו יצא לחוץ ידבר׃ 6
Adui yangu ajapo kuniona, huongea mambo yasiyo na maana; moyo wake hukusanya maafa yangu kwa ajili yake mwenyewe; na aondokapo kwangu, yeye huwaambia watu wengine kuhusu hayo.
יחד עלי יתלחשו כל שנאי עלי יחשבו רעה לי׃ 7
Wale wote wanaonichukia kwa pamoja hunon'gona dhidi yangu; nao wanafarijika kwa ajili ya maumivu yangu.
דבר בליעל יצוק בו ואשר שכב לא יוסיף לקום׃ 8
Wakisema, “Gonjwa baya limemshikilia yeye haswa; na sasa kuwa amelala kitandani, hatainuka kamwe.”
גם איש שלומי אשר בטחתי בו אוכל לחמי הגדיל עלי עקב׃ 9
Kweli, hata rafiki yangu wa karibu, ambae nilimuamini, aliye kula mkate wangu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.
ואתה יהוה חנני והקימני ואשלמה להם׃ 10
Bali wewe, Yahwe, unihurumie na uniinue ili kwamba niwalipizie kisasi.
בזאת ידעתי כי חפצת בי כי לא יריע איבי עלי׃ 11
Na hivi nitajua kuwa unafurahishwa nami, kwa kuwa adui yangu hatafurahia kunishinda.
ואני בתמי תמכת בי ותציבני לפניך לעולם׃ 12
Kwangu mimi, wewe unanisaidia katika uadilifu wangu na utaniweka mbele ya uso wako milele.
ברוך יהוה אלהי ישראל מהעולם ועד העולם אמן ואמן׃ 13
Yahwe, Mungu wa Israeli asifiwe milele na milele. Amen na Amen. Kitabu ya Pili

< תהילים 41 >