< תהילים 24 >

לדוד מזמור ליהוה הארץ ומלואה תבל וישבי בה׃ 1
Nchi ni ya Yahwe, na vyote viijazavyo, dunia, na wote wakaao ndani yake.
כי הוא על ימים יסדה ועל נהרות יכוננה׃ 2
Kwa kuwa yeye aliianzisha juu ya bahari na kuiimarisha juu ya mito.
מי יעלה בהר יהוה ומי יקום במקום קדשו׃ 3
Ni nani atakaye panda mlima wa Yahwe? Ni nani atakaye simama patakatifu pake?
נקי כפים ובר לבב אשר לא נשא לשוא נפשי ולא נשבע למרמה׃ 4
Yeye ambaye ana mikono misafi na moyo safi; ambaye hajauinua uongo, na haja apa kiapo ili kudanganya.
ישא ברכה מאת יהוה וצדקה מאלהי ישעו׃ 5
Yeye atapokea baraka kutoka kwa Yahwe na haki kutoka kwa Mungu wa wokovu wake.
זה דור דרשו מבקשי פניך יעקב סלה׃ 6
Kizazi cha wale wamtafutao Mungu ni kama hiki, wale ambao wanautafuta uso wa Mungu wa Yakobo.
שאו שערים ראשיכם והנשאו פתחי עולם ויבוא מלך הכבוד׃ 7
Inueni vichwa vyenu, ninyi malango; muinuliwe juu, milango ya milango ya kudumu, ili kwamba Mfalme wa utukufu aweze kuingia!
מי זה מלך הכבוד יהוה עזוז וגבור יהוה גבור מלחמה׃ 8
Huyu Mfalme wa utukufu ni nani? Yahwe, mwenye nguvu na uweza; Yahwe, mwenye uweza katika vita.
שאו שערים ראשיכם ושאו פתחי עולם ויבא מלך הכבוד׃ 9
Inueni vichwa vyenu, ninyi malango; muinuliwe juu, milango ya kudumu, ili kwamba Mfalme wa utukufu aweze kuingia!
מי הוא זה מלך הכבוד יהוה צבאות הוא מלך הכבוד סלה׃ 10
Huyu Mfalme wa utukufu ni nani? Yahwe wa majeshi, yeye ni Mfalme wa utukufu.

< תהילים 24 >