< יחזקאל 38 >
ויהי דבר יהוה אלי לאמר׃ | 1 |
Neno la Yahwe likanijia, likisema,
בן אדם שים פניך אל גוג ארץ המגוג נשיא ראש משך ותבל והנבא עליו׃ | 2 |
“Mwanadamu, weka uso wako kumwelekea Gogu, nchi ya Magogu, kiongozi mkuu wa Mesheki na Tubali; na kutabiri dhidi yake.
ואמרת כה אמר אדני יהוה הנני אליך גוג נשיא ראש משך ותבל׃ | 3 |
Sema, 'Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako, Gogu, kiongozi mkuu wa Mesheki na Tubali.
ושובבתיך ונתתי חחים בלחייך והוצאתי אותך ואת כל חילך סוסים ופרשים לבשי מכלול כלם קהל רב צנה ומגן תפשי חרבות כלם׃ | 4 |
Hivyo nitakugeuza na kuweka kulabu kwenye taya yako; nitakupeleka nje pamoja na jeshi lako lote, farasi, na waendesha farasi, wote wakiwa wamevaa silaha, kusanyiko kubwa pamoja na ngao ndogo na ngao kubwa, wote wakishikilia panga!
פרס כוש ופוט אתם כלם מגן וכובע׃ | 5 |
Persia, Kushi, Uajemi wapo pamoja nao, wote pamoja na ngao na chapeo!
גמר וכל אגפיה בית תוגרמה ירכתי צפון ואת כל אגפיו עמים רבים אתך׃ | 6 |
Gomeri na jeshi lake lote, na Beth-Togarma, kutoka sehemu za mbali ya kaskazini, na jeshi lake lote! Watu wengi wako pamoja nawe!
הכן והכן לך אתה וכל קהלך הנקהלים עליך והיית להם למשמר׃ | 7 |
Kuwa tayari! Ndio, jiandae na jeshi lako waliokusanyika pamoja na wewe, na amiri wao mkuu.
מימים רבים תפקד באחרית השנים תבוא אל ארץ משובבת מחרב מקבצת מעמים רבים על הרי ישראל אשר היו לחרבה תמיד והיא מעמים הוצאה וישבו לבטח כלם׃ | 8 |
Utaitwa baada ya siku nyingi, na baada ya miaka michache utaenda kwenye nchi iliyofunikwa kutoka upanga na ambayo iliyokusanywa kutoka watu wengi, iliyowkusanya kuwarudisha milima ya Israeli ambayo imeendelea kuangamizwa. Lakini watu wa nchi watatolewa na kabila za watu, na wataishi salama, wote!
ועלית כשאה תבוא כענן לכסות הארץ תהיה אתה וכל אגפיך ועמים רבים אותך׃ | 9 |
Hivyo utapanda juu kama tufani iendavyo; utakuwa kama wingu lililofunika nchi, wewe na jeshi lako lote, maaskari wako wote pamoja na wewe.
כה אמר אדני יהוה והיה ביום ההוא יעלו דברים על לבבך וחשבת מחשבת רעה׃ | 10 |
Bwana Yahwe asema hivi: Itakuwa siku hiyo hayo mawazo yataingia moyoni mwako, na utatunga njama mbaya.'
ואמרת אעלה על ארץ פרזות אבוא השקטים ישבי לבטח כלם ישבים באין חומה ובריח ודלתים אין להם׃ | 11 |
Kisha utasema, 'nitapanda hata nchi iliyowazi; nitaenda hata kwa watu wapole waishio salama, wote wakiishi mahali ambapo hakuna kuta wala makomeo, na mahali ambapo hakuna malango ya mji.
לשלל שלל ולבז בז להשיב ידך על חרבות נושבת ואל עם מאסף מגוים עשה מקנה וקנין ישבי על טבור הארץ׃ | 12 |
Nitanyakua mateka na kuiba mateka, ili nilete mkono wangu juu kuwaangamiza wale wakazi wapya, na juu ya watu waliokusanyika kutoka mataifa, watu wale waongezao wanyama na mali, na wale waishio katikatika ya dunia.'
שבא ודדן וסחרי תרשיש וכל כפריה יאמרו לך הלשלל שלל אתה בא הלבז בז הקהלת קהלך לשאת כסף וזהב לקחת מקנה וקנין לשלל שלל גדול׃ | 13 |
Sheba na Denani, na wafanya biashara wa Tarshishi pamoja na mahodari wake wote watakwambia, 'Je, umekuja kuteka nyara? Je, umewakusanya majeshi yako kuchukua mateka, kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua mifugo yao na mali na kuwakokota mateka wengi sana?'
לכן הנבא בן אדם ואמרת לגוג כה אמר אדני יהוה הלוא ביום ההוא בשבת עמי ישראל לבטח תדע׃ | 14 |
Kwa hiyo tabiri, mwanadamu, na mwambie Gogu, 'Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku hiyo, wakati watu wangu Israeli watakapoishi salama, je, hutajifunza kuhusu wao?
ובאת ממקומך מירכתי צפון אתה ועמים רבים אתך רכבי סוסים כלם קהל גדול וחיל רב׃ | 15 |
Utakuja kutoka mahali pangu mbali katika kaskazini pamoja na jeshi kubwa, wote wakiendesha farasi, kusanyiko kubwa, jeshi kubwa.
ועלית על עמי ישראל כענן לכסות הארץ באחרית הימים תהיה והבאותיך על ארצי למען דעת הגוים אתי בהקדשי בך לעיניהם גוג׃ | 16 |
Utawashambulia watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Katika siku za baadaye nitakuleta juu ya nchi yangu, ili mataifa wanijue nitakapojifunua mwenyewe kupitia wewe, Gogu, kuwa mtakatifu mbele ya macho yao.
כה אמר אדני יהוה האתה הוא אשר דברתי בימים קדמונים ביד עבדי נביאי ישראל הנבאים בימים ההם שנים להביא אתך עליהם׃ | 17 |
Bwana Yahwe asema hivi: Je, wewe siye yule ambaye niliyeongea naye katika siku za zamani kwa mkono wa watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri katika mda wao wenyewe kwa miaka niliyowaleta juu yao?
והיה ביום ההוא ביום בוא גוג על אדמת ישראל נאם אדני יהוה תעלה חמתי באפי׃ | 18 |
Basi itakuwa katika siku hiyo wakati Gogu atakapo ishambulia nchi ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-ghadhabu yangu itapanda katika hasira yangu.
ובקנאתי באש עברתי דברתי אם לא ביום ההוא יהיה רעש גדול על אדמת ישראל׃ | 19 |
Katika wivu wangu katika hasira ya moto wangu, ninasema kwamba katika siku hiyo kutakuwa na tetemeko kubwa la nchi katika nchi ya Israeli.
ורעשו מפני דגי הים ועוף השמים וחית השדה וכל הרמש הרמש על האדמה וכל האדם אשר על פני האדמה ונהרסו ההרים ונפלו המדרגות וכל חומה לארץ תפול׃ | 20 |
Watatetemeka mbele yangu-samaki wa baharini na ndege wa angani, wanyama wa mashambani, na viumbe watambaao juu ya nchi, na kila mtu aliyeko juu ya uso wa nchi. Milima itaangushwa chini majabali yataanguka, hadi kila ukuta utaanguka kwenye nchi.
וקראתי עליו לכל הרי חרב נאם אדני יהוה חרב איש באחיו תהיה׃ | 21 |
Nitaita upanga dhidi yake juu ya milima yangu yote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-upanga wa kila mtu utakuwa kinyume na ndugu yake.
ונשפטתי אתו בדבר ובדם וגשם שוטף ואבני אלגביש אש וגפרית אמטיר עליו ועל אגפיו ועל עמים רבים אשר אתו׃ | 22 |
Kisha nitamuhukumu kwa tauni na damu; nakufurika mvua na mvua ya mawe na kuchoma asidi nitainyeshea chini juu yake na jeshi lake na mataifa mengi yaliyo pamoja naye.
והתגדלתי והתקדשתי ונודעתי לעיני גוים רבים וידעו כי אני יהוה׃ | 23 |
Kwa kuwa nitaonyesha ukuu wangu na utakatifu wangu na nitafanya kujulikana mimi mwenyewe katiaka macho ya mataifa mengi, na watajua kwamba mimi ni Yahwe.”