< 馬可福音 2 >

1 過了一些日子,耶穌又進了葛法翁,人聽說他在家裏,
Aliporudi Kaperinaumu baada ya siku chache, ilisikika kwamba alikuwa nyumbani.
2 就聚來了許多人,以致連門前也不能再容納,他就對他們講道。
Watu wengi sana walikuwa wamekusanyika pale na haikuwepo nafasi tena, hata ile ya pale mlangoni, na Yesu alisema neno kwao.
3 那時,有人帶著一個癱子到他這裏來,由四個人抬著;
Kisha baadhi ya watu walikuja kwake waliomleta mtu aliyekuwa amepooza; watu wanne walikuwa wamembeba.
4 但因為人眾多,不能送到面前,就在耶穌所在之處,拆開了房頂;拆穿之後,把床縋下去,癱子在上面躺著。
Wakati waliposhindwa kumkaribia kwa sababu ya umati wa watu, waliondoa paa juu ya mahali pale alipokuwa. Na walipokuwa wamekwishatoboa tundu, walishusha kitanda ambacho mtu aliyepooza alikuwa amelala.
5 耶穌一見他們的信心,就對癱子說:「孩子! 你的罪赦了。」
Alipoiona imani yao, Yesu alimwambia mtu aliyepooza, “mwanangu, dhambi zako zimesamehewa.”
6 那時,有幾個經師坐在那裏,心裏忖度說:「
Lakini baadhi ya waandishi wale waliokuwa wamekaa pale walijihoji mioyoni mwao,
7 怎麼這人這樣說話呢﹖他說了褻瀆的話;除了天主一個外,誰能赦罪呢﹖」
“Anawezaje mtu huyu kusema hivi? Anakufuru! Nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”
8 耶穌憑自己的神力,即刻認透了他們私自這樣忖度,遂向他們說:「你們心中為什麼這樣忖度呢﹖
Mara Yesu alijua rohoni mwake walichokuwa wakifikiri miongoni mwao wenyewe. Aliwaambia, “Kwa nini mnafikiri hivi mioyoni mwenu?
9 什麼比較容易呢﹖是對癱子說:你們的罪赦了;還是說:起來,拿你的床走﹖
Lipi ni jepesi zaidi kusema kwa mtu aliyepooza, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema 'Simama, chukua kitanda chako, na utembee?'
10 但為叫你們知道:人子在地上有權柄赦罪──遂對癱子說:
Lakini ili wapate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka ya kusamehe dhambi katika dunia, alimwambia yule aliyepooza,
11 我給你說:起來,拿你的床,回家去罷!」
“Nakuambia wewe, inuka, chukua mkeka wako, na uende nyumbani kwako.”
12 那人遂起來,立刻拿起床,當著眾人的面走出去了,以致眾人大為驚愕,遂光榮天主說:「我們從未見過這樣的事!」
Alisimama na mara moja akachukua mkeka wake, na alikwenda nje ya nyumba mbele ya kila mtu, hivyo wote walishangaa na walimpa Mungu utukufu, na wakasema “Kamwe, hatujawahi kuona jambo kama hili.”
13 耶穌又出去,到了海邊,群眾都到他跟,前他便教訓他們。
Alienda tena kando ya ziwa, na umati wote wa watu walikuja kwake, na akawafundisha.
14 當他前行時,看見阿耳斐的兒子肋未坐在稅關上,便向他說:「你跟隨我罷!」肋未就起來跟隨了耶穌。
Alipokuwa akipita alimwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi kwenye sehemu ya kukusanyia kodi na akamwambia, “Nifuate.” Alisimama na kumfuata.
15 當耶穌在肋未家中坐席的時候,有許多稅吏和罪人,也與耶穌和他的門徒一起坐席,因為己有許多人跟隨了他。
Na wakati Yesu alipokuwa akipata chakula katika nyumba ya Lawi, wakusanya kodi wengi na watu wenye dhambi walikuwa wakila na Yesu na wanafunzi wake, kwa kuwa walikuwa wengi nao walimfuata.
16 法利賽黨的經師看見耶穌與罪人和稅吏一起吃飯,就對他的門徒說:「怎麼,他與罪人和稅吏一起吃喝﹖」
Wakati waandishi, ambao walikuwa Mafarisayo, walipoona kwamba Yesu alikuwa akila na watu wenye dhambi na wakusanya kodi, waliwaambia wanafunzi wake, “Kwa nini anakula na wakusanya kodi na watu wenye dhambi?”
17 耶穌聽了,就對他們說:「不是健康的人需要醫生,而是有病的人;我不是來召義人,而是召罪人。」
Wakati Yesu aliposikia hivi aliwaambia, “Watu walio na afya katika mwili hawamhitaji tabibu; ni watu wagonjwa pekee ndio wanamhitaji. Sikuja kuwaita watu wenye haki, lakini watu wenye dhambi.”
18 當時,若翰的門徒和法利賽人正在禁食。有人來向耶耶穌說:「為什麼若翰的門徒和法利賽人的門徒禁食,而你的門徒卻不禁食呢﹖」
Wanafunzi wa Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Na baadhi ya watu walikuja kwake na kumwambia, “Kwa nini wanafunzi wa Yohana na mafarisayo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?
19 耶穌對他們說:「伴郎豈能在新郎還與他們在一起的時候禁食﹖他們與新郎在一起的時候,決不能禁食。
Yesu aliwaambia, “Je waliohudhuria harusini wanaweza kufunga wakati bwana harusi bado akiwa pamoja nao? Kwa vyovyote bwana harusi akiwa bado yuko pamoja nao hawawezi kufunga.”
20 但日子將要來到:當新郎從他們中被劫去時,在那一天,他們就要禁食了。
Lakini siku zitakuja wakati bwana harusi atakapoondolewa kwao, na katika siku hizo wao watafunga.
21 沒有人將未漂過的布補在舊衣服上的;不然,補上的那一塊新布要扯裂了舊的,破, 綻就更加壞了。
Hakuna mtu ashonaye kipande kipya cha nguo kwenye vazi kuukuu, vinginevyo kiraka kitabanduka kutoka katika hilo, kipya kubanduka kutoka katika kikuukuu, na kutakuwepo mpasuko mbaya.
22 也沒有人把酒裝在舊皮囊裏的;不然酒漲破了皮囊,酒和皮囊都喪失了;而是新酒應裝在新皮囊裏。」
Hakuna mtu atiaye divai mpya katika viriba vikuukuu, vinginevyo divai itavipasua viriba na vyote viwili divai na viriba vitapotea. Badala yake, weka divai mpya katika viriba vipya.”
23 有一次,正當安息日,耶穌從麥田裏路過,他的門徒在行路時掐食起麥罄來。
Katika siku ya Sabato Yesu alipita kwenye baadhi ya mashamba, na wanafunzi wake walianza kuchukua baadhi ya masuke ya ngano.
24 法利賽人向耶穌說:「你看! 他們為什麼做安息日做的事﹖」
Na Mafarisayo walimwambia, “Tazama, kwa nini wanafanya kitu ambacho ni kinyume cha sheria katika siku ya Sabato?”
25 耶穌對他們說:「你們從未讀過:達味在急迫中和同他一起的人,在饑餓時所作的事嗎﹖
Aliwaambia, “Hamkusoma kile alichofanya Daudi alipokuwa katika uhitaji na njaa—yeye pamoja na watu waliokuwa pamoja naye?
26 當厄貝雅塔爾作大司祭時,達味怎樣進了天主的殿,吃了除祭司外,誰也不許吃的供餅,並且還給了同他一起的人﹖」
Jinsi alivyoenda katika nyumba ya Mungu wakati Abiathari alipokuwa kuhani mkuu na akala mkate uliowekwa mbele—ambao ilikuwa kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kula isipokuwa makuhani—na aliwapa hata baadhi ya wale waliokuwa pamoja naye?”
27 耶穌又對他們說:「安息日是為了人立的,並不是人為了安息日;
Yesu alisema, “Sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, siyo mwanadamu kwa ajili ya Sabato.
28 所以,人子也是安息日的主。」
Kwa hiyo, Mwana wa Adamu ni Bwana, hata kwa Sabato.”

< 馬可福音 2 >