< 1 Corinthians 12 >

1 And concerning the spiritual things, brothers, I do not wish you to be ignorant;
Kuhusu karama za rohoni, kaka na dada zangu sitaki mkose kufahamu.
2 you have known that you were nations, being carried away as you were led to the mute idols;
Mwajua ya kuwa mlipokuwa wapagani mliongozwa kufuata sanamu zisizoongea, kwa njia zozote mliongozwa nazo.
3 for this reason, I give you to understand that no one, speaking in the Spirit of God, says Jesus [is] accursed, and no one is able to say Jesus [is] LORD, except in the Holy Spirit.
Kwa hiyo, nataka mfahamu kwamba hakuna yeyote anenaye kwa Roho wa Mungu akisema, “Yesu amelaaniwa.” Hakuna yeyote atakayesema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa katika Roho Mtakatifu.
4 And there are diversities of gifts, and the same Spirit;
Basi kuna karama tofauti tofauti, bali Roho ni yeye yule.
5 and there are diversities of ministries, and the same Lord;
Na kuna huduma tofauti tofauti, bali Bwana ni yeye yule.
6 and there are diversities of workings, and it is the same God—who is working all in all.
Na kuna aina mbalimbali za kazi, lakini Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
7 And to each has been given the manifestation of the Spirit for profit;
Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote.
8 for to one through the Spirit has been given a word of wisdom, and to another a word of knowledge, according to the same Spirit;
Maana mtu mmoja amepewa na Roho neno la hekima, na mwingine neno la maarifa kwa Roho yule yule.
9 and to another faith in the same Spirit, and to another gifts of healings in the same Spirit;
Kwa mwingine humpa imani kwa Roho yeye yule, na kwa mwingine karama ya uponyaji kwa Roho mmoja.
10 and to another in-workings of mighty deeds; and to another prophecy; and to another discernings of spirits; and to another [various] kinds of tongues; and to another interpretation of tongues:
Kwa mwingine matendo ya nguvu, na mwingine unabii. Na kwa mwingine uwezo wa kupambanua roho, mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingnine tafsiri za lugha.
11 and the one and the same Spirit works all these, dividing to each individually as He intends.
Lakini Roho ni yule yule atendaye kazi hizi zote, kumpa kila mtu karama kwa kadiri ya uchaguzi wake mwenyewe.
12 For even as the body is one, and has many members, and all the members of the one body, being many, are one body, so also [is] the Christ,
Kwa maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote ni vya mwili ule ule, vivyo hivyo na Kristo.
13 for also in one Spirit we were all immersed into one body, whether Jews or Greeks, whether servants or freemen, and all were made to drink one Spirit,
Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi au Wayunani, kwamba tu watumwa au huru, na wote tulinyweshwa Roho mmoja.
14 for also the body is not one member, but many.
Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.
15 If the foot may say, “Because I am not a hand, I am not of the body,” is it not, because of this, not of the body?
Ikiwa mguu utasema, “kwa kuwa mimi si mkono, mimi si sehemu ya mwili,” hiyo haiufanyi kutokuwa sehemu ya mwili.
16 And if the ear may say, “Because I am not an eye, I am not of the body,” is it not, because of this, not of the body?
Na ikiwa sikio litasema, “kwa kuwa mimi si jicho, mimi si sehemu ya mwili,” hiyo hailifanyi kutokuwa sehemu ya mwili.
17 If the whole body [were] an eye, where the hearing? If the whole hearing, where the smelling?
Kama mwili wote utakuwa jicho, kungekuwa wapi kusikia? Kama mwili wote ukiwa sikio, kungekuwa wapi kunusa?
18 And now, God set the members, each one of them in the body, according as He willed,
Lakini Mungu aliweka kila kiungo cha mwili mahali pake kama alivyopanga mwenyewe.
19 and if all were one member, where [is] the body?
Na kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?
20 And now, indeed, [are] many members, but one body;
Hivyo sasa viungo ni vingi, lakini mwili ni mmoja.
21 and an eye is not able to say to the hand, “I have no need of you”; nor again the head to the feet, “I have no need of you.”
Jicho haliwezi kuuambia mkono, “sina haja na wewe.” Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, sina haja na ninyi.”
22 But much more the members of the body seeming to be weaker are necessary,
Lakini viungo vya mwili vinavyoonekana kuwa na heshima kidogo vyahitajika zaidi.
23 and those that we think to be less honorable of the body, around these we put more abundant honor, and our unseemly things have more abundant seemliness,
Na viungo vya mwili tunavyodhani vina heshima kidogo, twavipa heshima zaidi, na viungo vyetu visivyo na mvuto vina uzuri zaidi.
24 and our seemly things have no need; but God tempered the body together, having given more abundant honor to the lacking part,
Na sasa viungo vyetu vilivyo na mvuto havina haja ya kupewa heshima, kwa kuwa tayari vina heshima. Lakini Mungu ameviunganisha viungo vyote pamoja, na amevipa heshima zaidi vile visivyo heshimiwa.
25 that there may be no division in the body, but that the members may have the same anxiety for one another,
Alifanya hivyo ili pasiwepo mgawanyiko katika mwili, bali viungo vyote vitunzane kwa upendo wa mmoja.
26 and whether one member suffers, all the members suffer with [it], or one member is glorified, all the members rejoice with [it];
Na wakati kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote vyaumia kwa pamoja. Au wakati kiungo kimoja kikiheshimiwa, viungo vyote vifurahi kwa pamoja.
27 and you are the body of Christ, and members in particular.
Sasa ninyi ni mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.
28 And some, indeed, God set in the Assembly: first apostles, secondly prophets, thirdly teachers, afterward powers, afterward gifts of healings, helpings, governings, various kinds of tongues.
Na Mungu ameweka katika kanisa kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu, kisha wale wote watendao matendo makuu, kisha karama za uponyaji, wale wasaidiao, wale wafanyao kazi ya kuongoza, na wote walio na aina mbalimbali za lugha.
29 [Are] all apostles? [Are] all prophets? [Are] all teachers? [Are] all powers?
Je sisi sote ni mitume? Sisi sote ni manabii? Sisi sote ni waalimu? Je sisi sote tunafanya matendo ya miujiza?
30 [Do] all have gifts of healings? Do all speak with tongues? Do all interpret?
Je sisi sote tuna karama ya uponyaji? Sisi sote tunaongea kwa lugha? Sisi sote tunatafsiri lugha?
31 And earnestly desire the better gifts; and yet I show to you a far [more] excelling way:
Tafuteni sana karama zilizo kuu. Nami nitawaonesha njia iliyo bora zaidi.

< 1 Corinthians 12 >