< 馬可福音 5 >
Walikuja mpaka upande mwingine wa bahari, katika mkoa wa Gerasi
2 耶穌一下船,即刻有一個附邪魔的人,從墳墓裏出來,迎著他走來,
Na ghafla wakati Yesu alipokuwa akitoka nje ya mtumbwi, mtu mwenye roho chafu alikuja kwake kutoka makaburini.
3 原來那人居住在墳墓裏,再沒有人能捆住他,就是用鎖鍊也不能,
Mtu huyu aliishi makaburini. Hakuna aliyeweza kumzuia zaidi, hakuna hata kwa minyororo.
4 因為人屢次用腳鐐和鎖鍊將他捆縛,他卻將鎖鍊掙斷,將腳鐐弄碎,沒有人能制服他。
Alikuwa amefungwa nyakati nyingi kwa pingu na minyororo. Aliikata minyororo na pingu zake zilivunjwa. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na nguvu za kumshinda.
Usiku na mchana akiwa makaburini na milimani, alilia na kujikata yeye mwenyewe kwa mawe makali.
Alipomwona Yesu kwa mbali, alikimbilia kwake na kuinama mbele yake.
7 大聲喊說:「至高天主之子耶穌,我與你有什麼相干﹖我因著天主誓求你,不要苦害我!」
Alilia kwa sauti kuu, “Wataka nikufanyie nini, Yesu, Mwana wa Mungu aliye Juu sana? Ninakusihi kwa Mungu mwenyewe, usinitese.”
Kwa kuwa alikuwa amemwambia, “Mtoke mtu huyu, wewe roho mchafu.”
9 耶穌問他說:「你名叫什麼﹖」他回答說:「我名叫『軍旅』,因為我們眾多。」
Naye alimwuliza, “Jina lako ni nani?” Naye alimjibu, “Jina langu ni Legion, kwa kuwa tuko wengi.”
Alimsihi tena na tena asiwapeleke nje ya mkoa.
Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likilishwa juu ya kilima,
12 他們懇求耶穌說:「請打發我們到那豬群,好讓我們進入牠們內。」
nao walimsihi, wakisema, “Tutume kwa nguruwe; tuingie ndani yao.”
13 耶穌准許了他們;邪魔就出來,進入了豬內。那群豬約有二千,便從山崖上直衝到海裏,在海裏淹死了。
Hivyo aliwaruhusu; roho wachafu waliwatoka na kuingia ndani ya nguruwe, nao walikimbilia chini ya kilima mpaka baharini, na karibia nguruwe elfu mbili walizama baharini.
14 放豬的人就逃去,到城裏和鄉間傳報開了;人都出來看是發生了什麼事。
Na wale waliokuwa wakiwalisha nguruwe walikimbia na kutoa taarifa ya kilichotokea katika mji na katika nchi. Ndipo watu wengi walitoka kwenda kuona kilichotokea.
15 他們來到耶穌跟前,看見那個附魔的人,即為「軍旅」所附的人,坐在那裏,穿著衣服,神志清醒,就害怕起來。
Ndipo walikuja kwa Yesu na walimwona mtu aliyepagawa na pepo—aliyekuwa na Jeshi—amekaa chini, amevikwa, na akiwa katika akili yake timamu, nao waliogopa.
16 看見的人就把附魔的人所遇到的事,和那群豬的事,都給他們逑說了。
Wale waliokuwa wameona kilichotokea kwa mtu aliyekuwa amepagawa na pepo waliwaambia kilichotokea kwake na pia kuhusu nguruwe.
Nao walianza kumsihi aondoke katika mkoa wao.
18 當耶穌上船時,那曾附過魔的人,懇求耶穌讓他同耶穌在一起。
Na alipokuwa akiingia ndani ya mtumbwi, mtu aliyekuwa amepagawa na mapepo alimsihi kwamba aende pamoja naye.
19 耶穌沒有允許他,但對他說:「你回家,到你的親屬那裏,給他們傳逑上主為你作了何等大事,怎樣憐憫了你。」
Lakini hakumruhusu, lakini alimwambia, “Nenda nyumbani kwako na kwa watu wako, na uwaambie alikufanyia Bwana, na rehema aliyokupa.”
20 那人就走了,在十城區開始傳揚耶穌為他所作的何等大事,眾人都驚奇不已。
Hivyo alienda na alianza kutangaza mambo makuu ambayo Yesu amefanya kwake katika Dekapoli, na kila mmoja alistaajabu.
21 耶穌乘船又渡回對岸,有大夥群眾聚集在他周圍;他遂留在海濱。
Na wakati Yesu alipovuka tena upande mwingine, ndani ya mtumbwi, umati mkubwa ulikusanyika kumzunguka, alipokuwa kando ya bahari.
22 那時,來了一個會堂長名叫雅依洛,一見耶穌,就跪伏在他腳前,
Na mmoja wa kiongozi wa sinagogi, aliyeitwa Yairo, alikuja, na alipomwona, alianguka miguuni pake.
23 懇切求他說:「我的小女兒快要死了,請你來,給他覆手,叫她得救回生。」
Akamsihi zaidi na zaidi, akisema, “Binti yangu mdogo anakaribia kufa. Ninakusihi, njoo na uweke mikono yako juu yake ili kwamba aweze kupata afya na kuishi.”
24 耶穌就同他去了。有一大群人跟隨著他,擁擠著他。
Hivyo alikwenda pamoja naye, na umati mkubwa ulimfuata nao walimzonga karibu wakimzunguka.
Kulikuwa na mwanamke ambaye damu yake ilikuwa imetoka kwa miaka kumi na miwili.
26 她在許多醫生手裏,受了許多痛苦,花盡了自己所有的一切,不但沒有見效,反而病勢更加重了。
Aliteseka vya kutosha chini ya matabibu wengi na alitumia kila kitu alichokuwa nacho. Hata hivyo hakusaidika kwa chochote, lakini badala yake alizidi kuwa na hali mbaya.
27 她聽了有關耶穌的傳說,便來到人群中,從後邊摸了耶穌的衣裳,
Alisikia habari kuhusu Yesu. Hivyo alikuja nyuma yake wakati alipokuwa akitembea ndani ya umati, naye aliligusa vazi lake.
28 因為她心裏想:「我只要一摸他的衣裳,必然會好的。」
Kwa kuwa alisema, “Kama nikiyagusa mavazi yake tu, nitakuwa mzima.”
29 她的血源立刻涸竭了,並且覺得身上的疾病也好了。
Alipomgusa, kutokwa damu kulikoma, na alijisikia katika mwili wake kwamba aliponywa kutoka kwenye mateso yake.
30 耶穌立時覺得有一種能力從自己身上出去,就在人群中回過頭來說:「誰摸了我的衣裳﹖」
Na ghafla Yesu aligundua ndani yake mwenyewe kwamba nguvu zimemtoka. Na aligeuka huku na huku katika umati wa watu na kuuliza, “Ni nani aliyeligusa vazi langu?”
31 他的門徒向他說:「你看! 群眾四面擁擠著你,你還問:誰摸了我﹖」
Wanafunzi wake walimwambia, “Unaona umati huu umekusonga ukikuzunguka, nawe wasema, 'Ni nani aliyenigusa?'”
Lakini Yesu alitazama huku na huku kuona ambaye aliyekuwa amefanya hili.
33 那婦人明知在自己身上所成的事,就戰戰兢兢地前來,跪伏在耶穌前,把實情完全告訴他。
Mwanamke, akijua kilichotokea kwake, aliogopa na kutetemeka. Alikuja na alianguka chini mbele yake na kumwambia ukweli wote.
34 耶穌便向他她說:「女兒,你的信德救了你,平安去罷! 你的疾病必得痊癒!」
Alisema kwake, “Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa amani na uponywe kutoka kwenye ugonjwa wako.”
35 他還說話的時候,有人從會堂長家裏來,說:「你的女兒死了,你還來煩勞師傅做什麼﹖」
Alipokuwa akizungumza, baadhi ya watu walikuja kutoka kwa kiongozi wa Sinagogi, wakisema, “Binti yako amekufa. Kwa nini kuendelea kumsumbua mwalimu?”
36 耶穌聽所說的話,就給會堂長說:「不要怕,祇管信。」
Lakini Yesu aliposikia ambacho walikisema, alimwambia kiongozi wa Sinagogi, “Usiogope. Amini tu.”
37 除伯多祿、雅各伯和雅各伯的弟弟若望外,他沒有讓任何人跟他去。
Hakumruhusu yeyote kuongozana naye, isipokuwa Petro, Yakobo, na Yohana, ndugu yake Yakobo.
38 他們到了會堂長的家裏,耶穌看見群眾非常喧噪:有的哭泣,有的哀號,
Walikuja nyumbani kwa kiongozi wa Sinagogi naye aliona vurugu, kulia kwingi na kuomboleza.
39 便進去,給他們說:「你們為什麼喧噪哭泣呢﹖小女孩並沒有死, 祇是睡著了!」
Alipoingia nyumbani, aliwaambia, “Kwa nini mmesikitika na kwa nini mnalia? Mtoto hajafa bali amelala.”
40 他們都譏笑他。他卻把眾人趕出去,帶著小女孩的父親和母親,及同他在一起的人,進了小女孩所在的地方。
Walimcheka, lakini yeye, aliwatoa wote nje, alimchukua baba wa mtoto na mama na wale waliokuwa pamoja naye, na aliingia ndani alimokuwa mtoto.
41 他拿起小女孩的手,對她說:「塔里塔,古木!」意思是:「女孩子,我命妳起來!」
Aliuchukua mkono wa mtoto na alimwambia, “Talitha koum,” ambayo ni kusema, “Binti mdogo, nakuambia, amka.”
42 那女孩子就立刻起來行走,原來她已十二歲了;他們都驚訝得目瞪口呆。
Ghafla mtoto aliamka na kutembea (kwa kuwa alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili). Na ghafla walishikwa na mshangao mkubwa.
43 耶穌卻嚴厲命令他們,不要叫任何人知道這件事;又吩咐給女孩子吃的。
Aliwaamuru kwa nguvu kwamba hakuna yeyote anapaswa kujua kuhusu hili. Na aliwaambia wampatie yule binti chakula.